Hii biashara ni nzuri na inalipa iwapo tuu utazingatia 1) location ya goli lako, 3)Aina ya usimamizi, 3) huduma utakazotoa kulinganisha na salon za karibu.
Nafanya hii biashara mwaka wa tatu sasa, hii biashara wakabidhi vinyozi, hakikisha unamteka kinyozi mmoja ili awe overall incharge na ajione goli kama la kwake huku bila ya kusahau kuweka respect, (yaani wafanyakazi wako wakutambue wewe ni nani na wajibu wao ni upi katika kazi)
Vinyozi ni pasua kichwa sana, ila jitahidi kuwasom wanataka nini, lakini kuna muda hawaelewekagi , ila wakitulia wanatulia kweli, halafu vinyozi wanakuaga na roho za kwanini wenyewe kwa wenyewe.
Kama utafungua barbershop, mbilinge nyingine ipo kwa wadada, kwa upande wangu hawa ndio wasumbufu kuliko vinyozi, nilishasumbuka nao sana, baadae nikaja kukabidhi jukumu la wadada ikiwamo malipo ni juu ya vinyozi, mimi ninachotaka wateja wasikose huduma
Wadada wa scrub kwenye barbershop wanavutia wateja kwa asilimia kubwa sana, kwahiyo wakiwa bom, andika maumivu, hawa watu wachukulie usiwadharau japo ukipata wasiojielewa hawatofautiani sana na wahudumu wa bar, ila pia usigegede wafanyakazi wako.
soon nafanya ukarabati, mzigo wa zamani naupeleka wilayani kufungua kijiwe kipya ili walau grease ipatikane.