Ndevu mbili,
Siyo kweli kabisa kuwa kila mafanikio ya mtu husababishwa na uchawi, mafanikio ya mtu ni bidii yake mwenyewe, jinsi anavyojituma na kumtegemea Mwenyenzi Mungu. Hakuna tatizo lolote kuhusiana na mafanikio ya mtu.
Isipokuwa yapo mafanikio ya watu yenye utata, ambayo yanaambata na nguvu za shetani. Mkoa wa Lindi ambao ndio wa pili wenye wachawi wakubwa nchini, ukienda kwa hawa jamaa wanaojiita wataalamu, ni lazima utembee kwa miguu kwa siku tatu ndipo ufike walipo. Wao wanagawa utajiri, lakini masharti yao ni lazima uwape mke, mtoto au mzazi wako, au utakuta ndani ya familia hiyo kuna mtoto ambaye ni zezeta au taahira, na watoto wa namna hii ukiondoa nguvu ya uchawi uliwekwa ndani yao wanapona na wanakuwa sawasawa kabisa, kama watoto wengine.(Wapo watoto wanazaliwa na utaahira na wapo wanao pewa utaahira wa kupata mali unaosababishwa na wazazi au walezi wao hawa wa kundi la pili ndio ninawazungumzia)
Sasa hivi kidogo wamelegeza masharti, wao watakupa mali nyingi sana kwa mkataba wa miaka mitatu au mitano, muda huo ukifika ni lazima, ni lazima tu utakufa, warithi wa mali zako zenye mikataba ya kifo, nao wakimaliza miaka hiyo nao wanakufa.