Bei ya sangara na sato inatofautiana. Sato siku zote iko juu. Kwenye kipindi cha mvua samaki wanapatikana wengi na kwa Bei nafuu. Kipindi hiki samaki sangara kilo kwa jumla ni 4500. Wakati sato anaenda mpaka 5500.
Samaki wanapimwa kwa kilo. Unaweza kununua moja kwa moja kutoka kwa wenye mitumbwi yao au kutoka kwa walanguzi ambao wao huzinunua kwa wingi na kuzihifadhi Kwenye mafriza baada ya kuwatoa mautumbo na mabondo.
Hawa walanguzi ndiyo wenye Bei niliyokupa hapo juu. (Ukumbuke Bei hubadilika ) walanguzi hawahawa ukitaka samaki wanakufungia vizuri na kuwapakiza Kwenye mafuso. Fuso zote zinapakulia pale urafiki freti. Ila unalipia usafiri mwenyewe.
Kuhusu kibali mlanguzi huwa anakibali na mwenye fuso anakibali cha usafirishaji. Na ushuru utalipwa na mlanguzi. (Ukitaka namba ya mlanguzi utaniambia).
Bei ya kuuza huku samaki mbichi kilo ni kuanzia elf 8-10.
Of course ukitaka kuwa na frem lazima uwe na leseni nenda halmashauri na tra lazima ikuhusu.
Ukitaka nafuu sambazia mzigo ukiwa home kwako.