Biashara ya mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo n.k)


Mkuu suluhisho ni wao wakulima kuwa katika vikundi na kuwekeana mikakati ya uuzaji wa mazao, na kingine wawe na shughuli zingine Mbadala kama Ufugaji wa kuku, Nyuki, Vikundi vya kuweka na Kukopa,
 

hakuna usanii kwenye biashara hio.ng'ombe wananuliwa minadani hasa kanda ya ziwa.
Unaweza mnunua ngombe kwa shs 200,000,kisha unamnenepesha,chakula ni mashumu ya pamba na pumba za pamba .vyakula hivi unavipata toka kwenye oilmill zilizotapakaa mwanza,shinyanga,geita,simiyu.
Ng'ombe ananenepa kwa mda wa miezi mitatu .
Ukimfikisha pugu utamuuza hadi 700,000.
Gharama ya kumlisha ng'ombe mmoja kwa mda huo haizidi laki moja.
Usafiri hadi pugu ,kuna mafuso au semi yakipeleka mizigo kanda ya ziwa au kongo yanarudi tupu .waweza kodi fuso kwa gharama haizidi laki nne,kama unang'ombe chini ya 20.
Kama una ng'ombe zaidi ya hapo unachukua semi trail au pulling ,nayo gharama haizidi laki sita.
Biashara haina cha leseni ni kibali tu na sidhani hata kama wanalipa kodi hawa jamaa.
Wakati mwingine wacomoro wanakufuata hadi sehemu unayolishia ng'ombe mnafanya biashara na yeye anapakia ng'ombe na kusepa.
Inalipa ,nimeshuhudia vijana wadogo wanazungusha mamia ya mamilioni kwenye biznes hii.ukimuona anaendesha baiskeli unamuona wakawaida wakati he is worth even 500 millions.
 
Maada endelevu kama hizi ndio zilinifanya nijiunge JF, watu wanatumia vichwa kufikiri na sio kufugia nywele. Nakiona kizazi cha wajasiria mali kinakuja kwa kasi. Mwenye data za mazao yatokanayo na mifugo zaidi ya nyama atumwagie tafadhali. Viwanda vya ngozi, kwato au utafiti wowote uliofanywa karibuni kwa hii sekta. Ninachojua Tanzania ni nchi ya tatu (3) barani afrika kwa wingi wa mifugo. Niko tayari kusahihishwa iwapo naipotosha jamii.
 

huo usanii si ndio akili yenyewe?
 
Heshima kwenu wazee wa Jukwaa hili Ikimpendeza MUNGU kuanzia Mwaka ujao nitaingia Rasmi kwenye ufugaji wa NOA na Wanyama wengine nakwakuwa mambo hayo yanahitaji MTAJI wakutosha ili kz niifanye kwa uhakika nimeona nifanye Biashara ya Mbuzi kuchukua Mikoani na kuleta DAR OMBI kwaanaejua ni MKOA upi naweza kupata MBUZI kwa Bei nzuri ikiwezekana na Bei ya kila mbuzi 1 Mpaka sasa naendelea na utafiti mdg wa SOKO la uhakika ukiacha pale VINGUNGUTI natanguliza Shukrani,,,!!!
 

Maeneo ya mkoa wa manyara kuna wafugaji wengi kama uko serious nikutafute mkuu
 
Lushoto, Korogwe pia ila msimu mzuri wakulima wawe wameishauza mazao yao yameisha utapata bei nzuri. Mifugo ndio assets au akiba yao huuzwa waklwa hawana kitu kama wametoka kuvuna mazao utapata kwa shida na bei juu. Hadi mwaka jana bei ya juu ilikuwa elfu 40 ila upate mwenyeji pia.
 
Maeneo ya mkoa wa manyara kuna wafugaji wengi kama uko serious nikutafute mkuu

Niko serious MKUU wangu ndomana nataka kujua wapi Ntawapata kwa bei nzuri Unaweza kujua huko Bei zao zikoje? nachangamoto za huko natanguliza Shukran!
 
Asante MAMA JOE! Kwa uzoefu wako unadhani nikipindi gani DEC? au? Unaweza kuwa na mtu wa Uhakika ukanielekeza kwake nijaribu kuchek nae? Km hutajali
Barikiwa ndg!
 
Kwa mwezi wa 12 soko liko UCHAGGANI, egesha mbuzi "wanono" pale Njia panda himo, Uchira na pale YMCA - moshi
usijeleta visivyonona manake ndo wanahamisha hela DSM na mikoammingineyo kupeleka kwao UCHAGGANI
 
Matola unaweza kusaidia hapa?
Natanguliza shukranj
 
Last edited by a moderator:
Niko serious MKUU wangu ndomana nataka kujua wapi Ntawapata kwa bei nzuri Unaweza kujua huko Bei zao zikoje? nachangamoto za huko natanguliza Shukran!

Mkuu kwa sasa cjafika kwenye minada muda kidogo ila kuna rafiki zangu ni wamasai na pia ni wafugaji nitawatafuta alafu nitakupa info zaidi kipindi kizuri ni kwenye kiangazi bei inakua nzuri sana changamoto ni usafiri ukiwa na usafiri wa uhakika wa kuzunguka kwenye minada nta ku pm no zangu.
 
Kwa mwezi wa 12 soko liko UCHAGGANI, egesha mbuzi "wanono" pale Njia panda himo, Uchira na pale YMCA - moshi
usijeleta visivyonona manake ndo wanahamisha hela DSM na mikoammingineyo kupeleka kwao UCHAGGANI

Asante kwa Info Kiongozi nalifanyia kz!!
 
mbuzi wapo huku shinyanga kwenye minada, price ranges btn 40-60.. uliza bei hapo vingunguti, then ni-pm # yako. we cn do

Sawa mkuu nikishakamilisha utafiti wangu ntatupia Mawacliano yangu hapa hapa Jamvini
 

pamoja sana!
 
Yoyote mwenye kutaka order ya mbuzi anipigie tufanye biashara hapahapa Dar es salaam 0714064767
 
vip mi nataka kufanya hiyo biashara,je inalipa?wapi wanapitikana na wapi soko?nilisikia kuwa pugu soko linapatikana ni kweli? naomba kwa anaefahamu anidadavulie please!
 
Habari ndugu, marafiki na jamaa!!, naomben ushauri juu ya biashara hii ya ng'ombe, mbuzi au kondoo kuhusu soko na gharama za usafiri kutoka Ruvu(pwani) hadi sokoni!!, lakin si mbaya kama kuna mfanyabiashara hiyo akashirkiana nami!!!. huwa mm nanunua kwa wafugaji na kuuza kwenye masoko ya huku porini ambayo hayana bei!!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…