Biashara ya Restaurant inamshinda ndugu yangu

Hizo biashara ni za wapemba mgoni wapi na wapi na hizo biashara, kila biashara inawenyewe.
Wapemba na Wasomali hawajawahi kufeli kwenye restaurants. Binafsi nimewahi kufanya hiyo biashara kwahiyo naielewa vizuri.

Kizungumkuti kikubwa cha hii biashara ni kupata wataalamu wa mapishi na ukitaka ufanikiwe katika hilo basi hakikisha wanakuwa ni wa kiume, wenye kujitambua na nidhamu ya kazi. Kingine ni customer care nzuri na usafi.

Shida ipo kwenye kupata hao wapishi wazuri.
 
Kama unampenda nduguyo mshauri...

Atafute wapishi hodari au wapembe upande wa vitafunwa, chips na nyama za kuchoma au kukaanga

Atafute wapishi wazuri wa misosi

Kwa kuwa ni restaurant atafute wahudumu nadhifu wa kike na wakiume wenye lugha nzuri Kwa wateja.

Mazingira yawe safi sana.

Vyakula viwe tayari Kwa muda muafaka

Mfano asubuhi saa 12:30 basi vinavyohusiana na kifungua kinywa viwe tayari mfano, chai, vitafunwa, supu na mtori, juice fresh

Ifikapo saa Tano na nusu Cha mchana kiwe tayari....hiki anaweza kuunganisha kikafika Hadi jioni.

Mkewe amuweke kusimamia wapishi wapike Kwa muda na mauzo.

Fridge amkabidhi mmoja wa wahudumu ili ikitokea loss iwe rahisi kujua wapi imepatikana. So huyo mhudumu mmoja kazi yake ni kuhudumia vinywaji, asubuhi anakabidhiwa vilivyomo kwenye fridge na vitavyotarajiwa kuongezwa, jioni wanavyofunga wanakabidhiana pia.

Jikoni pia amtafute mmoja awe msimamizi wa vitu vya jikoni maana wanatabia ya kuchukua vitu, so anayekabidhiwa ndio atahusika na lolote.
Azingatie huu ushauri.
 
Wapemba na Wasomali hawajawahi kufeli kwenye restaurants. Binafsi nimewahi kufanya hiyo biashara kwahiyo naielewa vizuri.

Kizungumkuti kikubwa cha hii biashara ni kupata wataalamu wa mapishi na ukitaka ufanikiwe katika hilo basi hakikisha wanakuwa ni wa kiume, wenye kujitambua na nidhamu ya kazi. Kingine ni customer care nzuri na usafi.

Shida ipo kwenye kupata hao wapishi wazuri.

Wewe umefanya biashara hii ndo maana Una uelewa...kuna watu wanadhani mtu yeyote Yule anaesema anaweza kupika unaweza muweka kwenye biashara ya vyakula....

Mapishi ya nyumbani na ya restaurant tofauti Sana .... kwenye biashara quality ikiyumba Tu unapoteza wateja
 
Hapo kumtoa huyo mke sasa ndo mgogoro huanza😁😁😁😁. Eti hapa dronedrake unasemaje?

Yaani wewe umenielewa ...
Kuna watu kumwambia mkeo mapishi yake ndo yanakufukuzia wateja ataona kama umemdharau mkewe......kumuelewesha kuwa anahitaji wapishi wa ukweli huku yeye anamuona mkewe bonge la mpishi...ni kazi Sana
 
Wewe umefanya biashara hii ndo maana Una uelewa...kuna watu wanadhani mtu yeyote Yule anaesema anaweza kupika unaweza muweka kwenye biashara ya vyakula....

Mapishi ya nyumbani na ya restaurant tofauti Sana .... kwenye biashara quality ikiyumba Tu unapoteza wateja
Nyumbani michapati ikiwa migumu mtaisokomezea mdomoni hivyo hivyo ila kwenye biashara mteja anaweza kukuachia hapo hela asilipe na ndio ukawa umempoteza hivyo
 
BIASHARA ya restaurant ni biashara inayohitaji usimamizi wa hali ya juu sana sana,

Ukiachana na ubora wa chakula unachopika bila mgawanyo wa majukumu ulio kaa

ukaeleweka biashara inakufia huku uki iangalia na sio kwamba wateja hupati ila ni wewe

muendesha biashara hutoona faida ya biashara unayofanya.Biashara Nyingi za restaurant

zilizokufa si kwamba wateja waliacha kwenda kula ila ni usimamizi mbovu uliopelekea upotevu wa faida.

Ukija kwenye Kuboresha huduma za upishi na vyakula na huduma kwa ujumla hizo ni added tips

za kufanya tu biashara yako iende mbele, wateja wa mabarabarani hawajali sanaaaaa mambo ya taste

wengi huja kula kwasababu wana NJAAA, wanajua kabisa kwamba hawawezi pata chakula kitamu mtaani

ndio maana wanakuja kula hvyo hvyo,Zipo restaurants nazijua zina miaka 5+ tangu nizifahamu

Asubuhi chapati zao ni sawa na maturubai,Mchana vyakula vyake ni vile hata juma nature anaweza Pika

lakini biashara inadunda miaka nenda rudi inaenda tu,Hamnaga hata siku moja nimekula hizo sehemu

chakula chao nisiende kuharisha,ni wachafu na wabovu ila biashara inapepea TU, WHY? Wanajua kui manage

Pamoja na chakula chao kibovu/kichafu ukitua tu pale muhudumu kafika umehudumiwa,hujakaa sawa

muhudumu wa vinywaji huyu hapa,ukiinua tu shingo ujinyooshe Muhudumu kaja anajua umemuita

Wafanyakazi wapo wa kutosha Cashier sio mmoja, Vinywaji vina cashier wake,Jiko la chakula Cashier wake

Nyama Choma Cashier wake,Asubuhi Cashier wake ni mgawanyo wa majukumu Hela haipotei kila senti inaonekana.

Ukiweza kuwa na management nzuri ya Restaurants hata kila siku upike vyakula vibichi,wateja wataendelea kuja

watakua wanakula huku wanalalamika,Biashara its all about time ukiweza okoa MUDA wa mteja yeyote

anaefika ofisini kwako akaondoka ON TIME umemaliza kila kitu,mambo mengine tunafanya ili kunogesha biashara zetu.

Wapishi wazuri chakula flani
Wapishi wazuri wa vitafunwa
waandaaji wazuri wa nyama choma

Yani huko kote ni kuongezea nyama nyama kwenye Biashara yenye management sahihi,Ndugu/rafiki yako biashara inamshinda sio kwasababu chakula ni kibaya ila sababu ni Ubovu wa usimamizi wa hiyo biashara.
 
Nimekupenda bure we kaka

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Yaani wewe umenielewa ...
Kuna watu kumwambia mkeo mapishi yake ndo yanakufukuzia wateja ataona kama umemdharau mkewe......kumuelewesha kuwa anahitaji wapishi wa ukweli huku yeye anamuona mkewe bonge la mpishi...ni kazi Sana
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Ndio maana tukaambiwa tusichanganye familia na mambo ya biashara madhara yake ndio hayo

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom