LANGO LA KUZIMU LA TABORA
Mji wa Tabora ni moja ya miji ya zamani sana, mji huu ulianzishwa na wafanya biashara wa Kiarabu, na ulikuwa ni kiungo muhimu cha biashara ya watumwa, waliokuwa wanakamatwa kutoka mikoa ya ziwa, Kongo, Burundi na Rwanda, kabila ya kusafirishwa hadi Bagamoyo kisha kuingizwa kwenye majahazi na kusafirishwa hadi soko kuu la watumwa la Zanzibar.
Lango la kuzimu la Tabora liko ndani kabisa ya soko kuu, Mkuu wa lango hili anajulikana kwa jina la Swaheral, akisaidiwa na majini yafuatayo:-
1) Alibadiri ni jini katili sana, likitumwa linaua kifo cha aina yoyote lililotumwa kufanya kwa muda mfupi na kwa usahihi.
2) Anzula ni jini linalowaingia sana vijana wa kike na wa kiume, linawazuia vijana kuoa au kuolewa. Usiku wanaota wanafanya tendo la ndoa na msichana mzuri sana, na huwa wanamaliza hamu wenyewe. Raha anayopata ni zaidi ya anayopata akifanya mapenzi na msichana/mvulana.
3) Maimuna ni jini ambalo huwakamata kina baba wenye ndoa zao, usiku anaota anafanya mapenzi na msichana mzuri sana, kumbe anafanya tendo la ndoa na hili jini, baba anakuwa hana hamu kabisa na mke wake wa ndoa, hali inayosababisha ndoa kuvunjika na kuachana.
4) Makata (Simba au leo) hili jini linawaingia sana wanawake, usiku anaota ndoto anafanya mapenzi na huwa anapata raha kuliko anayoipata akifanya mapenzi na mume wake.
5) Kafurani ni jini linalofanya watu wawe bubu, utakuta mtu alizaliwa mzima kabisa lakini kwenye ujana wake anaanza kupoteza uwezo wa kuongea.
Jini hili pia ndilo linalosababisha watu kupooza, pia linasababisha au linaharibu kabisa nguvu za kiume za akina baba, na kuondoa uwezo wao wa kufanya tendo la ndoa.
6) Kabru jini hili likiingia kwenye ukoo wenu, linaua watu wasiopungua wawili kila mwaka, na vifo vinatokea miezi inayofanana kila mwaka. Kama limeanza kuuwa mwezi wa April basi kila mwaka mwezi huo ukifika ni lazima atakufa mtu.
7) Eziruni hili jini linatumwa kwa njia ya ujumbe. Linaweza kutumwa ndani ya barua na unapoifungua barua jini hili hukuingia na kukumaliza, au hujilaza barabarani eneo unalopita, ukilikanyanga, matatizo yanaanza kwenye mguu na kuenea mwili mzima.
8) Subha hili ni jini la kujiinua na kujiona sana, kuwa hakuna mwingine zaidi yako, pia linafanya mtu anakuwa kichaa au linamfanya mtu ananuka sana, kiasi kuwa unatumia kila aina marashi lakini hayasaidii.
9) Al-Maul hili jini linamfanya mtu anakuwa omba omba sana, kila siku yeye kazi hafanyi ni kuzunguka zunguka kila sehemu akiomba, na kila siku anakuwa ni mtu mwenye matatizo yasiyoisha.
10) Zuhura au Zohar ni jini la fujo, mtu wa namna hiyo ukimkosea yeye anachojua ni kupigana tu kitu kinachoitwa samahani kwake ni mwiko.
11) Araba jini hili linapenda sana harufu ya udi (ubani), unapochomwa ni lazima jini hili lifike eneo la tukio, na linapenda sana kutafuna tafuna vitu, hivyo hutafuna kitu chochote kitakachokuwa nyumbani kwako.