Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

Kwa belo la nguo nzuri za kinadada ni 280000-35000 kwa Mnazi mmoja Dar es Salaam.
Nakushauri uongeze mtaji au utafute patner ili mchukue mzigo mzuri.
Kwa viatu Mshanajr kuna viatu alisema anavyo sijui kama bado vipo?

love thé love or hâte thé love.....
 
Kwa belo la nguo nzuri za kinadada ni 280000-35000 kwa Mnazi mmoja Dar es Salaam.
Nakushauri uongeze mtaji au utafute patner ili mchukue mzigo mzuri.
Kwa viatu Mshanajr kuna viatu alisema anavyo sijui kama bado vipo?

love thé love or hâte thé love.....


Asante mkuu kwa ushauri,ngoja niufanie kaz
 
Habari wadau.
Tafadhari ninaomba ushauri.
Nahitaji kufanya biashara ya viatu. Nko mwanza, tafadhari kama kuna mzoefu wa biashara hili anisaidie mawazo kwa hili, hata mahali vinakopatikana kwa bei nafuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nairobi kama vya mtumba kama special nenda Kariakoo au Uganda.
Uganda tuseme simpo moja utanunua elfu 75 ya uganda bei ya jumla sawa na 5000 ya TZ. Ambapo vinauzwa sio chini ya
12,000 hadi 15,000 hapa nchini. Ukichukua mzigo mkubwa utapata faida

Unaweza ukatumia Saibaba au Mordern coach kusafilisha mzigo wako kwa bei poua
Nauli 130,000/= kwenda na kurudi. Weka hapo kula kulala. Kuna sehemu panaitwa MUKWANO MALL ndo kariakoo ya Uganda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nairobi kama vya mtumba kama special nenda Kariakoo au Uganda.
Uganda tuseme simpo moja utanunua elfu 75 ya uganda bei ya jumla sawa na 5000 ya TZ. Ambapo vinauzwa sio chini ya
12,000 hadi 15,000 hapa nchini. Ukichukua mzigo mkubwa utapata faida

Unaweza ukatumia Saibaba au Mordern coach kusafilisha mzigo wako kwa bei poua
Nauli 130,000/= kwenda na kurudi. Weka hapo kula kulala. Kuna sehemu panaitwa MUKWANO MALL ndo kariakoo ya Uganda

Sent using Jamii Forums mobile app
Nice comment...!

The Great Gatsby
 
Habari wakuu nahitaji kufanya biashara ya kuuza nguo
Ninaa 5milion kam mtaji ushauri wa mawazo na wapi kwa kupata nguo kwa bei nafuj
Shukrani kwenu
 
Hahahaha ulibug usingeshuka mukono ni kama uje Dar kufata mzigo harafu ushukie chalinze.!!
Wiseboy umemsoma Stunna [emoji651]?
......ngoja nirud kwenye biashara sasa...kusema ukweli uganda nguo za duka, viatu vya duka, mikoba ya special vinauzwa angalau bei kdogo, ila mtumba mh cjaona faida kwa kweli kwa 7bu zifuatazo
1.nilienda kuchukua nguo ndo ilikuwa mara ya kwanza hvyo ckujua bei ya huku bongo
2.nilitaka kufunguliwa baro na kuchaguliwa grade A tu ya nguo, hvyo mnunuz anabak na makapi, wanaita furges wenyewe
3.kwa 7bu hzo hapo juu nilidondokea pua kwan nakumbuka sket ndefu niliuziwa elf 13, fupi elf 10 gauni ndefu 21elf, gaun fupi 15elf, tops elf 6, kwa mantiki hiyo nilivyorud bongo kusema ukweli hazikulipa kbsaa kwan hzo bei nilizochukulia ndo za kuuzia bongo.
Ila nilichanganya mzigo wa nguo za special zikawa zinalipa mfano skin surual nilichukua kwa elf 6 nauza 12, simple shuz 6elf nauza 12, n.k


May Allah bless Me and You
 
Uganda nguo ni bei nafuu sana kwa sababu nchi za America,Asia na Europe zimefanya uganda kama sehemu ya kupeleke nguo ,begi,viatu etc kutokana na kuwa hawana urasimu wa biashara na kodi ni kidogo sana.Tanzania kuna urasimu na kukandamiza sana wafanyabashara kwa njia za kodi.kule wanasapoti wafanyabiashara kwa vitendo.

