Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,081
Habari
Hivyo vifaa vinapatikana wapi wajameni?
Hivyo vifaa vinapatikana wapi wajameni?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuhusiana na Mtaji inategemeana unataka kutengeneza bidhaa gani na kwa kiwango gani kwa siku etc. Mfano kwa minimum hata 3 mill unaweza anaza kwa keki ndogo. Kwa kununua mixeer ya kg 5 kwa laki 9, Oven single deki ya 1.5 then laki sita ikawani pans na ingredients.
Vifaa vinavyohitajika kwa mradi wa bakery yaani unatengeneza wa keki, mikate, biscuits etc ni kama ifuatavyo commercial Oven, mixer mashine, slicer, improver, kabati, Pan/ filling, nozzels and mashine, decorations accesories, neckbag na vingine vidogo vidogo.
Maduka ya vifaa nayafahamu baadhi yako ambayo ni ya vifaa bei rahisi na mengine juu kidogo:
1. Maduka ya vifaa expensive ila vifaa vyao vina ubora wa hali ya juu. Duka la kwanza liko mtaa wa samora avenue inatazamana na PPF house, duka la pili liko posta mkabala na wizara ya sayansi na taknolojia na duka la tatu liko tazara veterani pale Penye petrol station. Haya. maduka vifaa vyao vinatoka UK, Turkey na baadhi ya nchi za Ulaya.
2. Vifaa vya at least bei rahisi ni kutoka China maduka ni moja liko Kariakoo mtaa wa agreey ukimaliza Bakhresa mbele kuja jengo lina hospitali. Pili ni maduka mawili yanatazamana na kituo cha mafuta Bigborn.
Nakaribisha uwanja wa maswali kwa jambo lolote kuhusiana na bakery.
Asante mkuu,angalau umetoa njia.
Sie wengine tupo Mbali,je una Idea ya Bei?
Achilia mbali na hivyo vya mchina,nasema vile Genuine.
Tatizo Maduka yetu makubwa hata website hayana,kazi kweli.
Halafu Msaada mwingine.
Kwa Budget ya 15 - 30m,unaweza kuanza na Level ipi ya Bakery,ni Small au Mid
I seee! JF ni kiboko, ukiwa unasoma hivi tu unatoka na miradi elfu kidogo, juzi hapa nimefuatilia mradi Wa maji ya chupa ulikuwa well analysed! Sasa ona huu nao jamaa wanavyochambua! Hongera JF, hongera mwanzilishi Wa hii media!
Habari za mchana ndhani mtakua mnaendelea vyema
Naomba msaada
Ukitaka kuanzisha kiwanda kidogo cha kuoka mikate ni vitu gani hasa ambavyo unatakiwa kuwa navyo na may be kiasi gani cha pesa
KWA VIFAA TU NA MTAJI WA KUANZA
1.GARI YA KUSAMBAZIA IPO
2.SEHEMU YA KUFANYIA KAZI HIYO IPO
So swala hapa ni mashine na vitu gani vya kuanzia
Natanguliza shukrani
ningependa kama ningepata mchanganuo kidogo,faida na hasara
Changamoto ni soko.
Soko ukiwanalo, biashara nzuri sana.
Kila la kheri..!!!
soko lipo lakini muisrael nataka kuanzisha kidogo sana ambacho kwa mara ya kwanza kitakua kinatengeneza mikate kama 500 kwa siku
embu niambie gharama kuhusu tfda sawa ila sasa nataka nianze na kama home scale hivi kuna haja ya kuwaita hao
naomba uniteneneezee gharama ambazo zitahitajika
plzzz nashukuru
Kwa kupika mikate 500 kwa siku, ni lazima uwe na vifaa hivyo hapo juu.
Kwa ukubwa wa huo wa bakery, lazima uwaone TFDA kabla, Lazima..!!
Huwezi kufanyia biahsra hiyo ya bakery ya mikate 500 kwa siku halafu jamaa wasijue.
Maafisa afya wa kata wanahusika hapo pia.
Hao ndio wanaotoa certification ya kwanza kabla ya TFDA.