Biashara ya Uchawi Tanzania

Biashara ya Uchawi Tanzania

Majimoto pia kuna hili suala la mama wajawazito unakuta alikuwa hana shida yeyote ile lakini mwisho wa siku karibu na kujifungua linaibuka tatizo na kuambiwa kuwa wewe ni lazima tukufanyie upasuaji,je nalo hili linasimama upande upi Kiroho,kwani hiyo imekuwa sana kuna hospital moja hapo Arusha imekuwa na Sifa hiyo wengi wanaokwenda hapo ni hilo huwapata.
 
Majimoto kwa kweli nimesoma kwa siku moja na ikibidi kuipia tena ila kuna swali hapo juu umeulizwa kwa wale waliokwishapata kikombe wafanayeje basi waepukane na hiyo Mauti/Kifo

Swali langu jingine ni kuwa nimekuwa nikiangalia sana vipindi wa Emmanuel Chanel na kuna siku alikuwa anasema kuna laana ya kufilisika ambayo huandama kizazi hadi kizazi,kweli nikarecall na kwetu babu yangu upande wa baba alikuwa tajiri sana mwenye mali yakiwemo mashamba na ni wa kwanza kuwa na gari kijijini hapo Kilimanjaro,yaani ameishiwa imekuwa historia,ikafuata kwa wazazi naye baba alikuwa vizuri,zilimwandama kesi za ajabu ajabu,na kuibiwa na hatimaye hayuko vizuri kama zamani,baba mkubwa naye alikuwa na kampuni ya Utalii hapo Arusha Kakakuona Tours hadi kupata tuzo ya kuendesha huduma hiyo vizuri huko Spain,jamani amekuwa choka mbaya.
Kwani ilitokea tu akawa hasimamii shughuli za ofisi vizuri kama hapo awali,akawa ana shinda bar hakuwa hivyo awali lakini ilitokea hivyo tu.
Baada ya kuona hivi na kukagua kizazi cha upande wa baba hii inawatafuna je inaweza kuwa ni laana au ni jini katumwa?

Nitakupm ili kupata maelezo ya maswali personal zaidi

Mary Chuwa, Zamani wazee wetu walikuwa wakifanya matambiko ya aina mbalimbali kwa mizimu, matambiko hayo shabaha yake ilikuwa ni kuomba ulinzi wa mizimu iwalindie ukoo, ilinde watoto au mizimu isadie mvua zinyeshe kipindi ambacho kiangazi kimepitiliza sana na mvua kuchelewa kunyesha au kama kuna jambo lolote lisilokuwa la kawaida limetokea kwenye ukoo au familia, matambiko haya yalikuwa yanafanywa kuomba msaada wa mizimu, matambiko haya bado yanaendela kufanywa na familia nyingi.

Mizimu ni nini? Watu wengi wanafikiri mizimu ni ndugu wa ukoo waliofariki miaka mingi sana (mababu na mabibi). Mara nyingi utakuta ukoo au familia zina Mzee wa ukoo, ambaye ndiye anayeratibu taratibu zote za kufanya matambiko. Kimsingi hakuna uhusiano wowote ule kati ya mizimu na mwanadamu. Mara nyingi matambiko hufanyika kwa kuchinja wanyama na damu ya mnyama hutumika kuomba dua kwa mizimu iwatendee mambo yote wanayoyataka yafanyike, kisha hufuatiwa na viapo vya ukoo kwa mizimu kuwa watafuata yale yote mizimu itakayo sema wayafanye.

Matambiko kwa lugha nyingine tunaweza kusema ni kamba za kuzimu, zinazowafunga wanadamu wakiwa duniani. Mizimu ikishafunga ukoo kwa kamba shughuli yake huwa ni pevu kijinasua. Mizimu huifanyia familia jambo lolote ovu jinsi wanavyoamua, na jinsi wapendavyo, hizi kamba za kuzimu ni sawasawa kabisa na unavyotumia remote control ya television kubadilisha vipindi mbalimbali bila kuwepo na waya wa moja kwa moja toka kwenye tv hadi kwenye kitufe cha kuongozea tv. ndivyo hivyo hivyo mizimu inavyoyumbisha maisha ya watu wakiwa kuzimu kwa matatizo na magonjwa ya kila aina.