Pia soko ni kubwa kuna watu toka tanzania,Kenya ,rwanda,Congo,Burundi,Eritrea,Ethiopia,China,India etc na hakuna sheria kali za uhamiaji kama tanzania kwa ufupi kule hakuna kufatiliana utaifa ni free kabisa.Twende kwenye maswali yako sasa,

Sehemu ambazo unaweza nunua mzigo ni city centre lakin mitaa ya Ben Kiwanuka,Tax park,Copper complex,Arua park na Owino market na sehemu jiran na Owino market.
Kwa vile unataka mitumba ingia Owino Market uko vitu ni bei rahis sana ila inahitaji ubageini na ni lazima ubageini,viatu ( TimberLand )ambavyo nanunua Tanzania 90,000 tzsh kule nanunua kwa 15,000-18,000 tzsh ila wanakuanzia mbali unaomba upunguziwe.
Uko Owino wafanyabiashara wanajua kiswahili vizuri ila ukiambiwa bei,wewe sema ambayo ni kidogo sana kutegemea na mzigo pia wakat unanunua ndio wakat mzuri wa kujua pia utauza kiasi gani.
Tshirt ya 15,000 tzsh pale unapata kwa 1,500 tzsh tena hiyo bei rejareja kwa wewe ukinunua kwa uwingi bei ni rahis sana.Uganda imefanywa kama dampo la bidhaa hizo na watu wa ulaya,asia na america.

Sehemu ya kulala maeneo ya copper complex kuna guest nzuri moja inaitwa Galaxy Guest house ni nzuri sana,bei zake ni ndogo sana kutegemea na unachukua room gani bei uanzia 15,000 ugsh hadi 30,000 Ugsh ndio bei ya juu kabisa.
room zipo ghorofan chini ni mgahawa,pia ukikuta imejaa jiran na hapo kuna nyingine Boston guest house ni nzuri pia na ata wafanyakaz wa hapo uongea kiswahili .bei zake ni ndogo.na hizo sehemu ni jiran na shoprite pia kutoka hapo hadi owino ni dakika 2 tu kutembea na hizo sehemu ndio kwenye maduka mbalimbali.

Kuhusu kodi,kuna mbinu inafanyika nitaku pm si vizuri nikieleza hapa.Kuna njia mbili za kwenda uko kuna njia ya kupitia Nairobi hadi Kampala na kuna jia ya kati hadi Bukoba kisha unapanda bus za Friends huondoka saa moja asubuh kutoka bukoba kwenda kampala,na saa sita na nusu uko kampala,ukifika hapo chukua bodaboda hadi Galaxy Guest house au Boston zipo maeneo ya copper complex jiran na shoprite ambapo kwa bodaboda haizid 2000 ugsh.

Pia ata maeneo ya Arua park kuna guest za kulala pia. ( hayo maeneo ni kama unavyoona kariakoo majina ninayotaja ni kama mitaa tu mfano msimbazi etc hizo sehemu ziko jiran jirani )

Rate za ubadilisha pesa ni 1.5 hadi 1.6
yani 1,000 Tzsh ni 1550-1600 Ugsh.
wakat ambapo shule zinafunguliwa rate inashuka sababu wanafunz wengi wa kitanzania wanakuja na pesa na wanachange inaweza pungua hadi 1.5 au 1.55.

kuna bus kama Falcon utoka dar kupitia njia ya kati hadi bukoba kisha kampala.
njia ya nai mfano kuna spider utokea dar-nairob-kampala.

ni wewe sasa kuamua,nawajua watu wengi wanawake/wanaume wamefanikiwa sana kimaisha kupitia biashara hii.cha muhimu ukinunua kitu uombe sana kupunguziwa pia usiingiwe tamaa za kununua vitu ambavyo hukupanga kuna vitu vizuri sana kule na cha muhimu kuwa makini ili usiibiwe pesa,uporaji kule hakuna labda mtu achane pochi yake bila wewe kujua.

mkiwa na swali ulizeni
nami naomba tuonane pm unipe mbinu za kodi plss stunna
 
Stunna webale nyo webalile dalla na a'kasigadeyo katwongeleko sebbo, ki ukweli ukitaka kuifaidi biashara ya nguo Kampala, hebu dili na nguo za special, nguo za mitumba kiasi fulani kuna ugumu japo inawezekana pia. Kama utatokea mutukula ukiwa unarudi ukifika Kyaka kuna figisu nyingi sana kuliko hata pale TRA ya mutukula,. Ila biashara ya nguo za special kwa kampala zinalipa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom