BIASHARA ya restaurant ni biashara inayohitaji usimamizi wa hali ya juu sana sana,
Ukiachana na ubora wa chakula unachopika bila mgawanyo wa majukumu ulio kaa
ukaeleweka biashara inakufia huku uki iangalia na sio kwamba wateja hupati ila ni wewe
muendesha biashara hutoona faida ya biashara unayofanya.Biashara Nyingi za restaurant
zilizokufa si kwamba wateja waliacha kwenda kula ila ni usimamizi mbovu uliopelekea upotevu wa faida.
Ukija kwenye Kuboresha huduma za upishi na vyakula na huduma kwa ujumla hizo ni added tips
za kufanya tu biashara yako iende mbele, wateja wa mabarabarani hawajali sanaaaaa mambo ya taste
wengi huja kula kwasababu wana NJAAA, wanajua kabisa kwamba hawawezi pata chakula kitamu mtaani
ndio maana wanakuja kula hvyo hvyo,Zipo restaurants nazijua zina miaka 5+ tangu nizifahamu
Asubuhi chapati zao ni sawa na maturubai,Mchana vyakula vyake ni vile hata juma nature anaweza Pika
lakini biashara inadunda miaka nenda rudi inaenda tu,Hamnaga hata siku moja nimekula hizo sehemu
chakula chao nisiende kuharisha,ni wachafu na wabovu ila biashara inapepea TU, WHY? Wanajua kui manage
Pamoja na chakula chao kibovu/kichafu ukitua tu pale muhudumu kafika umehudumiwa,hujakaa sawa
muhudumu wa vinywaji huyu hapa,ukiinua tu shingo ujinyooshe Muhudumu kaja anajua umemuita
Wafanyakazi wapo wa kutosha Cashier sio mmoja, Vinywaji vina cashier wake,Jiko la chakula Cashier wake
Nyama Choma Cashier wake,Asubuhi Cashier wake ni mgawanyo wa majukumu Hela haipotei kila senti inaonekana.
Ukiweza kuwa na management nzuri ya Restaurants hata kila siku upike vyakula vibichi,wateja wataendelea kuja
watakua wanakula huku wanalalamika,Biashara its all about time ukiweza okoa MUDA wa mteja yeyote
anaefika ofisini kwako akaondoka ON TIME umemaliza kila kitu,mambo mengine tunafanya ili kunogesha biashara zetu.
Wapishi wazuri chakula flani
Wapishi wazuri wa vitafunwa
waandaaji wazuri wa nyama choma
Yani huko kote ni kuongezea nyama nyama kwenye Biashara yenye management sahihi,Ndugu/rafiki yako biashara inamshinda sio kwasababu chakula ni kibaya ila sababu ni Ubovu wa usimamizi wa hiyo biashara.