amu huyu
Zanzibar Spices anafanya biashara ya bodaboda, biashara ya kirikou, biashara ya kuuza mashuka ya kigoma, biashara ya.... biashara ya.... sema ninachompendea huwa sio mchoyo wa maarifa.
Mi ni msemaji wake kwa siku ya leo tu. ha ha ha
Hahaha,Mkuu njaaa mbaya,ndio nahangaika aisee.
Nikweli Bodaboda nafanya,na Carry nafanya,ila mashuka niliacha muda mrefu,maana soko kwa Zanzibar lilikufa.Kuna mashuka yanatoka UK yanauzwa matatu kwa pamoja bei rahisi,na watu kujua ubora wa mashuka ya Kigoma ilikuwa mbinde sana.Na Mitumba grande ya mwanzo huku Zanzibar telee,so ni sheeda sana.
Nimeamua kuingia kwenye usafiri maana sijaona changamoto ya kunishinda kwa muda wote wa biashara zangu.Nipo Zanzibar ila mfumo wa biashara ya usafiri unanipa nafasi ya kufanya yangu bila usimamizi mkubwa zaidi ya ndugu yangu mmoja tu ndio namlipa mshahara kwa mwezi ili awe msimamizi na nilimpeleka Gerage Pale Magomeni then nikampandisha VETA,basi kesi za Gari zangu hizo mbili tatu,sina kabisaa na Drivers wangu wote watu wazuri saaana,maana nawafanya kama familiy members.
Na pia ununuzi wa Vigari hivi kwa Zanzibar kwa sie Wajanja mpaka 4m naitoa yard,maana huku Zanzibar ukitaka gari we chukua pesa weka ndani wala usiwe na haraka kabisaa,kuna siku utanunua gari ubweteee,maana kuna watu wanaleta gari ili kuziba gepu la pesa kidogo ya kutolea mizigo au gari nyingine bandarini,sasa hawa Magari kwao sio biashara.Na wapo ambao wao ni biashara na ndio ghali kiasi.Maaana Mwezi uliopita kabla sijasafiri kuna jamaa alikuwa na Noah kamnunulia mama yake anauza kwa 7m tu liteace mbichii,maana mama yake aliletewa gari nyingine na Kaka yake.
Mjini kaka ni kutuliza akili tu ndugu yangu,maana maisha haya ya wendawazim na wewe ukijifanya mstaarabu hamuendi,maisha yakiwa kichaa basi wewe kuwa kichaa zaidi,yakiwa yametulia na wewe tulia.Ila ukienda tofauti tu basi umepotea na ukipanic basi safari ya Dodoma hiyooo.
October mwishoni nataka kuingia kwenye NOAH,maana naanza na moja nikikolea naongeza.
Mkuu maisha safari ndefu kaka,niliuza Nyumba mie kwa ajili ya Biashara,nikatengwa na Brothers wa upande wa Baba na nilipata Support kubwa sana kwa Only Sister ambae tumezaliwa Mama mmoja kwa kunipa moyo sana katika mapito ya maisha baada ya kuachishwa Kazi kwa mambo ya Siasa.
Mafanikio ya Maisha kwa Vijana yapo kwenye Nyayo za Marafiki bora tu.Muhim ni kujitambua kwamba maisha yako ni wewe na sio mwingine.Na ukikosea wa kujilaumu ni wewe na sio Mzazi wako au mwenzio.Na waliofanikiwa weengi duniani ni wale waliokosea sana kwenye maisha ya kutafuta.Ukikosea na kujitambua kwamba umekosea basi jua Mungu anakupa njia ya kwamba ukipata ujue ulipotoka na ujue kwamba Maisha sio ya kuchezea.
Wapo waliopata mamilioni ya pesa na tunawajua mitaani kwetu au makazini kwetu ila leo wapo taabani sana.Wapo watakaoibuka tena upya na wapo wataopotea kabisa kama watamuweka mungu Mbali na kukubali makosa yao.
Hakuna kitu kinachotuangamiza vijana na kumkera Mungu saana pale anapotupa rizki na kuitumia kumuasi yeye mwenyewe alietupa tena mbaya zaidi kwa kile kipato cha mwanzo cha ufungua wa maisha ndio kinatumiwa vibaya,na ndio maana kwenye makanisa na miskiti kwa sasa weeengi sana ni Vijana.
Na kila mmoja kwenye maombi anaomba maisha mazuri,ila mungu anachelewa baadhi yetu kutupa kwakuwa anajua nafsi ya kila mmoja wetu,na wapo ambao wanaomba mungu huwezi amini haipiti mwezi wanafanikiwa,ila subiri muda mfupi tu,wanasahau kila kitu na kuona kwamba wao ndio wajanja na akili zao ndio zimefanya wafanikiwe,jeuri telee,dharau teleeee.Na kuona wanaoenda kwenye Nyumba za Ibada woote ni wenye Shida ya Utajiri wa Dunia kama yeye,na kuona kwamba wao hawawezi kufanikiwa kama yeye.Kumbe hajui kwamba Kule watu wanafuta Baraza za mungu tu,Unaweza kuwa Milionea na huna baraza za mungu ni sawa na Bure,na kuna mtu analalia ugali maharage akawa juu sana kwenye daraja la mungu kuliko wewe.Na akawa na amani na furaha na maisha na familia yake kuliko wewe mwenye kujiona Unakipato.
Na ndio maana pia unakuta kuna vijana mara miezi hii wapo nyumba za Ibada kama kawaida,mara baadhi ya miezi wakifanikia haoooo,wanasepa.
Mungu atubariki sote na atupe wepesi kwenye maisha yetu na atufungulie pale tumepokwama,na atupe maamuzi sahihi kwenye maisha kwa faidi ya vizazi vyetu na Imani zetu,na pia atuongoze pale anapotupa kipato ili tusiweze kukitumia kumuasi yeye mwenyewe "AMEEN"