Biashara ya Nafaka mtaji mkubwa faida kiduchu

Ilinishinda kwenye Michele miaka kadhaa nyuma..game tight sana kwenye biashara ya nafaka...gunia la kilo 100 linakupa faida ya 10,000 TU...ukinywa bia 5 tayari unakuwa umetafuna mtaji.....ni biashara nzuri ukiwa na diapline ..binafsi ilinishinda.
 
Circulation ndo itakupa pesa, uzoefu kazin na ukubwa wa biashara utaonekana kwa kuzingatia uzoefu wako kazini

Jamaa yangu alianza na mtaji usiofika hata 1M, sas anatengeneza profit ya 5M per single month
 
Sijui wenzangu mnafanyaje biashara lakini biashara ya nafaka ina faida tena kubwa sana kwa upande mm natoa mchele Tabora napeleka dar na zenj sikosi faida ya kuanzia 300 per kilo tena mm nanunua mchele wala sio mpunga, nanunua sembe 850 per kilo na nauza 1200 per kilo na biashara inakwenda sasa sijui wenzangu mnakwama wapi.
Wengi kwenye Biashara wanahisi kuwa na mtaji mkubwa ndio kutoboa but uzoefu+ujanja+ubunifu lazima utoboe.
Mchele mzuri bei ni
1100 -1200 per KG
Usafiri Taboara to Dar ni Tsh 100 per KG
Mabega Tsh 7 per KG
Mambo mengine cost Tsh 100
 
Mkuu biashara ndivyo ilivyo, usitegemee faida kubwa sana kwenye mzigo mmoja. Biashara inahitaji turnover ya wateja. Pia biashara ya nafaka unatakiwa kucheza na demand and supply. Wakati supply iliwa kubwa huko unakonunulia ndio muda wa kununua then demand ikiwa kubwa ndio wakati wa kuuza.
 
Circulation ndo itakupa pesa, uzoefu kazin na ukubwa wa biashara utaonekana kwa kuzingatia uzoefu wako kazini

Jamaa yangu alianza na mtaji usiofika hata 1M, sas anatengeneza profit ya 5M per single month
Ni kweli nakuelewa kwa upande wa circulation, ila kwa sisi ambao ni waajiriwa, kupotezwa dimbani ni rahisi
 
Unapozungumzia ujanja ndio unamaanisha kuchanganya mali nzuri na mbaya? Ndio uhuni unaofanyika, unanunua mchele super, wanachanganya na bei rahisi, au maharage mazuri wanachanganya na maharage mabovu.
 
Mtaji wa M30 kwa faida ya M2.5 nisingeacha.Labda kama siyo faida.
 
Unapozungumzia ujanja ndio unamaanisha kuchanganya mali nzuri na mbaya? Ndio uhuni unaofanyika, unanunua mchele super, wanachanganya na bei rahisi, au maharage mazuri wanachanganya na maharage

Unapozungumzia ujanja ndio unamaanisha kuchanganya mali nzuri na mbaya? Ndio uhuni unaofanyika, unanunua mchele super, wanachanganya na bei rahisi, au maharage mazuri wanachanganya na maharage mabovu.
Hapana sina maana hiyo maana ya ujanja hapa imebase katika timing and calculation lazima ujue muda mzuri wa kununua mchele na lazima uwe na hesabu kali katika kuwa approach wateja mfano mchele super nauweka viroba viwili mteja namwambia super hii 2500 na super hii nyengine ni 2800 kwa akili za mteja atanunua wa 2800 maana ataona bora zaid lkn ni aina moja akili ya binadamu lazima uipe option katika best product
 
Hujajua hesabu ya biashara ww vizuri hiyo 100 inalipa sana tafuta soko uwe unakimbiza kila week hiyo 300000 ukikimbiza kwa mwezi mara 3 yaani kila baada yasiku 10 utakuwa na 900000 kwa mtaji 6000000 ni sawa jali soko zaidi na mashamba zaidi
Biashara ya mitandaoni hiyo,kumbuka unaweza kununua mzigo Kwa 2500,kufika sokoni ukakuta bei imeshuka Kwa 2300! Biashara ya mazao ww isikie mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…