Familia nyingi zimekuwa mateka wa mizimu, kwa makosa yaliyofanywa na wakale wetu, na mizimu kwa kutumia remote control wameendelea kutaabisha familia nyingi, kiasi kwamba utakuta ukoo karibu wote wanaugua aina moja ya ugonjwa unaofanana kama kichaa, sukari, mapigo ya moyo n.k. au utakuta familia inaanza na maisha mazuri yenye wasomi wazuri na vipato vya kuridhisha, lakini mali hutoweka na huishia katika maisha ya mahangaiko na ufukara wa kutupwa. Familia nyingine utakuta wanawake hawaolewi au wakiolewa ndoa haidumu. Familia nyingine kila mwaka na mwezi unaofanana ni lazima afe mwanaukoo. Familia nyingi zimefungwa na kamba za kuzimu bila ya kijijua, anapozaliwa mtoto mizimu muda huo huo kukifunga kichanga hicho kwa kamba shingoni, na hali hiyo huendelea kizazi kimoja hadi kizazi kingine.

Kila mwanadamu mauti inapomfika ni lazima anapokelewa, familia iliyofungwa kwa kamba za kuzimu anapofariki shughuli yake huwa ni kubwa na kifo chake huwa na mahangaiko yasiyokuwa ya kawaida. Roho ya mwanadamu inapoachana na mwili macho ya kimwili hufunga na macho ya rohoni hufunguka, macho ya rohoni yanapofunguka huwaona wenyeji wake waliokuja kumpokea, wale aliokuwa akiwaita mizimu ya babu na bibi, kumbe ni majoka ya kutisha, yanapokuja kumpokea, yanakuja na vicheko na kumdhihaki na huanza kumshika mgeni wao ili waondoke naye. Mtu wa aina hiyo anakuwa anaongea lugha ya mizimu, ambayo wanaomuguza hawaelewi maana yake, lakini huwa anakataa kuondoka nao, akijaribu kuwafukuza. Wanapoanza kumshika ndiyo maana utakuta mtu aliyefungwa kwa kamba za kuzimu anatupatupa miguu na mikono kila upande ili majoka wasimshike.

Mtu asiyefungamana na kuzimu, roho yake inapoachana na mwili, macho yake ya kiroho hufunguka na huwaona wenyeji wake waliokuja kumpokea, wenyeji wake huwa ni watu waliovaa mavazi meupe kabisa na nyuso zao zinang'aa, anapokelewa kwa nyimbo nzuri ajabu, kinachofanyika kwa mtu huyo, mikono yake huilaza juu ya tumbo lake na anakufa akitabasamu akifurahia nyimbo tamu za wenyeji wake.

Mary uwezo wa kukata kamba za kuzimu zilizoifunga familia yenu ya Chuwa upo mikononi mwako, inawezekana kabisa na ni jambo jepesi.
 
Majimoto pia kuna hili suala la mama wajawazito unakuta alikuwa hana shida yeyote ile lakini mwisho wa siku karibu na kujifungua linaibuka tatizo na kuambiwa kuwa wewe ni lazima tukufanyie upasuaji,je nalo hili linasimama upande upi Kiroho,kwani hiyo imekuwa sana kuna hospital moja hapo Arusha imekuwa na Sifa hiyo wengi wanaokwenda hapo ni hilo huwapata.

Dada kabla ya Majimoto kuja na jibu lake, kuna baadhi ya hospitali hasa za binafsi zimegeuza akina mama wanaotaka kujifungua kuwa mtaji kwani wakimfanyia upasuaji analipa pesa zaidi. Dar kuna hospitali moja kubwa iko maeneo ya Mikocheni ina huo mtindo.
 
Majimoto pia kuna hili suala la mama wajawazito unakuta alikuwa hana shida yeyote ile lakini mwisho wa siku karibu na kujifungua linaibuka tatizo na kuambiwa kuwa wewe ni lazima tukufanyie upasuaji,je nalo hili linasimama upande upi Kiroho,kwani hiyo imekuwa sana kuna hospital moja hapo Arusha imekuwa na Sifa hiyo wengi wanaokwenda hapo ni hilo huwapata.

Habari yangu namba #16 ukurasa wa 1, nimeeleza uwepo wa shule za kufundisha wachawi nchini Tanzania, shule moja ipo Tandika Dar es Salaam na shule nyingine ipo barabara ya 10 Tanga.

