wiseboy kosa ulilofanya hukufanya utafiti vizuri. Siku nyingine huulize kwanza maana kama haujafanya utafiti ukienda sehemu yoyote utaumizwa.
Kila nchi kuna maduka ya gharama na bei ya chini ni vizuri kujua maeneo kabla ujaenda
.....JE NILIENDELEA AMA?...
Kwa kweli sijarud tena kuchukua huko mzigo nikaamua kubadili upepo, nikaenda maduka ya hapa dsm kwa wahindi wapumbavu watupu, wezi wale, matusi yao mizigo mibaya kama roho zao, just hasara juu ya hasara...
Kwa sasa nachukua nguo ilala na zinanilipa, kuna jamaa pale wana vijana wao wanapoint nguo kali kali wenyewe wanaita sumu, then inapofika mchana wanazitundika kwa pamoja, wamenizoe nikifika mfano mtu ana nguo kama elf 5000 katundika anakuruhusu uchague zile utakazo na wanafanyaje
1.tops nachukuaga kwa 3000 unauza elf 8000
2. Gauni ndef nachukuwa kwa 8000 nauza mwisho 15,000
3.gauni fupi 5000 nauza elf 10 mwisho
4.skin jeans nachukulia elf 5, nauza 10,000 mwisho,
5.sketi fupi 5000 na kuuza 10elf,
hvyo naona bora hii ya bongo kuliko uganda, sikutaka kuwa mchoyo kwan jf imenisaidia mengi ktk maisha yangu, pia kama kuna m2 ana ushauri kuhusu the way ninavyofanya hii biashara namkaribisha, kama kuna sehemu nyngne pana soko zuri la mtumba namkaribisha pia, nimeandika mara nyngi nyingi coz natumia 4n kuandika, karibuni wadau tusaidiane hasa vijana maisha yasonge mbele.
thamns sana ngoja nikupm
Mkuu Dumelang plz hebu niPM namba zako najaribu kukutumia ujumbe huko PM unagoma cjui kwanini Nina bwana mdogo wangu anataka kufata Viatu huko sasa anataka Mwangaza kwenye maeneo flan nikipata mawasiliano yako au yeyote mwenye uzoefu wahuko Itakuwa msaada tosha namba zangu ni 0764 504 540 Natanguliza shukrani
Dah, long tym leo ndio naona hii msg yako, unajua app ya jamii forum ni weak kidogo kuna uptodates kama za quote huwa hai alert, sorry bro ila nazani ushafanikiwa
Habari ya cku kiongozi kwakweli bado cjafanikiwa dogo amefungua kibanda cha kuunza nguo wenyewe wanaita kuPOINT lkn wazo lakwenda huko bado liko palepale....amepata oda ya simple shoes za kiume kutoka huko cz wateja wake wanasema simple ya kichina yakule iko na quality nzuri na bei ingemlipa sasa kila nikijaribu kuchek na watu wanaokwenda huko hawanipi majibu mazuri...so plz mkuu.. bado nahitaji mwongozo wako ikiwa unajua ni maduka ya maeneo gani akienda huko ataweza kupata bidhaa hiyo.....plz nichek humo...0776 800 648 na 0788 860048 natanguliza shukrani
Nimepata namba yako, nitakuunganisha na wanaokwenda kila mwezi, sisi wafanyakazi kazi huwa mpka likizo
Pamoja ...
Jamani, maisha nilikuwa nayaona magumu kweli! Nimesoma hii thread tu nikaona yamekuwa rahisi! Hakyanani inabidi nijipange ili mwaka 2015 kieleweke!
Nilivyokumisi, mh :busu !kumbe kiembe samaki ulikuwa hujafika huku ushayapatia maisha ndugu ila kaza buti na anza mchakato mapema usisubiri muda ukupite bure mwanzo wa asubuhi uanza mapema sio jioni upo hapo best
wewe inaelekea unafahamu mambo mengi sana ya biashara na yaelekea unafahamu njia mbalimbali za kibishara aiseee hongera sana nitakutafuta ngoja nijipange kwanza
Kwa nini kila mtu anafikiria kuchukua vitu nje na kuleta nchini? Kwa nini tusifikirie vitu vya kuchukua Tanzania kupeleka nje? Dola itafika 5000
Pasipo kufichana vitu vya Tz havina ubora kabisa, ukichukua mkoba hapa TZ ukapeleka nje tayari utakuwa umeua soko lako milele, maana mtumiaji akifanikiwa kutumia kwa miezi 3 basi hapo muujiza umehusika.
aisee vitu vyetu ni sheeedah!!!!!!! chukua kitenge cha tz kikifuliwa mara moja kinachuja rangi na kikikauka kimechakaaaa. chupi za kike ndio usiseme haieleweki imetengenezwa kwa material gani, ni kukomaa na kulegea tu. acha tutoe nje tulete ndani ili kulinda soko na wateja hatuna jinsi.
Nafikiri hata UG bidhaa nyingi zenye ubora hawa-produce wenyewe bali nao wana import kutoka nje?