Majimoto kwa kweli nimesoma kwa siku moja na ikibidi kuipia tena ila kuna swali hapo juu umeulizwa kwa wale waliokwishapata kikombe wafanayeje basi waepukane na hiyo Mauti/Kifo
Swali langu jingine ni kuwa nimekuwa nikiangalia sana vipindi wa Emmanuel Chanel na kuna siku alikuwa anasema kuna laana ya kufilisika ambayo huandama kizazi hadi kizazi,kweli nikarecall na kwetu babu yangu upande wa baba alikuwa tajiri sana mwenye mali yakiwemo mashamba na ni wa kwanza kuwa na gari kijijini hapo Kilimanjaro,yaani ameishiwa imekuwa historia,ikafuata kwa wazazi naye baba alikuwa vizuri,zilimwandama kesi za ajabu ajabu,na kuibiwa na hatimaye hayuko vizuri kama zamani,baba mkubwa naye alikuwa na kampuni ya Utalii hapo Arusha Kakakuona Tours hadi kupata tuzo ya kuendesha huduma hiyo vizuri huko Spain,jamani amekuwa choka mbaya.
Kwani ilitokea tu akawa hasimamii shughuli za ofisi vizuri kama hapo awali,akawa ana shinda bar hakuwa hivyo awali lakini ilitokea hivyo tu.
Baada ya kuona hivi na kukagua kizazi cha upande wa baba hii inawatafuna je inaweza kuwa ni laana au ni jini katumwa?
Nitakupm ili kupata maelezo ya maswali personal zaidi
Mary Chuwa, Zamani wazee wetu walikuwa wakifanya matambiko ya aina mbalimbali kwa mizimu, matambiko hayo shabaha yake ilikuwa ni kuomba ulinzi wa mizimu iwalindie ukoo, ilinde watoto au mizimu isadie mvua zinyeshe kipindi ambacho kiangazi kimepitiliza sana na mvua kuchelewa kunyesha au kama kuna jambo lolote lisilokuwa la kawaida limetokea kwenye ukoo au familia, matambiko haya yalikuwa yanafanywa kuomba msaada wa mizimu, matambiko haya bado yanaendela kufanywa na familia nyingi.
Mizimu ni nini? Watu wengi wanafikiri mizimu ni ndugu wa ukoo waliofariki miaka mingi sana (mababu na mabibi). Mara nyingi utakuta ukoo au familia zina Mzee wa ukoo, ambaye ndiye anayeratibu taratibu zote za kufanya matambiko. Kimsingi hakuna uhusiano wowote ule kati ya mizimu na mwanadamu. Mara nyingi matambiko hufanyika kwa kuchinja wanyama na damu ya mnyama hutumika kuomba dua kwa mizimu iwatendee mambo yote wanayoyataka yafanyike, kisha hufuatiwa na viapo vya ukoo kwa mizimu kuwa watafuata yale yote mizimu itakayo sema wayafanye.
Matambiko kwa lugha nyingine tunaweza kusema ni kamba za kuzimu, zinazowafunga wanadamu wakiwa duniani. Mizimu ikishafunga ukoo kwa kamba shughuli yake huwa ni pevu kijinasua. Mizimu huifanyia familia jambo lolote ovu jinsi wanavyoamua, na jinsi wapendavyo, hizi kamba za kuzimu ni sawasawa kabisa na unavyotumia remote control ya television kubadilisha vipindi mbalimbali bila kuwepo na waya wa moja kwa moja toka kwenye tv hadi kwenye kitufe cha kuongozea tv. ndivyo hivyo hivyo mizimu inavyoyumbisha maisha ya watu wakiwa kuzimu kwa matatizo na magonjwa ya kila aina.
Familia nyingi zimekuwa mateka wa mizimu, kwa makosa yaliyofanywa na wakale wetu, na mizimu kwa kutumia remote control wameendelea kutaabisha familia nyingi, kiasi kwamba utakuta ukoo karibu wote wanaugua aina moja ya ugonjwa unaofanana kama kichaa, sukari, mapigo ya moyo n.k. au utakuta familia inaanza na maisha mazuri yenye wasomi wazuri na vipato vya kuridhisha, lakini mali hutoweka na huishia katika maisha ya mahangaiko na ufukara wa kutupwa. Familia nyingine utakuta wanawake hawaolewi au wakiolewa ndoa haidumu. Familia nyingine kila mwaka na mwezi unaofanana ni lazima afe mwanaukoo. Familia nyingi zimefungwa na kamba za kuzimu bila ya kijijua, anapozaliwa mtoto mizimu muda huo huo kukifunga kichanga hicho kwa kamba shingoni, na hali hiyo huendelea kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
Kila mwanadamu mauti inapomfika ni lazima anapokelewa, familia iliyofungwa kwa kamba za kuzimu anapofariki shughuli yake huwa ni kubwa na kifo chake huwa na mahangaiko yasiyokuwa ya kawaida. Roho ya mwanadamu inapoachana na mwili macho ya kimwili hufunga na macho ya rohoni hufunguka, macho ya rohoni yanapofunguka huwaona wenyeji wake waliokuja kumpokea, wale aliokuwa akiwaita mizimu ya babu na bibi, kumbe ni majoka ya kutisha, yanapokuja kumpokea, yanakuja na vicheko na kumdhihaki na huanza kumshika mgeni wao ili waondoke naye. Mtu wa aina hiyo anakuwa anaongea lugha ya mizimu, ambayo wanaomuguza hawaelewi maana yake, lakini huwa anakataa kuondoka nao, akijaribu kuwafukuza. Wanapoanza kumshika ndiyo maana utakuta mtu aliyefungwa kwa kamba za kuzimu anatupatupa miguu na mikono kila upande ili majoka wasimshike.
Mtu asiyefungamana na kuzimu, roho yake inapoachana na mwili, macho yake ya kiroho hufunguka na huwaona wenyeji wake waliokuja kumpokea, wenyeji wake huwa ni watu waliovaa mavazi meupe kabisa na nyuso zao zinang'aa, anapokelewa kwa nyimbo nzuri ajabu, kinachofanyika kwa mtu huyo, mikono yake huilaza juu ya tumbo lake na anakufa akitabasamu akifurahia nyimbo tamu za wenyeji wake.
Mary uwezo wa kukata kamba za kuzimu zilizoifunga familia yenu ya Chuwa upo mikononi mwako, inawezekana kabisa na ni jambo jepesi.