Katika shule hizi wanafunzi huanza kufundishwa masomo ya kuloga, ambayo hufundishwa na kusoma kwa muda wa miaka mitano. Kipindi hicho mwanafunzi wa uchawi, hujifunza kwa vitendo kabisa, yapo maeneo ambayo kila mchawi mwanafunzi hupenda sana kuyafanyia kazi. Eneo moja ni jinsi ya kutengeneza pepo la kifafa cha mimba, kutengeneza pepo la ukimwi, kutengeneza pepo la kuondoa nguvu za kiume kwa akina baba. Wakitengeneza haya mapepo hutumwa kwa mtu waliyemkusudia kumdhuru. Baadhi ya hospitali huwa zinatumiwa sana na hawa wachawi wanafunzi DSM zipo hospitali mbili moja ipo katikati ya jiji na nyingine ipo pembezoni mwa jiji, ukienda hospitalini hapo kujifungua ni lazima watamgeuza mtoto tumboni asiweze kupita kwenye njia ya uzazi ya kawaida, hadi upasuaji ufanyike.
 
Majimoto nashukuru kwa maelezo yako,naomba ufafanue jinsi ya kuzikata kamba za kuzimu zinazofunga familia.
 
Wanafunzi wa uchawi ni warika gani? Kama ni watoto au vijana shule hizi zetu wanahudhuriaje?
 
Wanafunzi wa uchawi ni warika gani? Kama ni watoto au vijana shule hizi zetu wanahudhuriaje?

Binti Sayuni, uchawi hauna rika, nadhani umewahi kusikia watoto wa shule za msingi wameanguka shuleni na kuzirai, tendo hilo linafanywa na wanafunzi wenzao ambao tayari ni wachawi na wako shule ya msingi wanasoma. Kimsingi watoto na wanawake ndio wanaopendwa sana katika fani ya ulozi, kwani wanakuwa na umakini mkubwa na hawafanyi makosa katika fani ya kuwanga.
 
Mary Chuwa, Zamani wazee wetu walikuwa wakifanya matambiko ya aina mbalimbali kwa mizimu, matambiko hayo shabaha yake ilikuwa ni kuomba ulinzi wa mizimu iwalindie ukoo, ilinde watoto au mizimu isadie mvua zinyeshe kipindi ambacho kiangazi kimepitiliza sana na mvua kuchelewa kunyesha au kama kuna jambo lolote lisilokuwa la kawaida limetokea kwenye ukoo au familia, matambiko haya yalikuwa yanafanywa kuomba msaada wa mizimu, matambiko haya bado yanaendela kufanywa na familia nyingi.

Mizimu ni nini? Watu wengi wanafikiri mizimu ni ndugu wa ukoo waliofariki miaka mingi sana (mababu na mabibi). Mara nyingi utakuta ukoo au familia zina Mzee wa ukoo, ambaye ndiye anayeratibu taratibu zote za kufanya matambiko. Kimsingi hakuna uhusiano wowote ule kati ya mizimu na mwanadamu. Mara nyingi matambiko hufanyika kwa kuchinja wanyama na damu ya mnyama hutumika kuomba dua kwa mizimu iwatendee mambo yote wanayoyataka yafanyike, kisha hufuatiwa na viapo vya ukoo kwa mizimu kuwa watafuata yale yote mizimu itakayo sema wayafanye.

Matambiko kwa lugha nyingine tunaweza kusema ni kamba za kuzimu, zinazowafunga wanadamu wakiwa duniani. Mizimu ikishafunga ukoo kwa kamba shughuli yake huwa ni pevu kijinasua. Mizimu huifanyia familia jambo lolote ovu jinsi wanavyoamua, na jinsi wapendavyo, hizi kamba za kuzimu ni sawasawa kabisa na unavyotumia remote control ya television kubadilisha vipindi mbalimbali bila kuwepo na waya wa moja kwa moja toka kwenye tv hadi kwenye kitufe cha kuongozea tv. ndivyo hivyo hivyo mizimu inavyoyumbisha maisha ya watu wakiwa kuzimu kwa matatizo na magonjwa ya kila aina.

Familia nyingi zimekuwa mateka wa mizimu, kwa makosa yaliyofanywa na wakale wetu, na mizimu kwa kutumia remote control wameendelea kutaabisha familia nyingi, kiasi kwamba utakuta ukoo karibu wote wanaugua aina moja ya ugonjwa unaofanana kama kichaa, sukari, mapigo ya moyo n.k. au utakuta familia inaanza na maisha mazuri yenye wasomi wazuri na vipato vya kuridhisha, lakini mali hutoweka na huishia katika maisha ya mahangaiko na ufukara wa kutupwa. Familia nyingine utakuta wanawake hawaolewi au wakiolewa ndoa haidumu. Familia nyingine kila mwaka na mwezi unaofanana ni lazima afe mwanaukoo. Familia nyingi zimefungwa na kamba za kuzimu bila ya kijijua, anapozaliwa mtoto mizimu muda huo huo kukifunga kichanga hicho kwa kamba shingoni, na hali hiyo huendelea kizazi kimoja hadi kizazi kingine.

