Biashara ya ndege haiwezi kuleta faida kabla pay back period haijafika

Biashara ya ndege haiwezi kuleta faida kabla pay back period haijafika

Kwanza Nielezee kidogo "Pay back period".Kwa faida ya wengi hii ni njia ya kubajeti mtaji (Capital Budgetting Method),inayo eleza muda utakaotumika kurejesha kiasi cha mtaji uliowekezwa katika mradi (Katika miaka).

Mfano. Kama Pay back period ni 1 Maana yake kwa mwaka mmoja tayari,kiasi cha mtaji kilichowekezwa kitakuwa kimerudi.
 
Kwanza Nielezee kidogo "Pay back period".Kwa faida ya wengi hii ni njia ya kubajeti mtaji (Capital Budgetting Method),inayo eleza muda utakaotumika kurejesha kiasi cha mtaji uliowekezwa katika mradi (Katika miaka).

Mfano. Kama Pay back period ni 1 Maana yake kwa mwaka mmoja tayari,kiasi cha mtaji kilichowekezwa kitakuwa kimerudi.
Safi mkuu, mimi kidogo kishwahili nimeanza kukisahau.
 
Tofautisha vitu viwili..
1. Return of Investment
Yaani kurudisha mtaji uliouwekeza kwenye biashara na biashara ikaendelea kuwepo.
2. Return on Investment
Yaani hapa sasa faida inaanza kuingia baadaya mtaji kurudi.

Hili la ATCL kujiendesha kwa hasara maana yake ni kuwa kwa trend inayoenda nayo, yaani operating income kuwa juu kuliko revenues(mapato) maana yake hiyo biashara haiwezi kamwe kurudisha mtaji(return of Investment)...achilia mbali kuleta faida(return on Investment)...itaenda kufa tu.

Mfano...kwa mwaka shirika litumie bilioni 100 ktk uendeshaji wa shughuli zake...kama ku service ndege..kulipa wafanyakazi n.k...baada ya kufanya kazi kwa mwaka mzima likapata mapato ya bilioni 40....hapo kuna hasara ya bilioni 60...yaani hata gharama za matumizi hazijarudi zote. Negative growth.

Hiki ndicho kinacholikumba shirika letu...linatumia costs nyingi kujiendesha..lakini mapato yanakuwa madogo kuliko matumizi. Hivyo financial statements zikiandaliwa lazima kuwe na loss...hakuna faida.

Hii ni tofauti na endapo kama ATCL ingekuwa inajiendesha kwa faida for the past 5 years...mfano kama kwa mwaka shirika limetumia bilioni 100 kujiendesha na likapata mapato ya bilioni 140 kwa mwaka...hapa litakuwa na faida ya 40 billion..positive growth.

Kuhusu kurudisha mtaji..
Biashara ambayo ina positive growth...ndiyo inaweza kurudisha mtaji na baadaye kuanza kuleta faida. Na hili linaonekana ktk hesabu za shirika za kila robo au mwaka....kuwa kuna ukuaji chanya unaoelekea kurudisha mtaji wa hela ya ndege zote na other costs

Kukiwa na profit..basi ni rahisi kupiga hesabu kuwa baada ya muda fulani mtaji uliowekezwa utarudi. Lakini hata kujiendesha kwenyewe tu ni kwa hasara...hapo sahau kurudi kwa mtaji....hela zetu za kodi ndizo zitazidi kuumia.
 
Forget pay back period, we all know economics.

Regardless of whether the payback period has been attained or not. ATCL Ni mzigo kwa mlipa Kodi. That means, the government had to inject 60b to save ATCL from sinking.

Kama unafanya kazi huko tafuta kazi nyingine. The white elephant will sink any time t.
 
ni kweli mkuu, sasa hapo anawaogopesha watanzania ni vyema angetuorozoshea kwanza zile fedha zilizowekezwa kama tayari zimesharudi then atupatie na kipindi cha Kurudisha kilikua ni miaka mingapi alafu atwambie sasa hizo ndege zinaingiza fedha kiasi gani kwa kila mwaka kabla ya kukokotoa hasara au faida.

Kwasababu kwa mtaji ulizowekezwa kwa kila ndege sitegemei shirika kuanza kupata faida haraka kiasi hicho.
Na kumbuka ATCL inakodi ndege kutoka kwa serikali hivyo uwekezaji wa kununua ndege haumhusu bali kinachomhusu ni uendeshaji, sasa payback ya investment ya kununua ndege huenda pia haimhusu. Huenda hasara yake ni ya kuendesha biashara ya kukodi ndege pasipo kupata faida. Yani gharama za uendeshaji ni kubwa kuliko anachoingiza hivyo ndiyo maana ikaitwa hasara.
 
