Biashara ya Uchawi Tanzania

Biashara ya Uchawi Tanzania

Mara nyingi ukitembea mitaa ya uswahilini, utakuta wananchi wameanika unga na katikati ya mkeka walioanikia unga wameweka kipande kikubwa cha mkaa.

Misukule chakula chao kikuu ni pumba au unga uliochanganywa na maji, mara chache hulishwa nyama za watu endapo mmoja wao atafariki, nyama yake hukatwakatwa na kulishwa misukule. Kwa kawaida misukule hufungiwa ndani wakati wa mchana, na usiku ndio hufunguliwa kwenda kufanya kazi mashambani, viwandani, ujambazi, ulozi nk. Kuna nyakati wenye misukule hukosa chakula cha kuwalishia misukule, hivyo huachiwa mchana kuingia mitaani kujitafutia chakula. Wanapokuwa mitaani wakikuta unga umeanikwa, wanaushambulia kwa kuchota na kula. Moja ya mafundisho wanayopewa ni kuwa wakiona kitu chochote cheusi, wasikisogelee na kama wanaona kinakuja upande waliopo wanatakiwa waondoke mara moja katika eneo hilo.

Ukiona unga na mikaa imewekwa juu yake mitaani kwako, jua kuwa eneo hilo ni maskani ya wachawi wa nchi, na kama unaishi maisha ya hovyo hovyo, hakika wewe ni msukule mtarajiwa.
 
Mkuu hiyo namba nne kuna siri gani hapo? Mbona viongozi sijawaona hapo maana nasikia nao ni wateja wakubwa wa uchawi.
Hapo umenena hata sheik Yahya alishasema wazi anawapa ulinzi baadhi ya viongozi , hivyo ni wateja wake, pia mtoa mada ajaribu kupata takwimu kwa waganga wa Bagamoyo anaweza kupata conclusion tofauti ya utafiti wake
 
Nimeeleza vizuri sana huko juu kuhusu jinsi ilivyo vigumu kumtambua mchawi, mke/mume anaweza kuwa ni mchawi wa kukata na shoka lakini usijue kabisa, jamii inaishia kuwahukumu watu wengine kwa kuangalia umri wa mtu, mabadiliko ya viungo vya mwili kutokana na uzee, ugonjwa au kutoka na mazingira anayoishi.

Je unawezaje kumtambua mchawi unayeishi naye ndani ya nyumba au mfanyakazi mwenzako?

Uchawi ni swala zima la kiimani.. mimi siamini.. so wala haunishughulishi.. simaini kama mtu anaweza kugeuka paka.. bilogical such a thing ni impossible, siami mtu anaweza akapaa na ungo.. mechanical physics + laws of gravity hazikubali.. in short i believe in riality not the Unseen magic powers
 
Mimi nataka niulize maswali mengi,
sasa kama hujibu,nitauliza vipi?
 
Mkuu maji moto, nina maswali mawili.

1. Kwa mujibu mwa maelezo yako kuna tofauti gani kati ya msukuleni na kuzimu.
2. Je, mtu akichukuliwa msukule, anaweza kurudishwa kwenye ulimwengu unaoonekana? Na kama ndiyo anakuwa kama zamani? Na lile kanisa la Kawe ( zamani ilikuwa Ubungo maji), huduma zake zina association na mambo haya? Na hao wachawi/waganga wa kichawi wanaweza kurudisha maisha ya zamani?
 
nikweli hii ni issue hasa kwa sisi waafrika, Nashangaa watu mnamtegemea maji moto tu, na wengine wengi wataalam wapo tu, mwageni ili tuzidi pata ufahamu wa ulimwengu huu
 
Hapo umenena hata sheik Yahya alishasema wazi anawapa ulinzi baadhi ya viongozi , hivyo ni wateja wake, pia mtoa mada ajaribu kupata takwimu kwa waganga wa Bagamoyo anaweza kupata conclusion tofauti ya utafiti wake

Inaoneka mjm nae ni kiongozi fulani
 
Uchawi ni swala zima la kiimani.. mimi siamini.. so wala haunishughulishi.. simaini kama mtu anaweza kugeuka paka.. bilogical such a thing ni impossible, siami mtu anaweza akapaa na ungo.. mechanical physics + laws of gravity hazikubali.. in short i believe in riality not the Unseen magic powers
Kujifunza na kuelewa kitu haimanishi kwamba umekubaliana nacho. Kuna waislamu wanajifunza biblia na wakristu wanajifunza kurani. Ni kuongeza maarifa na kujua hii dunia. Najua htujui vitu vingi kwenye dunia lakini hivi vichache ni vema tukavijua na kuvielewa. Pia kutona na mfano wako, natural science haiwezi kusupprot imani yoyote. e.g. Katika tunaamini kwa mungu lakini sayansi haakuna mungu.

Jifunze kujifunza kila siku na usishawishiwe na mazingira tu.
 
