Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wadau bado mmelala??



Habari za asubuhi wadau wa jukwaa hili,
Natumai miongoni mwetu kuna watu ambao wanafanya biashara tajwa hapo juu, waliowahi kuifanya na wenye idea na biashara hiyo.
Je ni vifaa gani vinavyohitajika na vya muhimu ili kuendesha biashara hiyo? Ni mahali gani ninaweza kupata vifaa hivyo kwa bei nzuri na genuine? Ni jinsi gani unaweza kumonitor biashara hiyo? Na kama kuna angalizo ama chochote ambacho unakifahamu kuhusu biashara tajwa tafadhali usisite kutoa mchango / mawazo yako.
Natangulisha shukrani.
Wasalaam
CL
cousin cha muhimu uanze kupanga flemu mahali ambapo kuna shule, vyuo, sehemu ambazo watu wanapita pita sana ili wakiona waingie na kuhudumiwa
b) ni vyema uwe na vifaa vifuatavyo:
1. Photocopy mashine aina ya canon au yoyote ya kuanzia
View attachment 175771
2 uwe na computer na printer View attachment 175773
View attachment 175774
c?) uwe na scanner, lamination machine ndogo ya kuanzia na paper cutting machine
ikiwezekana uwe na list ya vifaa vya shuleni na maofisini kwa kuuza na vitabu mbalimbali vya shule
kwa upande wa scanner siku hizi kuna printer ambazo zinakuwa 4in1 ni nzuri yaani zinakuwa na
copy, fax, printer na scanner hapo hapo
kuhusu upatikanaji wa vifaa hivyo ni vyema kabla ya kuanza kulipia flem ni vyema ukaenda madukani kkufanya window shopping kwani kuna maduka yanauza bei chee na meingine yanauza bei ghali inategemea na kule huo mzigo alikoutoa kingiine ni muhimu uangalie kwenye website ya ebay ili uone bei za huko nje zikoje ukipenda unaweza kuagiza ni hayo bestito
Shukrani sana Cousin... Nimefatilia bei ya vifaa hivyo. Bado nafanya mchakato wa stationeries kujua nitaagiza wapi!
bigup umefanya jambo la maana sana cousin kwani ni muhimu uwe na shughuli yako mwenyewe hata kama uko kazini kwani ile biashara yako itakuongezea maradufu mkuu ngoja nami nikuulizie huku bei ya hvyo vitu pindi ujapo uweze fanya window shopingi mwenyewe na kujionea kwani kuna maduka ambayo yanauza bei rahisi na ni bora na upande mwengine unaweza kuagiza kupitia hawa alibaba kwani wao bei zao ni nafuu sana ila kuwa makini sana na online marketing binamu karibu
Nimejaribu kupita aliexpress ila naona shipping bei kubwa sana, inakuwaje. Hebu nidadabvulie basi.
Ingawa wengi wanakushauri ununue hiki na kile na kile ila mimi nakushauri jaribu kupunguza overheads as much as possible yaani kwa kuanzia nunua hata vitu used wakati unajifunza na kuzoea kazi
Computer.., kwa kazi za kawaida za kuchapa hauitaji computer ya kisasa hata zile za CRT na Pentium IV au chini ya hapo inafaa sana tena hata used.., kwahio kwa hapa hata chini ya laki mbili unaweza ukapata..
