Biashara ya Stationery: Ushauri, Vifaa, Gharama na Mbinu za Uendeshaji


Nashukuru kwa ushauri wako wa thamani sana kwangu. Mambo mengine nilipanga kuyafanya ulisoyasema mfano pita pita mashuleni na vyuoni kuelezea ile uniqueness ya biashara yangu na pia namtegemea MUNGU. Asante
 

Nilipo ajiriwa sio rasmi mfanyakazi na volunteer huku nalipwa allowance due to performance of the work. Hivyo salary slip sina nalipwa dirishani.
 
God be with you malengo yatatimia ni hatua nzuri sana!
 
Wakuu nimepata wazo la kuanzisha Browsing Center(sijui ndio internet cafe hapa bongo) Baada ya kuona nina computer kama 4 hivi zimekaa bila kazi hivi nikitaka kufungua biashara ya cafe nkaomgezea na computer kama 4 hivi itanigharimu kiasi gani!(TAFADHALI UWEZO WA WANGU WA KOMPUTER NI USED!
 

Inategemea na chumba ulichopata,na internet tumia ya ttcl ni cheap sana kwa kifurushi cha speed ukiwa na computer ata 10 ni sh 40,000 kwa mwezi. hivo kwa hizo computer 4 unaweza chagua kifurushi cha bei chini ya apo.

Gharama zao jumla ya moderm na kukufungia inakuja 55,000/= hivo chumba inategemea na wewe= kufanya wiring yani kutoa wire kutoka kwenye moderm kwenda kwenye d link kisha kwa computer ni gharama ndogo inategemea na mtu aliokufanyia kazi hiyo.

D link router ya 8 port ni 70,000/= tafuta ya 8 port ili ukiongeza kompyuta na kufika 8 usipate tabu ya kununua tena hiyo router.

kiti na meza hakuna bei moja ni wewe tu.

kazi kwako tu
 

Kwaiyo wewe unamshauri atumie TTCL kwa vile ni cheap? TTCL wanazingua sana bora atafute ISP mwingine!
 
kwaiyo wewe unamshauri atumie TTCL kwa vile ni cheap? TTCL wanazingua sana bora atafute ISP mwingine!

TTCL ni nzuri matatizo uwa ni mara moja moja sana,lakin yeye pia anayo haki ya kuchagua baada ya utafiti wake,mi nimetoa tu ushauri
 

Am impressed. Jibu zuri sana umetoa.Nina huu mpango wa business hii pia
 
fered mbataa,

Kwa jinsi ulivyojielezea hata ungekuwa na hati ya nyumba ingekuwa ngumu bado kupata mkopo.

Benki haikopeshi mtu eti tu kwa sababu ana dhamana ! la hasha! , cha msingi wanachoangalia ni uwezo wako wa kulipa. Hii wataipata kwenye mzunguko wako wa biashara na kutazama iwapo unapata faida hasara, unadai, unadaiwa? nk
 
kila kitu kipo tayari computer kama kumi tatizo sijajua gharama za bundle ntanunuaje wakuu msaada
 
Kila kitu kipo tayari computer kama kumi tatizo sijajua gharama za bundle ntanunuaje. Wakuu msaada.
 
Vizuri mkuu ila kumbuka kuweka huduma ya wireless ili kuvutia watumiaji wa sim za smartphone kuja kufanya yao hapo vinginevyo hutapata wateja changamoto ni kubadirisha password kila mara.
 
Khaa, hii biashara ni ngumu kama vile kuendesha kampuni ya ndege. Nilifungua nikafunga ndani ya mwezi.

Rent 300,000, TTCL bundle Tsh 200,000, umeme 100,000, salary ya mhudumu 150,000, bado ulinzi na gharama nyingine jumla unajikuta unabidi uspend kama 700,000 kama fixed cost. Sasa na vile wateja wa kudunduliza. Bora ufungue mahali amabapo population ya watu ni kubwa, kama wanafunzi wa chuo vile.
 
Kamuulize Shirima wa Precision air, fly 540, au Joyce wa Quantas air ya Australia. Hao wachache watakwambia ilivyokuwa ngumu kupata faida kwenye kampuni ya airlines.
 
Tatizo siku hzi internet acces iko juu, wateja ni wachache sana labda, na ukiweka maeneo ya chuo nako vile vile kugumu vyuo vingi vina WIFI, So inategemea na eneo ila kiujumla hii busines utapiga pesa wakati wa matokeo.
 

Hapa mpaka nimecheka chezea biashara hyo wewe ndio maana shirika letu lilikufa ATC.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…