Niseme shukrani kwa
Money Stunna nilikwenda kampala July 15. Nililala kwa rafiki yangu mtz anafanya kazi kule kwenye kampuni moja ya mtz pia. Vitu kweli ni bei ya chini kulinganisha na TZ lakini changamoto niliyoiona ni kujua wapi upate hivyo vitu bei poa manake wanaanza bei ya juu kama wabongo. Mitumba (nguo,viatu,n.k) ni rahisi sana na kwa safari yangu hii nimedhamiria nijipange kwa ajili ya mitumba. Nguo za duka nimekuta nyingi ni za kichina na sio latest kama za TZ kwa vile sikubahatika kuyajua maduka yanayouza nguo au vitu vipya kwa bei ya chini kama alivyosema stunna.
MUHIMU: Kuna shopping center jirani na Owino imefunguliwa ina frame kibao kwa mtu anayehitaji kwenda kufanyia biashara kule zinakodishwa kwa bei latest JULY 17, 2014 nimeambiwa na wenyewe wenye jengo ni 1.2M UShs (around 800,000TShs) kwa miezi mitatu na kwa sasa kuna promo unaongezewa miezi 2 kufanya miezi mitano kwa pesa hiyo hiyo. Nimefanya uzembe kutonakili jina na nimeshalisahau.
Money Stunna na wengine mlioenda kama mimi mliofanikiwa kuyajua hayo maduka ya vitu vipya naomba mtujulishe. Nilihitaji sana kununua Timberland mpya kwa be ya chini lakini sikuyapata hayo maduka niliyoyaona bei ilikuwa 150,000Ushs.
Ahsante
Money Stunna na wote.
cc
Dumelang
MKuu
Mathematician
Hongera sana kwakuthubutu. Unajua jaman sisi tulioenda si wachoyo ila mtu anataka aulize habari za TRA mzigo unapitaje
Then mi nitiririke hapa, sasa mimi niseme tu kama upo serious we nenda UTaPITA, uki-fail Utalipia maana hata wao wanajua ISSUE zilivo lkn pia ikifika UGANDA , huwez kosa Mbongo pale hata atakaekupa mazingira halisi.
Niachane na upande huo nije kwa Mathematician tena, Bwana lile jengo jipya nililiona ila sikuulizia ila wewe naomba ulienda mbele zaidi, hongera.
Kuhusu Maeneo ya kununua vitu nazani Changamoto kubwa nikuwa tofauti na Bongo, wale jamaa vitu vinapatikana karibu sehemu moja.
Kwa mfano: Ukianzia Copper complex mpka Maeneo yanaitwa Nachivubo utaona nguo tu, humu wamechanganyika wafanyabiashara wanauza mzigo kwelikweli, kila duka ukiingia wakijua tu huongei luganda basi wanajua unataka nguo nyingi ni mgeni na bila shaka atakuambia labda hiz blouse au shirt rejareja ni 20000/=ush na jumla nitakupa 15000/=Ush
Utabageini mwisho atatua kwenye 14000/= au 13000/=ush
Uzoefu niliokuja kuupata ni kuwa hawa wote hawauzi jumla wanalangua tu yani hata ubageini ukahs nimeshushiwa, iyo bei ndo rejareja kaishapata na faida, Bei yenyewe ya jumla ipo chini ya hapo. Kwaiyo usiopokuwa makini bila shaka japo itaonekana ni cheap ila bado si bei ya jumla.
Ufanyeje sasa? Wapo wazoefu, utakapolala siku ya kwanza gesti. Gest za pale huwez mkosa mbongo mzoefu, mtumie.
Pili ukipata mganda anaejua mpe kidogo mwende nae Madukani, niliona mdada mmoja wa kikongo akifanya ivo alikuwa na kiuzoefu kidogo ila anatumia vijana wa pale gesti kwenda kununua vitu ( wapo poa sana wahudumu wa gesti na wanaushirikiano).
Lakn ukishindwa za njia hizijuu hapo, niligundua kuwa mara nyingi maduka ya jumla hana muda wakuanza na retail price, ana hit wholesale price moja kwa moja. Ukitaka ku bagain atakwambia thats wholesale price sir, na utaona tu ipo chini sana. Na pia atakuwa anakutajia bei ya kuanzia dozen. Labda jeans ukiuliza tu anakujibu kwa dozen. Na utaona pia ndan kapandanisha mizigo na sampo ni kiasi tu au hajaanika sampo kabisa. Waganda wanatumia sana midoli kuonesha sampo
Uo ndio uzoefu wangu na hii manunuzi ndo changamoto kweli,
mathematician nazani iki ndicho kilichokukumba pia, kuulizia bei unapewa ya rejareja, ukimwambia nataka wholesale price anashusha tu design lakn bado yeye pia anabaki na kitu yan hajauza jumla.
Labda nimekumbuka hili, tafta maduka ya wachina ndio mengi yanauza jumla viatu vya kike na nguo pia n.k. Inaweza kuwa njia rahs kwa mgeni kuanzia kupata duka la jumla.
Otherwise nili enjoy kuwa Uganda, si kwa starehe ila kwa ushapu wangu kwenda na kurudi tu nilipata mtandao mpana wa wajasiliamali wengine walionielekeza mengi, na namna yakutumia fursa pande zote na kupata masoko yanayolipa. Nilisave namba za kila aliekukubali kuwa rafiki na tunawasiliana, nakuwa limited tu, mimi nimeajiriwa, muda haunitoshi
😀
Haikutosha kuna mdada yule wakikongo nilisema hapo juu pia nilifanikiwa kumweka karibu nakuanza dodosa habari za kongo na fursa, kwasababu ya kanumba anawapenda wabongo.
😱 anatamani kuja bongo na yupo mbioni kuja kuona na yeye fursa. maana niseme tu pple ar trading jaman, si wabongo tu kwenda Uganda, wapo waganda wanakuja hapa, wazambia wanashuka moro pale kuunga safari ya kwenda kwao.
Nna mengi haitoshi kuandika, ila ukiwa na nafasi namtaji, jiunge na uanze sasa.
Nitafute private
Mathematician tupeane mawasiliano