Kila mwanadamu mauti inapomfika ni lazima anapokelewa, familia iliyofungwa kwa kamba za kuzimu anapofariki shughuli yake huwa ni kubwa na kifo chake huwa na mahangaiko yasiyokuwa ya kawaida. Roho ya mwanadamu inapoachana na mwili macho ya kimwili hufunga na macho ya rohoni hufunguka, macho ya rohoni yanapofunguka huwaona wenyeji wake waliokuja kumpokea, wale aliokuwa akiwaita mizimu ya babu na bibi, kumbe ni majoka ya kutisha, yanapokuja kumpokea, yanakuja na vicheko na kumdhihaki na huanza kumshika mgeni wao ili waondoke naye. Mtu wa aina hiyo anakuwa anaongea lugha ya mizimu, ambayo wanaomuguza hawaelewi maana yake, lakini huwa anakataa kuondoka nao, akijaribu kuwafukuza. Wanapoanza kumshika ndiyo maana utakuta mtu aliyefungwa kwa kamba za kuzimu anatupatupa miguu na mikono kila upande ili majoka wasimshike.

Mtu asiyefungamana na kuzimu, roho yake inapoachana na mwili, macho yake ya kiroho hufunguka na huwaona wenyeji wake waliokuja kumpokea, wenyeji wake huwa ni watu waliovaa mavazi meupe kabisa na nyuso zao zinang'aa, anapokelewa kwa nyimbo nzuri ajabu, kinachofanyika kwa mtu huyo, mikono yake huilaza juu ya tumbo lake na anakufa akitabasamu akifurahia nyimbo tamu za wenyeji wake.

Mary uwezo wa kukata kamba za kuzimu zilizoifunga familia yenu ya Chuwa upo mikononi mwako, inawezekana kabisa na ni jambo jepesi.

Kwenye red nakuunga mkono. Miaka ya 90 hivi kule kijijini kwetu kulikuwa na mama mmoja ambaye kwake alikuwa hajumuiki na wenzie kanisani kabisa. Akiambiwa kusali haji, hakutaka kubatizwa na wala hakutaka kubatiza watoto wake. Kifupi hakuwa na hofu ya Mungu hata chembe.
Kuna siku aliumwa sana akawa katika hali ya kufa. Alianza kulia na kulalamika sana kuwa anaungua miguu. Alilia na kusema kuwa kuna watu waajabu wanakuja kumchukuwa wamsaidie asiende nao. Pale kulikuwa na mkristo ana maji ya baraka nyumbani kwake. Yalichukuliwa yale maji na akaulizwa kama yupo tayari kubatizwa. (Kanisa Katoliki katika hatari ya kifo mkristo yeyote anaweza kumbatiza mtu aliye katika hatari ya kufa).
Yule mama alibatizwa na mara baada ya ubatizo alitulia akasema asante na baada ya muda kidogo alifariki. Ushuhuda huu ulitolewa makaburini na Katekista juu ya watu waliokuwa hawajali na wanajidai hawana hofu ya Mungu. Baada ya tukio lile watu kijijini walijawa na hofu kuu maana wengi walishuhudia na kanisa lilianza kujaa kuliko ilivokuwa awali.
Mwenye kuamini na aamini.
 
mkuuu mimi nataka niwe mchawi ili badae niweze kuuza huu uchawi kwa wati tofauti tofauti
 
Mary, nimekutumia kwenye PM

Majimoto, awali ya yote, asante kwa elimu uliyoimwaga hapa. Pili, tuko wengi tunaohitaji kuzikata kamba za kuzimu. Tafadhali, kama hutojali, tuwekee hapa mbinu za kuzikata hizo kamba ili nasi tuwekwe huru na yule mwovu. Natanguliza shukrani. Ubarikiwe.
 
