Una uwezo hafifu wa maswala ya kiuchumi na ndio maana hata ukiambiwa utoe ushauri ATCL ifanyeje ili ipate faida utashauri ndege ziuzwe. Mtu mwenye akili ndogo hawezi endeleza asset bali huwaza ziuzwe. Na ndio maana afrika hawana viwanda, afrika hawana makampuni ni kwasababu ya kuwa na waafrika wenye uwezo mdogo kama wewe hapo. Mliuza viwanda vyetu vyote vilivyo jengwa na Nyerere, mliua shirika la ndege lilianzishwa na Nyerere, mliua shirika la reli likawa halifanyi kazi vizuri, mliua kila kitu, ili kila biashara mzishirikirie nyinyi tena hata kodi mkawa hamlipi, mtaka mfanye free business matokeo yake serikali ikakosa hata fedha za Kujenga madaraja na Kujenga na barabara nzuri, huduma za afya zilikua mbaya, kwasababu tu mlijibinafsishia kila kitu.