Biashara ya Uokaji (Bakery): Mbinu, Ushauri na Changamoto Zake

Munkari bestito naomba uje hapa utajifunza mengi zaidi kuhusu kutaka kufahamu keki na uokaji wote

 
Last edited by a moderator:
....stand by HD generator, chumba, gharama za TFDA etc .....wawe angalau na 50-80m
 
Kuhusiana na suala la vifaa unaweza kucheki kwenye hii PDF pamoja na vifaa cost zote mpaka za ushauri nasaha wa aina za recipe za mikate-Kuna mikate aina nyingi sana ambayo kwa sasa sokoni mingi haipo ni inovative mojawapo kuingia sokoni kwa kishindo.Tumekuandalia seting ya mini bekary yenye uwezo wa kuzalisha tani moja kwa shifti moja yenye masaa 10 pia unaweza kufanya shifti ya usiku hiyo nii juu yako

Kama kutakuwa na swali au umeshindwa kudownload basi nicheki anthony@ugalla.com
nitakutumia moja kwa moja kwa email yako

Pia niwieni radhi kutokana na vifaa vingi kukosa tasfiri ya kiswahili basi nimeona doc yote iwe ya kizungu
 

Attachments

Wakuu naomba msaada wa kujua vifaa vinavyohitajika ili kuanza hii biashara!! Nataka kuanza katika small scale na kuajiri watu wachache pia kupata vifaa ambavyo siyo complicated, Je mtaji kiasi gani utatosha?
 
Wakuu naomba msaada wa kujua vifaa vinavyohitajika ili kuanza hii biashara!! Nataka kuanza katika small scale na kuajiri watu wachache pia kupata vifaa ambavyo siyo complicated, Je mtaji kiasi gani utatosha?


Mkuu hapo juu niliattach list ya vifaa kwa bekarindogo yenye uwezo wa kuzalisha tani moja kwa shifti moja...kwa kawaida gharama za kuanzisha bekari kamahii ni kama mil 50 to 60 inategemea na eneo husika...kwa kawaidabekari kama hii kwa siku faida yakeni kama milioni moja kwa hivyo ndani ya miezi miwili rahisi kurudisha pesa wakati miezi mingine ni kufikiria upanuzi wa biashara
 
mkuu hongera kwa kuthubutu ,jali ubora wamikate ,muonekano ,ujazo ,na taarehe za kuisha kwa matumizi ,yaani expire date .pia zingatia sana usafi ukijua kuwa unadeal na afya za mtu zaidi ya mmoja kosa moja litakugharimu ,na pia distibution yako pia uwe na network nzuri usiwaze super market baadhi wanatengeneza bidhaa zao wenyewe ,angalia maduka ya kawaida ,n.k
 
Hongera sana mkuu, Mungu akutangulie.

Changamoto kubwa hapo ni umeme na machine maintenance. Na imani umejipanga vyema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…