[h=3]WACHAWI WAWILI TOKA KIGOMA WAKAMATWA KANISA LA UFUNUO MWANZA.[/h]
Watu wanaosadikiwa kuwa ni wachawi
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wachawi wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani mwanza baada ya kukutwa katika kanisa la Ufunuo lililopo Butimba, jijini Mwanza.
Wananchi na baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi Mwanza wakiwa wamewazingira wachawi hao katika viwanja vya polisi Mwanza leo asubuhi katika kuchukuwa maelezo.
Watu hao ambao wamekutwa kanisani hapo leo majira ya saa 12 asubuhi na Mchungaji wa kanisa hilo Diana Bandele na Abigaili Zumaridi ambaye ni nabii wa kanisa hilo wametambulika kuwa ni wachawi mara baada ya kuhojiwa na kukiri kuwa wamesafiri kwa ungo kutoka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza kuwachukuwa watu walioagizwa kwaajili ya sadaka.
Pembejeo za kichawi mwanamke alisafiri kwa kutumia ungo na mwanaume akatumia mkuki na pembe.
Kwa mujibu wa mahojiano hayo wachawi hao ambao niMwanamke aliyejitambulisha kwa jina la
Masaganya Kalimanzila (30) na mwanaume Chiza Juma wamesema walipewa amri na wakuu wao wanao ishi chini ya maji kuwachukuwa watu watatu wa kanisa hilo kwa mazingira ya kichawi ili wawauwe kwaajili ya kafara na mazindiko.
Mchungaji wa kanisa la Ufunua Diana Bandele (kushoto) na Abigaili Zumaridi ambaye ni nabii wa kanisa
hiloambao waliwakuta wachawi hao kanisani mwao majira ya saa 12 kwani muda huo ni ada kwa wao kujitakasa kwaajili ya kuianza siku ya ibada.
Ingawa jeshi la polisi linaendelea kuchunguza juu ya tukio hilo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania hakuna kipengele kinacho utambua uchawi hivyo hakuna kesi inayowakabili watu hao