Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa hivi zipo shule kabisa za kufundisha uchawi nchini Tanzania, Shule moja ipo Temeke masomo yake huchukua miaka saba hadi unahitimu.
Ukimaliza Temeke, unaweza kujiunga na elimu ya juu katika fani ya uchawi, chuo kipo Tanga hapo wanatoa digrii ya kwanza ya uchawi kwa miaka mitano.
Wanatoa pia digrii ya pili ya elimu ya ulozi ambapo utakaa darasani kwa miaka mingine mitano.
Master digrii ya ulozi, bado hapa nchini hakuna chuo, inapidi uende Mombasa nchini Kenya ndipo kilipo chuo kikuu cha elimu ya ulozi.
Usafiri wa ungo upo wa aina nyingi, upo usafiri wa ungo unaotumia wanyama, upo usafiri wa kutumia fagio, upo usafiri wa kutumia fimbo, upo usafiri wa kutumia ungo.
Wachawi wote wana roho ya uchawi, roho ya uchawi ni roho inayokufanya uweze kupita eneo ngumu na kutokeza upande wa pili, kwa mfano wachawi wanapowanga usiku roho hizi huwafanya kuingia katika nyumba yoyote na kuwafanyia uchawi usiku watu waliolala ndani ya nyumba hizo bila ya kuonekana. Isipokuwa nyumba za walokole haziingiliki kabisa.
Roho za uchawi zinawawezesha wachawi kujibadilisha maumbo yao, kutoka maumbo ya kibinadamu na kugeuka kuwa paka, panya, kunguru n.k.
Wanapotaka kusafiri anakuwa na vifaa vyake vya kichawi, kisha huomba dua akinuizia majini yampeleke sehemu fulani, roho yake ya uchawi na majini humuinua juu angani kwa kasi hadi eneo alilokusudia. Usafiri wa aina hii ni hatari kwani unaweza kutunguliwa kirahizi ukiwa angani.
Usafiri wa kutumia wanyama kama fisi, hutumika kwa nchi kavu tu, hawawezi kuvuka bahari kwenda visiwani au nchi za mbali.
Usafiri wa kasi sana ni wa kutumia fimbo, kabla ya kuanza safari, unaomba dua ya manuizo na kukanyanga incha moja ya fimbo, roho ya uchawi na majini hukuinua juu angani, kama unataka kwenda Nigeria kutoka Dar, utaonyeshwa njia yote ilivyo, kama kuna hatari yoyote huonekana, na inabidi uhairishe safari, kama njia ni nyeupe, unatakiwa ukanyage incha ya pili ya fimbo, na safari huanza kwa kasi ya sauti. Kwa sababu safari ni ya kasi sana na upepo ni mkali sana, kiasi kuwa huwezi kufika ukiwa hai, majini huchomoa roho yako ndani ya mwili wako na roho kukutangulia mbele, mwili wako huikimbiza roho yako ukiwa katika hali ya umauti, unaweza kutumia sekunde 10 kufika Nigeria, lakini ni usafiri wa hatari kuliko zingine, usafiri huu hujulikana kama usafiri wa kujichinja.
Wachawi wa Marekani na bara Ulaya wao hutumia sana usafiri wa fagio.
Duu wewe utakuwa ndo mchawi kabisa! Utawezaje kuyajua yote haya ikiwa ww sio
Duu wewe utakuwa ndo mchawi kabisa! Utawezaje kuyajua yote haya ikiwa ww sio
kigoma ilikua zamani kuna kijiji nliambiwa kinaitwa Makere-ushingo-wilaya ya Kibondo. .... unanunua radi na majaribio wayafanya hapo hapo....
Kila kitu kina faida na hasara zake. Ila me nahisi biashara ya uchawi ndio ina hasara kubwa kuliko faida, kwa mfano utoaji wa kafala.
Mkuu hiyo namba nne kuna siri gani hapo? Mbona viongozi sijawaona hapo maana nasikia nao ni wateja wakubwa wa uchawi.
Mikoa saba nchini Tanzania ndiyo tishio kwa kuwa na nguvu kubwa za uchawi
1. Tanga ndio kinara
2. Lindi unafuatilia
3. Dar es Salaam
4. Mtwara
5. Tabora
6. Kigoma
7. Mwanza
Mikoa yenye wachawi wengi, kwa maana kwamba karibu kila kaya kuna mchawi
1. Sumbawanga (Rukwa) ndio kinara
2. Ruvuma inafuatialia
3. Mbeya
4. Singida
Mikoa ambayo wananchi wake ndio wateja wakuu wa wachawi
1. Kilimanjaro inaongoza
2. Morogoro inafuatilia
3. Kagera
Wateja wengine wa wachawi
1. Wafanyabiashara
2. Wasanii
3. Kina mama wa nyumbani
4. Wanafunzi wa shule za sekondari hasa wa kidato cha pili.
Mkuu mama porojo umepotea ,njoo utueleze kwanini ajali n nyingi sana kipindi,je? Kuna uhusiano na nguvu za Giza...
Mikoa saba nchini Tanzania ndiyo tishio kwa kuwa na nguvu kubwa za uchawi
1. Tanga ndio kinara
2. Lindi unafuatilia
3. Dar es Salaam
4. Mtwara
5. Tabora
6. Kigoma
7. Mwanza
Mikoa yenye wachawi wengi, kwa maana kwamba karibu kila kaya kuna mchawi
1. Sumbawanga (Rukwa) ndio kinara
2. Ruvuma inafuatialia
3. Mbeya
4. Singida
Mikoa ambayo wananchi wake ndio wateja wakuu wa wachawi
1. Kilimanjaro inaongoza
2. Morogoro inafuatilia
3. Kagera
Wateja wengine wa wachawi
1. Wafanyabiashara
2. Wasanii
3. Kina mama wa nyumbani
4. Wanafunzi wa shule za sekondari hasa wa kidato cha pili.
Sitaki kuamini hii post ina comment zaidi ya 840 wakati haina kitu cha maaana