Sawa payback period haijafika, imekuwaje hasara yote hii 60B itokee kwa kipindi kifupi hiki?

Kuna speech ya magufuli alishawahi kusema tangu zimenunuliwa zimeingiza faida ya bilion 20 ( nauhakika hata hapa usikute zilikuwa ni propaganda tu).

Lakini kwa mujibubwa ripoti ya mwaka 2019/2020 imepata hasara bilion 60.

Na kaongezea kwamba hata katika miaka mingine ya nyuma bado ilikuwa inaendeshwa kwa hasara.

Sasa tukiwnza ku classfiy tutaona mlango wa kuingilia hela ni mdogo kuliko wa kutokea. Point hiyo inatosha kufanya hata zile zinazosemekana ni faida kutokuwa na mashiko.
 
Pay back period ndo nn?
Payback period refers to the time required to recoup the funds expended in an investment, or to reach the break-even point. For example, a $1000 investment made at the start of year 1 which returned $500 at the end of year 1 and year 2 respectively would have a two-year payback period

Payback period ni kipindi ambacho zile fedha yaani mtaji na gharama ulizozitumia wakati wakuanza mradi uliowekeza zinarudi. Kinaweza kuwa ni siku kazaa, wiki kazaa, miezi au miaka kazaa kutegemeana na biashara unayofanya na uwingi wa fedha ulizowekeza na kutegemeana na soko lililopo. Hizo fedha zinazorudi zinaitwa payback au return of investiment. Baada ya kipindi hicho sasa ndipo unaanza kuhesabu faida.

Sasa kwa miradi mikubwa unapokokotoa hasara au faida lazima uhusishe bei za hizo ndege, mafuta, malipo ya wafanyakazi n.k Hapo ndege ndio inapesa nyingi zaidi, hivyo ukikokota tu lazima upate hasara. Kwasababu fedha iliyotumika kununulia bado haijarudi.
 
Na kumbuka ATCL inakodi ndege kutoka kwa serikali hivyo uwekezaji wa kununua ndege haumhusu bali kinachomhusu ni uendeshaji, sasa payback ya investment ya kununua ndege huenda pia haimhusu. Huenda hasara yake ni ya kuendesha biashara ya kukodi ndege pasipo kupata faida. Yani gharama za uendeshaji ni kubwa kuliko anachoingiza hivyo ndiyo maana ikaitwa hasara.
Sasa kama ni hivyo wakuwajibishwa ni hizo ndege au ATCL?
 
Sasa kama ni hivyo wakuwajibishwa ni hizo ndege au ATCL?
Swali lako halijaeleweka, ila kwa kifupi ni biashara kichaa ambayo matumizi yanazidi mapato. Yani hii ina maanisha shirika haliwezi kujiendesha.
Hivi mbona hujiulizi maigizo yaliyokuwa yanafanyika ya kutuongopea wanatengeneza faida hadi kutoa gawio?
 
Soma uelewe

Swali lako ni sawa na dreva wa daladala aliyepewa na mwenye daladala aulizwe lini gharama za kununua daladala zitarudi wakati daladala si lake. Yeye kazi yake ni kupeleka hesabu.

Sasa itokee sababu ya kukosa abiria dereva hapeleki hesabu ila kila wiki anakuja chukua pesa kwa ajili ya kuweka mafuta, kumlipa konda na service.

huu ndo utakuwa uhusiano wa ATCL na Serikali sasa.

Hiyo ni accounting profit/Loss. MAPATO TOA MATUMIZI.(MTAJI HAUHUSIKI MAANA NDEGE NI ZA SERIKALI NA HUWEZI ZIKAGUA MAANA ZIPO CHINI YA OFISI YA RAISI)

Ndege si za ATCL ni za serikali. ATCL imekodishiwa.

Payback period labda serikali iweke wazi thamani ya ndege kisha hesabu za commission wanayopokea kwa mwaka kutoka ATCL ziangaliwe ndo utajua pbp. Lakini hiyo haiwezekani sababu shirika linaingia hasara hivyo zile hasara zinaendelea kuongeza gharama za ndege.

Mpaka wakati watakapotengeneza faida kisha wakaacha kuchukua pesa serikalini halafu wakajiemdesha na kubakisha gawio la serikali hapo ndipo wataweza kufuta gharama za uwekezaji.
 
Ni ule muda ambao biashara yako inakurudishia fedha na gharama zote ulizowekeza wakati unaanzisha hiyo biashara. Hapo kuna gharama nyingi tu. Gharama za kununua ndege, gharama za kununulia mafuta wakati unakwenda kuzichukua, gharama za kuwalipa wafanyakazi wakati unaanza, n.k
Huo muda usiuweke katika pattern usieleweke ni muda gani. Muda ambao ni target ili urudishe pesa zako ni muda kiasi gani?

