Biashara ya internet cafe africa na Tanzania kwa ujumla bado ni big deal, cha muhimu ni location tu ambayo mtu anahitaji kusite. Mi nipo kwenye hii biashara tangu 2007 na nimesoma A'level na chuo kwa mgongo wa hii biashara ya internet cafe ambayo wengi wetu hapa wanaona kama imekufa kibudu.
Ni kweli ujio wa smartfones umepunguza biashara ya internet cafe , nacho amini kila siku katika hii biashara, Biashara ni wewe mwenyewe unavyo ihandle, speed nzuri ya mtandao, mazingira safi na machine zako zikoje hasa katika mantainance. internet cafe nyingi zimekufa hasa kutokana na wengi kufanya biashara hii bila kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu computer, matengenezo na n.k. hivyo kuwafanya kuwa watumwa kwa mafundi computer kitu ambacho kinapelekea kuua mitaji na machine kufa.
Tusidanganyane kwamba eti kwenye simu na tablet waweza surfing kama unavyofanya kwenye computer, na simu zenyewe zinavyokula chaji kama zina majini. Jipange na simamia biashara yako kwa uhakika bro, speed iwe ya uhakika na ufanye mantainance....utaenjoy hii biashara.