Uchawi ni swala zima la kiimani.. mimi siamini.. so wala haunishughulishi.. simaini kama mtu anaweza kugeuka paka.. bilogical such a thing ni impossible, siami mtu anaweza akapaa na ungo.. mechanical physics + laws of gravity hazikubali.. in short i believe in riality not the Unseen magic powers

Tehetehetehetehetehe. Kuna mwenzio mmoja alikwenda kijiji kimoja kinaitwa Bulima huko Mwanza ambacho kinajulikana kwa uchawi. Alipofika huko akawa anahutubia mahali anasema "watu wanasema eti kuna uchawi, mimi nasema haupo". Kesho yake alipolala akaamka yuko juu mlimani. Weeeeeee! Ilibidi atoroke haraka sana. Uchawi upo na kiboko yake ni BWANA YESU tu.
 
Mkuu maji moto, nina maswali mawili.

1. Kwa mujibu mwa maelezo yako kuna tofauti gani kati ya msukuleni na kuzimu.
2. Je, mtu akichukuliwa msukule, anaweza kurudishwa kwenye ulimwengu unaoonekana? Na kama ndiyo anakuwa kama zamani? Na lile kanisa la Kawe ( zamani ilikuwa Ubungo maji), huduma zake zina association na mambo haya? Na hao wachawi/waganga wa kichawi wanaweza kurudisha maisha ya zamani?

Watu wanachukuliwa msukule kwa ajili ya shughuli maalum kama vile kilimo, uvuvi, kuvuna misitu, kazi za viwandani, madereva, n.k. misukule ya namna hii huishi katika nyumba hizi hizi tunazoishi aidha wengi wanawekwa darini, ndani ya makabati, kwenye vyungu, mvunguni mwa kitanda au kwenye vijiji vya wachawi.

Kuzimu ni shimo, chini ya ardhi au chini ya bahari, watu waliochukuliwa msukule huwa wanarudishwa katika ulimwengu unaoonekana. Wanaporudishwa wengi wao huwa wamekatwa ulimi, maombi yanayofanyika ulimi huota upya, wanarudishiwa uwezo wao waliokuwa nao kabla na wanakuwa watu wa kawaida kabisa, wapo wengi sasa hivi ni madakitari, waimbaji, waalimu, wanafunzi na wafanyabiashara.

Hakuna mchawi au mganga wa kishenzi anayeweza kurudisha maisha ya zamani kwa msukule, ispokuwa kwa uwezo wa YESU pekee.
 
Mimi nataka niulize maswali mengi,
sasa kama hujibu,nitauliza vipi?

Samahani The Boss nilikuwa kijiji cha wachawi cha Ngende, ndani ya pori kubwa mkoani Lindi nina mengi ya kuwashirikisha, nimepita tu eneo lenye internet, bado niko vijijini.
 
Uchawi ni swala zima la kiimani.. mimi siamini.. so wala haunishughulishi.. simaini kama mtu anaweza kugeuka paka.. bilogical such a thing ni impossible, siami mtu anaweza akapaa na ungo.. mechanical physics + laws of gravity hazikubali.. in short i believe in riality not the Unseen magic powers

Viper, itakushangaza sana baada ya miaka isiyozidi 10 serikali itakuja na sheria ya kutambua uwepo wa wachawi na vitendo vya kichawi wanavyofanya kwani wataanza kuumbuliwa kwa mambo yao ya kificho na kila kitu kitaonekana mchana kweupe tena hadharani.
 
Samahani The Boss nilikuwa kijiji cha wachawi cha Ngende, ndani ya pori kubwa mkoani Lindi nina mengi ya kuwashirikisha, nimepita tu eneo lenye internet, bado niko vijijini.
Lete habari majimoto...
 
ndugu zangu nataka kuwa habarisha ya kuwa uchawi si kwa afrika au bongo tu kama mtoa mada alivyo ainisha utafiti wake lakini nilikuwa na wazo kiduchu tu, ni mwaka jana
au mwaka juzi kulitangazwa nafasi ya mchawi mkuu masikani Uingereza na sifa zake zilitangazwa ili kushindana na wengine kutoka mataifa mbalimbali, na kwa ufupi tu hebu ingia google search ''withch craft'' utapata mambo ambayo yatakupa muono wa ajabu na kweli ya duniani. nikiupata ule mtandao wa Australia unaotoa mafunzo mbalimbali ya uchawi nitawajuza. ahsante naomba kuwasilisha
 
Viper, itakushangaza sana baada ya miaka isiyozidi 10 serikali itakuja na sheria ya kutambua uwepo wa wachawi na vitendo vya kichawi wanavyofanya kwani wataanza kuumbuliwa kwa mambo yao ya kificho na kila kitu kitaonekana mchana kweupe tena hadharani.

Mkuu, niliona AG kapeleka miswada mbalimbali ya mabadiliko ya sheria mbele ya kamati ya bunge. Moja ya miswada hiyo ni ule wa uchawi ambao Tundu Lissu (MB) alitia shaka. Inahusiana na hii posting yako?
Na kama uchawi ni imani na haionekani, wataumbuliwa vipi?
 
Back
Top Bottom