Tumpara Dudu
JF-Expert Member
- Nov 15, 2016
- 625
- 506
Naomba kujulishwa hilo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba ni pm namba zako kakaUganda nguo ni bei nafuu sana kwa sababu nchi za America,Asia na Europe zimefanya uganda kama sehemu ya kupeleke nguo ,begi,viatu etc kutokana na kuwa hawana urasimu wa biashara na kodi ni kidogo sana.Tanzania kuna urasimu na kukandamiza sana wafanyabashara kwa njia za kodi.kule wanasapoti wafanyabiashara kwa vitendo.
Pia soko ni kubwa kuna watu toka tanzania,Kenya ,rwanda,Congo,Burundi,Eritrea,Ethiopia,China,India etc na hakuna sheria kali za uhamiaji kama tanzania kwa ufupi kule hakuna kufatiliana utaifa ni free kabisa.Twende kwenye maswali yako sasa,
Sehemu ambazo unaweza nunua mzigo ni city centre lakin mitaa ya Ben Kiwanuka,Tax park,Copper complex,Arua park na Owino market na sehemu jiran na Owino market.
Kwa vile unataka mitumba ingia Owino Market uko vitu ni bei rahis sana ila inahitaji ubageini na ni lazima ubageini,viatu ( TimberLand )ambavyo nanunua Tanzania 90,000 tzsh kule nanunua kwa 15,000-18,000 tzsh ila wanakuanzia mbali unaomba upunguziwe.
Uko Owino wafanyabiashara wanajua kiswahili vizuri ila ukiambiwa bei,wewe sema ambayo ni kidogo sana kutegemea na mzigo pia wakat unanunua ndio wakat mzuri wa kujua pia utauza kiasi gani.
Tshirt ya 15,000 tzsh pale unapata kwa 1,500 tzsh tena hiyo bei rejareja kwa wewe ukinunua kwa uwingi bei ni rahis sana.Uganda imefanywa kama dampo la bidhaa hizo na watu wa ulaya,asia na america.
Sehemu ya kulala maeneo ya copper complex kuna guest nzuri moja inaitwa Galaxy Guest house ni nzuri sana,bei zake ni ndogo sana kutegemea na unachukua room gani bei uanzia 15,000 ugsh hadi 30,000 Ugsh ndio bei ya juu kabisa.
room zipo ghorofan chini ni mgahawa,pia ukikuta imejaa jiran na hapo kuna nyingine Boston guest house ni nzuri pia na ata wafanyakaz wa hapo uongea kiswahili .bei zake ni ndogo.na hizo sehemu ni jiran na shoprite pia kutoka hapo hadi owino ni dakika 2 tu kutembea na hizo sehemu ndio kwenye maduka mbalimbali.
Kuhusu kodi,kuna mbinu inafanyika nitaku pm si vizuri nikieleza hapa.Kuna njia mbili za kwenda uko kuna njia ya kupitia Nairobi hadi Kampala na kuna jia ya kati hadi Bukoba kisha unapanda bus za Friends huondoka saa moja asubuh kutoka bukoba kwenda kampala,na saa sita na nusu uko kampala,ukifika hapo chukua bodaboda hadi Galaxy Guest house au Boston zipo maeneo ya copper complex jiran na shoprite ambapo kwa bodaboda haizid 2000 ugsh.
Pia ata maeneo ya Arua park kuna guest za kulala pia. ( hayo maeneo ni kama unavyoona kariakoo majina ninayotaja ni kama mitaa tu mfano msimbazi etc hizo sehemu ziko jiran jirani )
Rate za ubadilisha pesa ni 1.5 hadi 1.6
yani 1,000 Tzsh ni 1550-1600 Ugsh.
wakat ambapo shule zinafunguliwa rate inashuka sababu wanafunz wengi wa kitanzania wanakuja na pesa na wanachange inaweza pungua hadi 1.5 au 1.55.
kuna bus kama Falcon utoka dar kupitia njia ya kati hadi bukoba kisha kampala.
njia ya nai mfano kuna spider utokea dar-nairob-kampala.
