Biashara zooote za wanyama wadogo kama kuku bata mende sungura ni mkakati wa kitapeli kuwavuta wengi waingie ili inspirational speakers wapate hela, wauza vyakula na madawa wa wanyama hawa wapate hela mengine wanakuachia wewe mwisho wa siku kama utabahatika utakuwa na wingi wa hao wanyama lakini huna pa kuuzia kurudisha hela. heti: kilo moja ya mende China ni laki tano??? Jamani muogopeni Mungu. Sasa ingia mkenge uanze kufuga hao mende utauziwa mende mmoja wa mbegu 15,000 nautaambiwa unatakiwa uanze na mende 10 kwa kiasi cha 150,000. Hiyo semina ya jinsi ya kufuga mende unalipia kiingilio kwa mtu ni 50,000 wakipatikana 20 inspirational speakers kaishaula. Utauziwa chakula special cha mende kilo 35,000 na utaambiwa mpaka wakue unatakiwa ununue kilo 10. Utaambiwa ununue madawa ya kufanya wazaliane, kuwakuza na kuwafanya wawe na uzito, n.k. Amaaa kweli nyakati hizi za mwisho watu wanapigwa na kubaki mafukara wa kutupwa