Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari wana jamvi,naomba ushauri nataka kwenda uganda kuleta nguo za mitumba,pochi na viatu pamoja na vipodozi napenda kujua cha kufanya maana ndo nataka kuanza ikiwemo accomodation nikiwa uganda,je huku Tanzania nitaziuzaje,mtaji kwa mzigo wa kwanza uwe shingapi vip usafiri,Ushuru na TRA? Msaada plz.
ngojea ntafute karamu nakaratasi niupeluz uzi vizur
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Wakuu me nataka kufanya biashara ya nguo but mtaji Wang ni 2m msaada tafadhali
Inatosha kabisa. Ukianza anza na zile zinazo uzika sana kwenye soko
Dada yangu hebu nisaidie. Je,mtaji wa sh milioni 2 za TZ naweza kuanza?Umetoa maelezo mazur sana kwa maana hiyo ukiwa na mtaji wa m5 unaweza pata mzigo mkubwa na mzuri me napenda sana biashara aisee asante sana kwa maelekezo yako..
ukiwa na swali lolote kuwa huru kuuliza
mkuu stunna nakukubali na tusaidie kidogo kuhusu mambo kadhaa.
1: Je utaratibu upi unatumika wakati wa ununuzi? namaanisha wauzaji kule uganda wauza kwa robota au mtu unaweza chagua kidogokidogo haswa ukizingatia mitaji yetu midogo?
2: Je ukitokea moshi arusha nairob then uganda kunaweza usafiri huu umekaaje,? Namaanisha itachukua siku ngapi kufika uganda na njia hii inaweza kuwa na changamoto gani?
3: Je kama nafuata taratibu,itanilazimu kuwa na nini au kufanya nini mpaka mmzigo wangu ufike moshi?
4; Kwa ujumla kuna changamoto gani zingine za hii biashara maana wengine tunahamu na ndoto za kuifanya ila hatujawahi hata kuuza vocha,so tusaidie kujua lolote lingine kwenye hii biashara hasa changamoto za namna ya kununua na kusafirisha mizigo.
Hasante sana mkuu
Mtaji ninao,knowledge nimepata, vipi kuhusu soko nitalipataje na mie sina fremu?? ...Nipe idea ndio nataka nianze hii biashara sina uelewa wa soko.
du hii biashara sijui kama utaifanya,hata hujui uanze na mtaji kiasi gani!hata hujui utaishi wapi ukiwa uganda!kwani wewe ndo wale wakisafiri hadi afikie kwa nduguye!!
Kaka Money Stunna big up. Usafiri kutoka Dar hadi Kampala kwa sasa ni bei gani kama umesafiri karibuni.Inatosha kabisa. Ukianza anza na zile zinazo uzika sana kwenye soko
Uganda nguo ni bei nafuu sana kwa sababu nchi za America,Asia na Europe zimefanya uganda kama sehemu ya kupeleke nguo ,begi,viatu etc kutokana na kuwa hawana urasimu wa biashara na kodi ni kidogo sana.Tanzania kuna urasimu na kukandamiza sana wafanyabashara kwa njia za kodi.kule wanasapoti wafanyabiashara kwa vitendo.
Pia soko ni kubwa kuna watu toka tanzania,Kenya ,rwanda,Congo,Burundi,Eritrea,Ethiopia,China,India etc na hakuna sheria kali za uhamiaji kama tanzania kwa ufupi kule hakuna kufatiliana utaifa ni free kabisa.Twende kwenye maswali yako sasa,
Sehemu ambazo unaweza nunua mzigo ni city centre lakin mitaa ya Ben Kiwanuka,Tax park,Copper complex,Arua park na Owino market na sehemu jiran na Owino market.
Kwa vile unataka mitumba ingia Owino Market uko vitu ni bei rahis sana ila inahitaji ubageini na ni lazima ubageini,viatu ( TimberLand )ambavyo nanunua Tanzania 90,000 tzsh kule nanunua kwa 15,000-18,000 tzsh ila wanakuanzia mbali unaomba upunguziwe.
Uko Owino wafanyabiashara wanajua kiswahili vizuri ila ukiambiwa bei,wewe sema ambayo ni kidogo sana kutegemea na mzigo pia wakat unanunua ndio wakat mzuri wa kujua pia utauza kiasi gani.
Tshirt ya 15,000 tzsh pale unapata kwa 1,500 tzsh tena hiyo bei rejareja kwa wewe ukinunua kwa uwingi bei ni rahis sana.Uganda imefanywa kama dampo la bidhaa hizo na watu wa ulaya,asia na america.
Sehemu ya kulala maeneo ya copper complex kuna guest nzuri moja inaitwa Galaxy Guest house ni nzuri sana,bei zake ni ndogo sana kutegemea na unachukua room gani bei uanzia 15,000 ugsh hadi 30,000 Ugsh ndio bei ya juu kabisa.
room zipo ghorofan chini ni mgahawa,pia ukikuta imejaa jiran na hapo kuna nyingine Boston guest house ni nzuri pia na ata wafanyakaz wa hapo uongea kiswahili .bei zake ni ndogo.na hizo sehemu ni jiran na shoprite pia kutoka hapo hadi owino ni dakika 2 tu kutembea na hizo sehemu ndio kwenye maduka mbalimbali.
Kuhusu kodi,kuna mbinu inafanyika nitaku pm si vizuri nikieleza hapa.Kuna njia mbili za kwenda uko kuna njia ya kupitia Nairobi hadi Kampala na kuna jia ya kati hadi Bukoba kisha unapanda bus za Friends huondoka saa moja asubuh kutoka bukoba kwenda kampala,na saa sita na nusu uko kampala,ukifika hapo chukua bodaboda hadi Galaxy Guest house au Boston zipo maeneo ya copper complex jiran na shoprite ambapo kwa bodaboda haizid 2000 ugsh.
Pia ata maeneo ya Arua park kuna guest za kulala pia. ( hayo maeneo ni kama unavyoona kariakoo majina ninayotaja ni kama mitaa tu mfano msimbazi etc hizo sehemu ziko jiran jirani )
Rate za ubadilisha pesa ni 1.5 hadi 1.6
yani 1,000 Tzsh ni 1550-1600 Ugsh.
wakat ambapo shule zinafunguliwa rate inashuka sababu wanafunz wengi wa kitanzania wanakuja na pesa na wanachange inaweza pungua hadi 1.5 au 1.55.
kuna bus kama Falcon utoka dar kupitia njia ya kati hadi bukoba kisha kampala.
njia ya nai mfano kuna spider utokea dar-nairob-kampala.
ni wewe sasa kuamua,nawajua watu wengi wanawake/wanaume wamefanikiwa sana kimaisha kupitia biashara hii.cha muhimu ukinunua kitu uombe sana kupunguziwa pia usiingiwe tamaa za kununua vitu ambavyo hukupanga kuna vitu vizuri sana kule na cha muhimu kuwa makini ili usiibiwe pesa,uporaji kule hakuna labda mtu achane pochi yake bila wewe kujua.
mkiwa na swali ulizeni