Biashara ya samaki

Habari wana jukwaa naamini mko salama,

Naombeni kujuzwa kuna sehemu nimechunguza kuna uhitaji sana wa samaki na mimi nikaona hii inaweza kua fursa maana nipo tu sina kazi ninayofanya.

Sasa lengo langu la kuja humu jukwaani ni kuwauliza wapendwa wangu na wazoefu wanaofanya hii biashara je ni kitu gani natakiwa kukifanya ili kufanya samaki hawa wawe na mvuto kwa wanunuzi( Samaki wa kukaanga afu nakaa gengeni kuwauza)

Naomba mnisaidie ili ninavyoanza niwaandae kwa standard ya kuwavutia wateja.

Natumai nitapata ushirikiano mzuri, nitasoma kila kitakachosemwa.
 
Mbona hii ni rahisi sana...nunua samaki kwa bei ya chini...wakate vipande kama ni wakubwa wakubwa au kama ni wadogo haina haja....wakaange,peleka gengeni... panga bei unayoona itakupa faida
Usiwe na tamaa ikaweka bei kubwa mno,utafukuza wateja.
 
Kwanza inatakiwa ujue ni aina gani ya samaki (kuna sangara na sato kanda ya ziwa bila kusahau kamongo na kambale) Kuhusu pwani sijui sana

Soko umeshasema ni uhakika sasa kazi imebaki ni wapi utawapata hao samaki, mimi pia najihusisha na hii biashara kiukweli inalipa

Kama upo kanda ya ziwa unaweza kunicheki tukabadilishana ujuzi
 
Kaka naomba unicheki 0782210033 nahitaji kuuza samaki wa kukaanga huko.
 
Kaka naomba unicheki 0782210033 nataka hiyo biashara ya samaki

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Biashara ya samaki ni nzuri mkuu. Mimi nauza wabichi sato,sangara,jambalaya,kamongo n.k. Ila naanzia kg. 100 nakuendelea mkuu.
 
Mbona hii ni rahisi sana...nunua samaki kwa bei ya chini...wakate vipande kama ni wakubwa wakubwa au kama ni wadogo haina haja....wakaange,peleka gengeni... panga bei unayoona itakupa faida
Usiwe na tamaa ikaweka bei kubwa mno,utafukuza wateja.
Nashukuru kwa ushaul
 
Nipo mafinga rafikiangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…