Njia pekee hapa duniani ni ku surrender maisha yako kwa Yesu Kristo na kumwambia kwamba umefika end of the road na kwamba unaomba akubebee mizigo yako akuondolee nira wazee wako ambao waliingia maagano pasikujua walijiweka chini ya utawala wa mkuu wa kuzimu. Maana yeye ndiye njia kweli na uzima. Alikuja ili tuwe na uzima tena tuwe nao tele. Haijalishi utaongeanaye kwa luga gani ama order ipi ila tu udhamirie kweli toka moyoni. Nayeye atakuja hapo ulipo atakukumbatia atakupa toba ya kweli baadaye atakujaza nguvu yake (roho mtakatifu) na we utaona ndani mwako umebadilika na kupata ufahamu wa tofauti. Baada ya hapo tafuta watu wenye ujuzi kama Maji moto ama Ame wakueleze cha kufanya zaidi ya hapo. Watakusaidia katika hatua zako za awali kwani kama mtoto mchanga anavyohitaji maziwa baada ya kutoka tumboni mwa mama basi nao watakunyonyesha mpaka ufikie hatua ambapo sasa na wewe unaweza chagua mwenyewe mlo kamili ni upi na kipi ukila unavimbiwa; kipi ukiacha kula unapata utapiamlo. Baadaye wewe mwenyewe utakuwa fundi wa mapishi ya hivyo vyakula kwa watoto wachanga na hata wakubwa wenye mahitaji mbalimbali na pengine ukawa mpishi bora kwenye eneo lingine kama maji moto alivyo kwenye mambo ya biashara ya uchawi.

Wewe utasaidia ukoo wako mzima kutoka tika kongwa hilo la kushikiliwa na mikataba ya kuzimu baada ya kuwa sasa jemedari moja wapo katika jeshi la mbinguni huku ukisaidiana na jeshi zima la watoto wa Mungu kama comander Ame; Field marshal Maji moto na wengine wenye rank mbali mbali kwenye hili jeshi lenye magari ya moto na upepo kuharibu makambi ya wavamizi huko kwenye ulimwengu wa giza ili kuzidi kuwa fungua mateka wetu huko; kuwa ponya waliojeruhiwa na kuwapa raha waliosafishwa kwa damu ya mwanakondoo. Huku mambo yote yanawezekana na mpaka sasa hatujawahi poteza vita na wala hatutegemei kwani vita vilisha piganywa na jemadari wetu huyo Yesu ambaye sasa ametupa tu sisi nafasi ya kuwatemea mate maadui, kuwazomea, kuwa tia vidole machoni, kuwakanyaga vichwa na kuwa fanyia kila aina ya uonevu kabla hawajapelekwa rasmi gerezani. Hii ndiyo raha ya vita vyetu yaani tunapigana na adui asiye na nguvu tena aliyefungwa miguu na mikono na kwa sisi yule anayeweza kuzomea sana anapandishwa cheo; mwenye kujua kuwatemea mate anapewa taji; hata ukiweza tu kuwa nyanyasa kwa kuwaangalia vibaya unapewa cheo cha ukuruta.

Karibu sana kwenye bustani ya raha ambapo hakuna wivu; masimango; uonevu na kila jema ulilowahi kulisikia hapa duniani. Chakula chetu ni uzima hakuna kuugua ugua ovyo; hatuhitaji kufanya ufisadi kupata mahitaji tukiwa na hitaji la kitu chochote tunapiga simu tu namba yetu ni Yeremia 33:3 na tunaletewa yale yote tunayohitaji pamoja na ziada maana wakati mwingine vingine havijawahi kuvumbuliwa hapa duniani so tuna pewa kuonja kama tutapenda na ikionekana tunaburudika basi tunaambiwa tuendelee kwa wakati wetu. Karibu sana na kwa sasa ni mwachie Maji moto field Marshal amalizie.

Unaweza kusikiliza sera zetu hapa maana waha ni campaigners wetu wa ilani ya uchaguzi
http://www.youtube.com/watch?v=vhx0cXcxShU;

http://www.youtube.com/watch?v=95hzAamYXyc&feature=player_embedded
 
Asante sana Commander Ame. Nitashukuru zaidi ikiwa mtanisaidia (wewe na Majimoto) kuniongoza katika hii safari yangu ya kutoka utotoni hadi ukubwani. Tuwasiliane kwa PM. Baraka za Bwana Yesu ziwe nanyi daima.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Asante sana Commander Ame. Nitashukuru zaidi ikiwa mtanisaidia (wewe na Majimoto) kuniongoza katika hii safari yangu ya kutoka utotoni hadi ukubwani. Tuwasiliane kwa PM. Baraka za Bwana Yesu ziwe nanyi daima.

Commander Ame na mwenzake Field marshal Majimoto kila mara unakutana nao barabarani wewe ukikutana na moja wapo wiki hii basi elewa ndiyo mmoja kati ya hao. Uzuri ni kuwa huyu Yesu akija ndani mwako basi atakupa na ufahamu wa sauti ya Ame na mwenzako na hutapotea kwamba ni akina nani. Usifanye mgumu moyo wako mara ukikutana nao please waeleze yote nao watapata utambuzi kuwa ndiyo wewe uliepata divine visitation. Ubarikiwe na bwana na please usifanye kuwa mgumu moyo wako.
 
Back
Top Bottom