Changamoto ilikuwa nini mkuu? Muda unaotumia kukusanya mzigo au muda unaotumia mpaka mzigo uishe (mzunguko)? Au udogo wa faida?
Biashara ya kuuza mahindi ni pasua kichwa.
Hii kazi kwa sasa ishakua ngumu, saivi watu wengi mitaji yao imekuwa mikubwa ila kwenye jambo la biashara hawana mbinu ya kufanya biashara mpya, wamebaki kuiga tu.
Unakuta mtu ana pesa ndani ila biashara ya kufanya hajui, anakaa anaangalia mafanikio ya mtu kwanza kisha kazi gani anafanya ili aige.
Basi yeye mzima mzima anaingia kwenye hyo kazi ambayo ameiga kutoka kwa mtu fulani, bila kujua mwenzie amefanya lipi na lipi mpaka akasimama kibiashara.
Biashara ya mahindi kwa sasa sio biashara, KWANINI?
Hii kazi kwa sasa ni ngumu, una kwenda shamba kununua, kule unakuta kuna dalali wa mahindi shambani.
Huyo dalali ana kwambia (niache pesa nikukusanyie mzigo)
Ili ukusanye mzigo haraka inabidi uitawanye pesa yako kwa madalali wengi na sehemu nyingi tofauti tofauti.
Kila dalali unaweza kukusanya roba 10-15 kwa wiki, inategemea pesa yako na hali ya hewa kama inaruhusu.
Sasa kuna mawili, dalali wa shamba akimbie na pesa au akupe mzigo wako.
Sasa tatizo lingine ni unakuta mabosi mpo wengi mnao mwachia pesa dalali, labda ww ni wa4 kat ya hao mabosi mpaka kufikia zamu yako.
Hivo hali hyo itafanya ushindwe kwenda na muda, utakuta unakaa cku nyingi bila kutoa mzgo shamba na kipengele kingine ni usafiri.
Pesa nyingi sana inaishia kwenye usafiri wa kutoka shamba hadi kufika barbrn, baada ya hapo ndo upakie mzigo kwenye gari ya 1kwa1 mpaka mjini.
Kipnd cha nyuma tulikuwa tunapata faida ya elfu 7 kwa roba moja lenye uzito wa wastani kilo 128, ila kwa sasa bei ya shamba na mjini utakuta inapishana elfu 10, sasa ukipiga hesabu ya kibiashara inakuwa hailipi!
Kutoka nlipo hadi ufike huko mashambani unatumia saa 1-2 (spidi 50-70) kwa pkpk na inategemea na kasi yako.
Kutoka nyumbani nilipo mpaka mjini (km 110) na ukisema ununulie hapa hapa nyumbani unachelewa kueneza mzigo kwa muda unaotakiwa na bei inakuwa kubwa tofauti na shamba, maana bei za mahindi huwa znapanda na kushuka.
Muda mwingine baadhi ya madalali wa mjini pia huwa ni vipengele. Unampa mzigo afu yeye hakupi pesa taslimu, au anatengeneza mazingira akupige pesa kwa njia ya uchafu au vumbi la mahindi.
Kabla ya kupima roba lazima dalali alikague kwa kulipiga bambo kisha anaangalia mahindi kama mapya, zamani, meupe, njano, machafu(vumbi) au fangasi.
Sasa dalali anapga bambo roba la kwanza la pili la tatu kisha anakwambia mahindi yako machafu, yana vumbi hivyo nakata kilo moja kila roba na wengine anakukata hadi kilo 2, kwa7b unakua huna jinsi inabidi ukubaliane naye kupima ivo ivo.
Sasa ukipiga hesabu unakuta dalali ashakupga zaidi ya shilingi 300-600 mara idadi ya roba zako.
Kwa haraka haraka unaweza kuona hyo pesa anayokukata dalali ni ndogo ila ukija kuzidisha mara mzigo wako wote, anakuwa amekuvuta shat pakubwa sana yaan anaweza akachukua roba 1 kwenye roba 60.
Hizo ni baadhi ya changamoto ambazo unaweza kukutana nazo kazini.