Biashara ya nyama choma

Biashara ya nyama choma

OllaChuga Oc

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
21,569
Reaction score
24,812
Mimi kijana wa Kitanzania mwenye umri kamili wa miaka 26, mwenye Degree moja ya Procurement, ni mjasiriamali wa biashara ya chakula, Matunda na Forex ..lakini bado naitaji kuongeza kitega uchumi kimoja na nimeona ni deal na vitu hivyo vya kula kula maana mimi mwenyewe nakimbiza (nakula) japo bado ni kimbau mbau tu sijui kwanini😭

Enewei nataka nianzishe hii Harakati ya kuchoma nyama hapa hapa jijini Arusha lakini nataka niwe na atleast vijana wawili ambao tutachangia mtaji atleast 500k (tsh laki tano) kwa kila mmoja ili kufanikiwa hili suala. Nimeona kwa kiasi hicho ndo itakuwa kianzio ila tukikutana tunaweza kufanya mchanguo mzuri.

Jumla tunakuwa watatu na mtaji unakuwa 1.5M; popote ulipo kijana unaonaje tukaunganisha nguvu na kufanya hii Harakati? Hii yote ni kutafuta namna ya kutoboa na kuwa na chanzo nyingi ya mapato.

Hivyo kama uko tayari nitafute tufanye kitu, itapendeza kama utakuwa na uzoefu na kuchoma nyama kwa sababu mimi sina. Ila niko vizuri sana kwenye eneo la location😀 hapo sijawahi kukosea kwakweli.

Lengo nataka badae tuwe na Restaurant ya kuchoma nyama tu. Ndo hivyo yani Nyama tu😃 ..nataka watu wasahau kwa mromboo na maeneo mengine wanayochoma nyama hapa jijini Arusha. Tutachoma nyama za aina zote hadi samaki wa kuchoma atakuwepo, tutajitahidi. Nyama za kuku,ng'ombe,mbuzi,kondoo,bata,sungura na hata nyama za pori kama itawezekana.(sitanii wakuu)

Hivyo nafasi mbili ziko wazi kwa vijana hawa bila kujali jinsia( ila 'Ke' wanapewa kipaumbele zaidi maana kwenye hii sekta wapo wachache sana) karibuni sana.

Pia mnakaribishwa kupata Chakula bora pamoja na matunda maeneo ya Sakina Raskazoni ili tuendelee kujenga taifa. Asanteni.

Namba yangu 0768 246184.

Motto wangu ni ule ule "Usipofanya kitu hakitatokea kitu"
 

Attachments

  • 20200929_162535.jpg
    20200929_162535.jpg
    74.9 KB · Views: 38
Biashara za collabo haxifai kabisa Kaka. Naongea kutokana na uzoefu wangu, Sababu wewe au mmoja wenu anaweza akawa na mawazo mazuri na ambition kubwa, yupo very dedicated Ila akaangushwa na patners wake , na kumbuka hao Ni patners huwezi kuwafukuza au kuwaamrisha Kama boss wao.

Jipe muda mwenyewe upate hiyo hela iliyobaki ufanye ya kwako mwenyewe, mtaalamu utaajiri mwenyewe.

Patnership Ni pasua kichwa Sana Sababu wabongo wengi uswahili na kutokuchukulia mambo kwa u serious unaotakiwa
 
Biashara za collabo haxifai kabisa Kaka. Naongea kutokana na uzoefu wangu, Sababu wewe au mmoja wenu anaweza akawa na mawazo mazuri na yupo very dedicated Ila akaangushwa na patners wake , na kumbuka hao Ni patners huwezi kuwafukuza au kuwaamrisha Kama boss wao
Jipe muda mwenyewe upate hiyo hela iliyobaki ufanye ya kwako mwenyewe, mtaalamu utaajiri mwenyewe.

Patnership Ni pasua kichwa Sana Sababu wabongo wengi uswahili na kutokuchukulia mambo kwa u serious unaotakiwa
Mkuu siyo Kwamba nakuchukua tu kwa sababu umekuja kiasi hicho cha 500k, najua partnership ni changamoto ila nitazingatia ushauri wako. Asante sana
 
Nipo dar na nipo tayari nina ujuzi kidogo sio sana kidogo ila naweza kuchoma mbuzi/ng'ombe/kuku naweza na kumpa mtu akala akajiskia kala nyama. vifaa na location huko ulipo ndio sijajua sasa.
Nipigie mkuu tuongee.
 
Back
Top Bottom