ni wewe sasa kuamua,nawajua watu wengi wanawake/wanaume wamefanikiwa sana kimaisha kupitia biashara hii.cha muhimu ukinunua kitu uombe sana kupunguziwa pia usiingiwe tamaa za kununua vitu ambavyo hukupanga kuna vitu vizuri sana kule na cha muhimu kuwa makini ili usiibiwe pesa,uporaji kule hakuna labda mtu achane pochi yake bila wewe kujua.
mkiwa na swali ulizeni
sawaNenda mwanjelwa
Ulifanikiwa kwenda?Habari wadau! Mimi ni Mjasiriamali! Nataka niwe nafata mzigo wa nguo za akina Dada Kampala, na kuja kuziiuza jijini Mwanza, je itanilipa ? Naombeni ushauri kabla sijaingia bahari jamani!
Mawazo mapya yanakaribishwa ili kuweza kunijenga! Karibuni sana!
Chukua laki nane zidisha mara 1.5 hela utakayo pata hapo ndo hela ya uganda.. Hesabu haraka hapo una kama milioni na kitu za kiganda sasa cjajua ndani ya hela hiyo n pamoja na gharama za usafiri na malazi au n mzigo tu... Kama n mzigo nazani inatosha.. Ukifika ulale hotel za gharama nafuu maeneo ya owino au nakawa hapo ndo kwenye masoko makuu ya bidhaa kwa mji wa kampala.. Na unaweza kulala submarine au triple 8.. Au guest za bei ya kawaida zilizopo nyuma ya msikiti wa ghadafi au njia ya kushukia uwanja wa nakivubo kama unatokea kampala ss au citizen collegeHivi jamani laki nane haitoshi kwenda Uganda kufuata mzigo ?
Mzigo wa aina gani?Hivi jamani laki nane haitoshi kwenda Uganda kufuata mzigo ?
Kurunzi ndugu, iyo mikoba inakuwa ni model fashion tofaut na inayouzwa kRiakooHiyo hela tosha sana tena siyo kuagiza uganda china kabisa hasa mikoba kwani utapata mikoba bomba.
Mfano ukiagiza mikoba 200 itakugharimu 3500000 mpaka ikufikie hapo ulipo kwa dar ambayo kila mkoba itakuwa imesimamia 17500 ambayo unaweza kuuza hito mikoba kwa 28,000-35,000 kwa bei ya jumla ili uagize tena usikae na mzigo ukiwa uko tayari ni tufabye biashara
Ahsante sana kwamaelezo mazuri mkuu. Umetufungua macho wengi. Na km in Nguo za special Kwa kariakoo ni upande gani?
Sent using Jamii Forums mobile app
AsanteBroo Peter Majaliwa kama sikosei kuna uzi humu unaongea sana kuhusu Uganda jaribu kutafuta kaka utakusaidia sana. Ila watakuja hapa wajuzi wa hizo root kuleta ushuhuda
Mkuu kwann unauliza hivyo?wadau hivi huyu Money stunna yupo hai kweli?
Naona yupo kimya sana. Namuhitaj mnoo kama una cont zake nakuomba sana unitumieMkuu kwann unauliza hivyo?
.....kuhusu kodi za nguo kusema ukweli ni ujanja wako, nilisumbuliwa tu pale mpakan mwa uganda na kenya wakat narud, nikawapa elf 30, wakaruhusu kupita, huku kwngne hata huulizwi unapita tu, mm safari nilianzia arusha naul elf 65 nenda rud laki 30, mzigo nililipia 70....
Hvyo ushauri wangu kule chukua nguo za duka sio mtumba, pili fanya research ya biashara ya hzo nguo pale unapotaka kuweka frem zinauzwaje b4 hujaenda,
na unaweza wasiliana na huyu jamaa maarufu wa kuuza mitumba ya grade A pale uganda japo mh anawateja weng na ndo ivo bei zake +2569211759, all the best mpendwa!
....kama utahis kuna kitu utataka kujua kuhusu physical chalenges nilizopitia, just ask, tho naona money stunna nae anakuwa msaada.