Biashara ya Nafaka mtaji mkubwa faida kiduchu

Biashara ya Nafaka mtaji mkubwa faida kiduchu

Unapozungumzia ujanja ndio unamaanisha kuchanganya mali nzuri na mbaya? Ndio uhuni unaofanyika, unanunua mchele super, wanachanganya na bei rahisi, au maharage mazuri wanachanganya na maharage mabovu.
Mkuu kuna kuchanganya pia sasa mteja wa jumla anakwambia umletee mchele wa 1,400 na wewe unanunua kwa 1,200 ongeza gharama 100 upate faida ya 100 na kukukipa hakulipi yote. Cha kufanya tafuta mchele wa 1,000 punguza chenga unampelekea walau upate faida la sivyo anakufilisi
 
Kaka mtaji more than 30 million faida Tzs 2.5 million per month.. kaka faida n ndogo compared to capital invested n hustling aiseee..
Kila siku nawaambia watoto kama ninyi kuwa sio kila mtu ni mfanyabiashara
 
Mkuu kuna kuchanganya pia sasa mteja wa jumla anakwambia umletee mchele wa 1,400 na wewe unanunua kwa 1,200 ongeza gharama 100 upate faida ya 100 na kukukipa hakulipi yote. Cha kufanya tafuta mchele wa 1,000 punguza chenga unampelekea walau upate faida la sivyo anakufilisi
Hakika kila biashara ina teknolojia yake😄😄😄😄😄
 
Hii biashara ni nzuri na inatoka lakini bila kua mjanja mjanja basi kutoboa ni ngumu sana, zaidi ya kupata hela ya kula tu kwasababu faida yake kwa kila kilo ni tsh 50-100...haiwezi kuzidi hapo.

Nilikua na million 6 nikasema nikaangalie swala la mahindi, unaweza kujaza gari la tani 10, gunia 100, baada ya kufikisha sokoni ukapata faida ya laki 3, imagine fuso zima unapata faida ya laki 2-3 ni ndogo ukilinganisha na hustling huko vijijini porini mashambani inaweza kuchukua hata week 2, na ukifika sokoni kama huna sehemu ya kuuzia umpe mfanyabiashara kwa mkopo akiuza ndio akupe hela.

Kwenye maharage ni hivyo hivyo, unanunua gunia kwa 2500/= shambani/mnadani unakuja kuuza kwa 2600/=....imagine unanunua kilo 2000, ambayo ni kama 5,000,000/= alafu unaenda kuuza kwa 2600/= ambayo ni sawa na 5,200,000/=....

Investment ya million 5 upate laki mbili, million 10 upate laki 4, sasa hii biashara si pasua kichwa? Ingekua kwa mwezi unaenda safari 3/4 ingekuwa poa sana, lakini unajikuta kwa mwezi mpaka mzigo uishe unaenda mara moja tu,..

Lakini ukiwa na mzunguko mzuri na ukawa na eneo lako la kuuzia basi hii biashara utaipenda.
Biashara sio ya kila mtu, hakuna biashara inayolipa kama mazao
 
Hakuna biashara inalipa Kama Nafaka ukiwa MTU unazingatia ubora quality inalipa Sana.

Nimefanya hii biashara kikubwa usifocus kuuza cheap product
Tatizo kuna watu hawaelewi kabisa hii biashara
Faida ni kubwa ila inataka storage za uhakika na uwe na kila aina ya mazao sio mchele tu
Unanunua kila kitu mchele, ufuta, mahindi, karanga
Mtaji wangu ulikuwa mkubwa na nilipiga hela sana
Anaesema faida ndogo basi mtaji mdogo pia
10m is nothing weka x10 uone
 
Kaka 2.5 million faida mtaji n zaid ya million 30 kwa mwezi.. faida hii n ndogo sana kaka.. advantage tu ni TRA hawakugusi.. ni ushuru tu unalipia..
Akipiga trip 10 huyo kisia atakuwa na mtaji wa kiasi gani tatizo wabongo tunapenda mafanikio ya chap chap bila jasho na pia tunataka biashara yenye profit margin kubwa kwa mara moja
Kwa faida hii tuchukulie umedumu kwenye biashara miaka 10 huyu atakuwa a mtaji koasi gani kama ni mtu mwenye malengo
Hawa akina mo ,bakhresa ,GSM na wengineo wanapata mpaka faida ya sh . 10 kwa kilo na wanaifurahia.cha msingi angalia mzunguko
 
Kaka mtaji more than 30 million faida Tzs 2.5 million per month.. kaka faida n ndogo compared to capital invested n hustling aiseee..
Hukuona mbali tu,kwenye biashara inatakiwa uwe na jicho la mbali baada ya mwaka 1,2,3,.n,k amini nakwambia kwa faida hiyo kwa mwaka uko mbali
 
Sasa 10% ya 30m ni 150k ...duh!
Tatizo lako hujaelewa afu unakaza fuvu
Mwenzako kasema faida ya 2.5M ni almost 10% ya mtaji wake wa 30M,so asingeacha ni nzuri maana kuna watu wanawekeza mtaji mkubwa ila faida kidogo kwa mwezi akamtolea mifano hiyo ya waliojenga nyumba za kupqngisha kwa 300M na 30M (huyu anapata laki na nusu kwa mwezi)
 
Back
Top Bottom