Biashara ya Uchawi Tanzania

Biashara ya Uchawi Tanzania

Sasa hivi zipo shule kabisa za kufundisha uchawi nchini Tanzania, Shule moja ipo Temeke masomo yake huchukua miaka saba hadi unahitimu.

Ukimaliza Temeke, unaweza kujiunga na elimu ya juu katika fani ya uchawi, chuo kipo Tanga hapo wanatoa digrii ya kwanza ya uchawi kwa miaka mitano.

Wanatoa pia digrii ya pili ya elimu ya ulozi ambapo utakaa darasani kwa miaka mingine mitano.

Master digrii ya ulozi, bado hapa nchini hakuna chuo, inapidi uende Mombasa nchini Kenya ndipo kilipo chuo kikuu cha elimu ya ulozi.

Mmmh hii nayo kali !! We umeyajuaje hayo?? Na akishafuzu mafunzo yote hayo anaajiriwa wapi?
 
Mkoa wa Dar naona nao unakuja kwa kasi kuhusu uchawi,baada ya miaka kama 5 nafikiri utakua unaongoza kwa wachawi na watumiaji wa huo uchawi
 
Usafiri wa ungo upo wa aina nyingi, upo usafiri wa ungo unaotumia wanyama, upo usafiri wa kutumia fagio, upo usafiri wa kutumia fimbo, upo usafiri wa kutumia ungo.

Wachawi wote wana roho ya uchawi, roho ya uchawi ni roho inayokufanya uweze kupita eneo ngumu na kutokeza upande wa pili, kwa mfano wachawi wanapowanga usiku roho hizi huwafanya kuingia katika nyumba yoyote na kuwafanyia uchawi usiku watu waliolala ndani ya nyumba hizo bila ya kuonekana. Isipokuwa nyumba za walokole haziingiliki kabisa.

Roho za uchawi zinawawezesha wachawi kujibadilisha maumbo yao, kutoka maumbo ya kibinadamu na kugeuka kuwa paka, panya, kunguru n.k.

Wanapotaka kusafiri anakuwa na vifaa vyake vya kichawi, kisha huomba dua akinuizia majini yampeleke sehemu fulani, roho yake ya uchawi na majini humuinua juu angani kwa kasi hadi eneo alilokusudia. Usafiri wa aina hii ni hatari kwani unaweza kutunguliwa kirahizi ukiwa angani.

Usafiri wa kutumia wanyama kama fisi, hutumika kwa nchi kavu tu, hawawezi kuvuka bahari kwenda visiwani au nchi za mbali.

Usafiri wa kasi sana ni wa kutumia fimbo, kabla ya kuanza safari, unaomba dua ya manuizo na kukanyanga incha moja ya fimbo, roho ya uchawi na majini hukuinua juu angani, kama unataka kwenda Nigeria kutoka Dar, utaonyeshwa njia yote ilivyo, kama kuna hatari yoyote huonekana, na inabidi uhairishe safari, kama njia ni nyeupe, unatakiwa ukanyage incha ya pili ya fimbo, na safari huanza kwa kasi ya sauti. Kwa sababu safari ni ya kasi sana na upepo ni mkali sana, kiasi kuwa huwezi kufika ukiwa hai, majini huchomoa roho yako ndani ya mwili wako na roho kukutangulia mbele, mwili wako huikimbiza roho yako ukiwa katika hali ya umauti, unaweza kutumia sekunde 10 kufika Nigeria, lakini ni usafiri wa hatari kuliko zingine, usafiri huu hujulikana kama usafiri wa kujichinja.

Wachawi wa Marekani na bara Ulaya wao hutumia sana usafiri wa fagio.

Duu wewe utakuwa ndo mchawi kabisa! Utawezaje kuyajua yote haya ikiwa ww sio
 
sijauona mkoa wa zanzibar. huko ndo hakuna mpinzani. Waulize hata simba na yanga
 
Kila kitu kina faida na hasara zake. Ila me nahisi biashara ya uchawi ndio ina hasara kubwa kuliko faida, kwa mfano utoaji wa kafala.
 
Mkuu mama porojo umepotea ,njoo utueleze kwanini ajali n nyingi sana kipindi,je? Kuna uhusiano na nguvu za Giza...
 
Mkuu hiyo namba nne kuna siri gani hapo? Mbona viongozi sijawaona hapo maana nasikia nao ni wateja wakubwa wa uchawi.

hahaha hapo nazani itakua ile average ya 30 ku pass kwendaaa kidato cha tatu ahaha
 
Mikoa saba nchini Tanzania ndiyo tishio kwa kuwa na nguvu kubwa za uchawi
1. Tanga ndio kinara
2. Lindi unafuatilia
3. Dar es Salaam
4. Mtwara
5. Tabora
6. Kigoma
7. Mwanza

Mikoa yenye wachawi wengi, kwa maana kwamba karibu kila kaya kuna mchawi
1. Sumbawanga (Rukwa) ndio kinara
2. Ruvuma inafuatialia
3. Mbeya
4. Singida

Mikoa ambayo wananchi wake ndio wateja wakuu wa wachawi
1. Kilimanjaro inaongoza
2. Morogoro inafuatilia
3. Kagera

Wateja wengine wa wachawi
1. Wafanyabiashara
2. Wasanii
3. Kina mama wa nyumbani
4. Wanafunzi wa shule za sekondari hasa wa kidato cha pili.

Aisee, poleni sana Watanzania mnao tumia uchawi. Ndio maana Nchi yenu ni MASKINI YA KUTUPWA kwa sababu ya uchawi mnao uedekeza.

Watakabahu
 
Mkuu mama porojo umepotea ,njoo utueleze kwanini ajali n nyingi sana kipindi,je? Kuna uhusiano na nguvu za Giza...

Mahitaji ya DAMU yalikuwa makubwa kuwezesha rasimu ya katiba kupita bila mizengwe.
 
Mikoa saba nchini Tanzania ndiyo tishio kwa kuwa na nguvu kubwa za uchawi
1. Tanga ndio kinara
2. Lindi unafuatilia
3. Dar es Salaam
4. Mtwara
5. Tabora
6. Kigoma
7. Mwanza

Mikoa yenye wachawi wengi, kwa maana kwamba karibu kila kaya kuna mchawi
1. Sumbawanga (Rukwa) ndio kinara
2. Ruvuma inafuatialia
3. Mbeya
4. Singida

Mikoa ambayo wananchi wake ndio wateja wakuu wa wachawi
1. Kilimanjaro inaongoza
2. Morogoro inafuatilia
3. Kagera

Wateja wengine wa wachawi
1. Wafanyabiashara
2. Wasanii
3. Kina mama wa nyumbani
4. Wanafunzi wa shule za sekondari hasa wa kidato cha pili.

hapo kwa kidato cha pili??????????? ckuamini
 
Sitaki kuamini hii post ina comment zaidi ya 840 wakati haina kitu cha maaana
 
Back
Top Bottom