Scanner ni bei rahisi ila hata kama hauna unaweza ukaanza kazi
Photocopy hapa chukua used tena ukichukua IR series unaweza ukapata ambayo ina-print kwahio una-connect inakuwa inaprint hence bei ya printing inakuwa sawa sawa na photocopy ila nakushauri ununue pia laser printer sababu opc ya copy inaweza ikawa chafu kidogo mtu akakubali hio kama photocopy ila asikubali uki-print (quality yake ikawa sio kubwa)
Printer hapa angalia wateja wako kama unaprint sana kadi za harusi na rangi unahitaji inkjet printer (ambayo unaweza kununua epson yenye mitungi ya nje) au kama haufanyi printing kwa sana unaweza kununua hata hp tu ila catridge bei kubwa sana hivyo itabidi uwe unafanya refilling kwa sindano.. (kwa mwendo wa kununua catridge mpya huwezi ku-break even sababu hizi catridge ni bei ya juu sana kulinganisha na soko/bei wateja wanayotaka).. Kama una-print sana black and white ni muhimu kuwa na laser printer (nadhani hizi zinaanzia kwenye laki mbili au chini kidogo) tatizo la hizi catridge yake bei mbaya nadhani mtaani unaweza kuipata kwa kwenye elfu 70 mpaka laki na nusu.., ila dawa hapa kila wino ukiisha unafanya refilling na sio kununua mpya unaweza hata ukafanyiwa refilling kwa elfu 15.., na hii inaweza kutoa kama copies 2000
Mengineyo Sababu hii biashara imeshaanza kuwa saturated watu wengi wanafanya kwahio bei ni za chini sana usipokuwa mwangalifu au kujua undani wa biashara unaweza ukafunga baada ya muda mfupi.., mafundi wanachakachua sana pindi vitu vikiharibika pia wafanyakazi wanaiba vile vile unaweza ukashaangaa matumizi yanazidi mapato.., hivyo kuwa mwangalifu kufuatilia kazi (mfano mashine za ir series zina count hivyo unaweza ukajua ni copies ngapi zimetoka) as well as jifunze mashine ujue makosa madogo madogo sio kila mashine ikikwama unaita fundi (bei utapigwa kubwa as well as kuibiwa spare)
Subsidize na Vingine usitegemee dukani faida ya copy na kuchapa kazi peke yake (ukizingatia bei za copy zinaenda as low as tshs 30 na printing as low as 100 na kuchapa kazi hata chini ya 500/=) ongezea na vitu vingine kidogo kidogo mfano kuuza pen, madaftari, karatasi (ingawa faida yake ndogo sana), mmpesa (kama mzunguko ni poa hii inaweza kulipia hata chumba na mfanyakazi), luku, voucher n.k.
Shukrani sana mkuu kwa ushauri wako...
Nitaufanyia kazi, ila hapo kwenye Used machine hujanishawishi, naogopa sana tena sana make nilishaumwa na nyoka, nikisikia hata unyasi nahisi ni nyoka.
Siongelei used kutoka bongo kwa photocopy sababu photocopy nyingi zinazotoka dubai na nje ni used.., alafu kuna copier zinaweza zikawa mpya ila sababu sokoni hazijatumika sana haujui matatizo yake au spares zake sio nyingi... pili kuweka labda mtaji wa 1.5m au laki nane kuchukua PC mpya wakati ya Laki Mbili ingefanya kazi sioni kama ni kutumia rasilimali vizuri.., bora hizo pesa zinazobaki ungeongezea kwenye mtaji mwingine wa vitu vidogo vidogo..
Labda kwa swali nikuulize unapanga utumia kama tshs ngapi kwa kununua vifaa ? na huenda ukanunua vifaa kibao kwa kuanzia kabla haujajua soko la hapo.., huenda ukachukua lamination machine ya bei mbaya kumbe pale wateja wengi ni wa binding au ukanunua epson yenye mitungi ya nje ku-print color kumbe hapo wateja wa printing rangi ni wachache na mashine kukaa bila kazi inapelekea kuziba.. (kumbe kwa kuanzia hata hp ya kawaida ingetosha)
Nimepata darasa zuri sana kuhusu biashara ya stationary charminglady umewasaidia wengi kwa maswali yako ya ufahamu
Wakuu Mimi naumizwa na namna ya kufanya monitoring kwenye mapato ya photocopy! Kijana Wa kazi ananipiga maboblish siyo kidogo! Hebu aliyefanikiwa kudhibiti wizi kwenye hii kazi anisaidie mbinu, mwisho nitafunga kijiwe wakuu!
Tupo!
Niliwahi kupata ushauri wa hii biashara mwaka jana, nikashawishika kuifungua. Inahitaji usimamizi wa karibu kwani mauzo yake ni kudunduliza eg photocopying.
Niliifungua Nganza (nadhani upo Mwanza) jirani na Kanisa Katoliki. Niliifanya kwa miezi mitatu nikiwa na imonitor kwa karibu.
Hatimaye nilihama kikazi kwenda mkoa mwingine na kumwacha mdada wa kazi akiendeleza hadi muda huu.
Kwa kuwa unataka vifaa kwa reasonable price, basi nimeorodhesha hapa chini kama utakuwa interested, tuwasiliane kwa pm.
- Photocopy machine kubwa- ina print na kutoa copy
- HP printer/scanner- black/colour
- Laminating machine
- Spiral binding machine
- Steppler machine kubwa
- Desktop Pc
- Paper cutter
- office table
- office chair