Kumbuka unavyozidi kusotea kuutafuta huo muda ili urudishe hizo pesa upande wa pili unazidi kupata hasara

Mpaka hapo unajiweka katika hatari ya kutafuta pesa ya gharama ya chombo na kutafuta pesa kwa ajili ya ku fix hasara, pamoja na profit kitu ambacho ni ngumu ku make ukiangalia na rotation yako ilivyozidiwa na majabari ya hasara kubwa kubwa kuzidi faida

Halafu hizo ndege mara nyingi zinakuwa na free derivery kwa hiyo point ya kusema gharama ya usafirishaji hapo itoe wala haina mashiko kabisa
 
Report ya Cag ina utata mwingi sana mfano kama hasara ni bil 60 mbona hajasema nani awajibishwe na hasara lkn bil 3 mtu kachukuliwa hatua iwe wazi kama msomi hapa kachemka sana
Mnamtafuta mchawi, biashara ya ndege ngumu sana sasa utamwajbisha mtu kwa cost za uendeshaji kuwa kubwa kuliko mapato. Huyo wa bilioni tatu zimepigwa kwa uzembe au kqa ushirika wake, anastahili adhabu kabisa.

Uzuri CAG siyo mpya ni yule yule msije sema katumwa na beberu
 
Hapana any investment lazima iwe na plan yake na ijue ni lini pesa iliyowekezwa itakuwa imerudi kabla ya kupata faida. Hali hiyo tunaita PAY BACK PERIOD. Lkn ikiwa mwaka husika kampuni gharama ilizotumia na kile kilichopatikana kikiwa sawa hapo ndio tunasema BEP
Hapo sawa jombaa kama maelezo yako ni ya kweli! Je ikafika mwaka ambapo gharama ikawa kubwa kuliko gharama walizojipangia! Hapo tunapaitaje kitaalamu??? Au ikafika mwaka gharama ikawa ndogo kuliko kiasi walichojipangia! Na hapo kitaalamu tunaitaje?? Please naomba ufafanuzi.
 
Biashara ya ndege haiwezi kuleta faida kabla pay back period haijafika
ni vyema unapotwambia imeingiza hasara uwe unatupa na pay back period ilikua ni miaka mingapi. Na je tayari ilishafikiwa. Ila kama hiyo hasara unaikokotoa bila kutwambia pay back period ilikua ni miaka mingapi hapo watanzania utawachanganya.

Mimi nadhani tungepewa hesabu nzima, tusiandikiwe tu hasara.

Tupewe pesa iliyotumika kufanya investiment ni kiasi gani kwa ndege zote.

Alafu tuambiwe kila ndege zinaingiza kiasi gani kwa mwaka.

Hiyo ndio hesabu tunayoitaka,
Mimi nacho kijua na kukielewa hiyo ni long term business ambayo inatumia higher investiment. Hivyo haiwezi kuleta faida kabla haijafikia payback period.

Twambie kwanza pay back period ilikua ni ya miaka mingapi ndipo uje na hiyo hesabu ya hasara.

Ukitwambia tu hasara hatuwezi kuelewa vizuri.

Maana bado siijui payaback period

Ipo miradi mingi mikubwa ambayo ikiianza usitegemee kupata faida ndani miaka minne, it's impossible. Tuna mradi wa LNG, huo mradi payback period yake ni ndefu sana. Tusitegemee kuja kuanza kupata faida ndani ya muda mfupi. Katika Biashara kubwa lazima uwe mvumilivu.

Mimi kiukweli ningependa kusikia tu return of investiment imefikia kiasi gani basi. Hapo ningechakachua kichwa na kujua wapi tunaelekea.
Kukusaidia tu mleta mada, fahamu haya.

-Mpaka sasa ATCL haijapewa mtaji wa pesa wa kujiendesha, ndege inazotumia ambazo zimenunuliwa na Magufuli ni mali ya wakala mkuu wa ndege za serikali, ATCL wamekodishwa kwa mkataba wa siri (bure!).

-Mpaka leo hii ATCL inaendeshwa kwa ruzuku ya pesa za serikali.

-Mtaji wa ATCL uko hasi, kutokana na mzigo wa madeni ilionao. Ukiwapa leo mtaji, mtaji wote unakwenda kuzama kufidia madeni.

-Faida/Hasara inayosemwa na CAG kwa ATCL, ni kile ambacho ATCL wanakipata baada kuchukua Mapato yao (Total income) halafu wakatoa gharama za uendeshaji (Operation cost) kwa mwaka.
 
Back
Top Bottom