Biashara ya sukari sasa imekuwa kama ya ngada, tupo tayari kununua sukari hata kwa 4000/= ipatikane tu

Biashara ya sukari sasa imekuwa kama ya ngada, tupo tayari kununua sukari hata kwa 4000/= ipatikane tu

Niko tayari kununua vitu vingine nielekeze sukari ipo duka gani

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii Arusha Mkuu sema maeneo mengine huku inapatikana kwa bei elekezi tuu mengine ndio hakuna kabisa Kama ipo baadhi ya maduka ya mjini wanakuuzia mpaka wakujue kwa bei yao ili usilete wazee...wengi wanaouza uji mjini wanajua machimbo sukari ilipo hata huko watumie hao utapata sukari...
 
Mwez wa nne na wa-tano wanasimamishaga uzalishaji kupisha maintenance na miwa iliyooteshwa kukua
Usiamini kila wanachosema kwa nini hiyo kitu ianze miaka hii ya kuanzia 2012 kuendelea? Huko nyuma hawakua wanafanya maintenance?? na hiyo miwa inayosubiriwa kukua sasa hivi kwani zamani ilikuwa inatokea wapi? Kwanini wasipishanishe miezi ya kufanya matengenezo baina ya viwanda vyetu?

Mathalani tuna viwanda 8, basi vitano vifanye kazi na hivi vitatu vifanye matengenezo yao kwa miezi miwili kisha vianze kazi? Baadae vifuate tena vingine vitatu kisha wamalizie na viwili na kwanza hakunaga utaratibu wa kufunga uzalishaji wa kiwanda chochote kila mwaka kisa ni maintenance ingekua hivyo basi ingekua kawaida kabisa nchi kukosa umeme kwa miezi kadhaa, kukosa vifaa vya ujenzi kama cement, bati, misumari, nondo nk kisa kikiwa ni viwanda vinatengenezwa

Kwa hiyo viwanda vya sukari tu ndio vinaharibika kwa kufanya kazi sana? wenzao wenye viwanda vingine wao hawaharibikiwi? Huu ujinga sijui utatuisha lini watz kama tatizo ni miwa inaachwa ikue mbona mazao mengine kama ngano yanayotumika sana kwa kazi tofauti huwa hayakoseni, bia zinanyweka kama kawaida mwaka mzima, maandazi, chapati, keki zinalika mwaka mzima, sembuse miwa ambayo mashamba ya miwa mengi nchini yanalima miwa kipindi chote cha mwaka maana wana mifumo ya umwagiliaji mashambani.

Huu ni ujinga....waseme ukweli tatizo ni nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Arusha Mkuu sema maeneo mengine huku inapatikana kwa bei elekezi tuu mengine ndio hakuna kabisa Kama ipo baadhi ya maduka ya mjini wanakuuzia mpaka wakujue kwa bei yao ili usilete wazee...wengi wanaouza uji mjini wanajua machimbo sukari ilipo hata huko watumie hao utapata sukari...
Hii ni kwelo kabisa,ukitaka watume hasa hasa mama mtilie unaweza kupewa na asiulize kama ipo
 
Wakuu hili suala na utamu kwa maana ya Sukari kwa Sasa ni Kama wafanyabiashara wameamua kuigomea serikali.

Kuna maeneo Bei Sukari imekuwa juu na mamlaka zinazohusika zipo kimya Kama hawaoni na hawajui nini kinaendelea.
Huku Chanika Sukari kilo moja no Tsh.7000/=

Wananchi tunajiuliza inamaana hakuna hatua au malmaka za kushughulikia tatizo hili?
 
Waimba mapambio watasema.

'Kama sukari ni ghali achana nayo tumia chumvi'.
 
Wakuu hili suala na utamu kwa maana ya Sukari kwa Sasa ni Kama wafanyabiashara wameamua kuigomea serikali.

Kuna maeneo Bei Sukari imekuwa juu na mamlaka zinazohusika zipo kimya Kama hawaoni na hawajui nini kinaendelea.
Huku Chanika Sukari kilo moja no Tsh.7000/=

Wananchi tunajiuliza inamaana hakuna hatua au malmaka za kushughulikia tatizo hili?
Njoo kitunda 4000 unachukua kilo zako tano swaaaafi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo nimenunua sukari za kupimwa kwenye mzani kwa Tsh 3000, Nikanunua kilo 2 fasta maana niliulizia karibia maduka mawili kulikwa hakuna kabisa nilivyoifuma nikachukua kilo mbili fasta.
Eti nilivoifuma[emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom