Biashara ya Uokaji (Bakery): Mbinu, Ushauri na Changamoto Zake

Biashara ya Uokaji (Bakery): Mbinu, Ushauri na Changamoto Zake

Hapa kuna vitu vichache vya kuzingatia ili ujue utatumia vifungashio gani.

Una target wateja wa aina gani na hizo bidhaa bei zako umezipangaje? Nakuuliza hivyo kwa sababu kama unatarget mabosi wao wanaexpect packaging ya kueleweka na mara nyingi hawana tatizo na bei lakini kama una target walalahoi wao wapo very price sensitive hadi haelewi thamani ya packaging. Kama una target walalahoi kuna mifuko ya khaki inauzwa kariakoo inakuwa 50 au 100 not sure, watu wengi wenye bakery wanaitumia.
na target maboss na online customers
 
Unajua dada yangu packaging ni muhimu kinoma coz ni presentation ya product na vile vile husaidia kuuza bidhaa.

Kwa sababu ndio unaanza anza simple na hizo khaki packaging sio mbaya coz bado hauna defined market lakini kama upo vizuri kimtaji kuna packaging nzuri sana za bakery products unaweza kuagiza kutoka South Africa.
na target maboss na online customers
 
Tofauti na khaki, nazani ni mifuko transparent laini kama ile ya mikate. Mcheki bakhressa ana kampuni yake ya packaging inaitwa OPIL ipo pugu rd kama anatengeneza iyo mifuko.
tofaut na kaki hakuna vifungashio vzur zaid kwa Tanzania hii?
 
Vifungashio vinauzwa, ukitaka kuboresha zaidi unatengeneza na label yako unaweka na contact ili vikiwa poa tukupigie ku order tena....
All the best
kuweka label ndo plan yang.Kinachonikwamisha ni pakuvipata hvo vifungashio.Kama unapafaham nielekeze plz
 
Maduka ya wajasiriamali ndo wapi?
Maduka ya wajasiriamali ni maduka yanauzaga mahitaji spesho kwa ajili ya wajasiriamali, ukitaka vifungashio vipo vya kila aina, ukitaka kutengeneza sabuni materials unapata hapo n.k n.k dar kariakoo yapo japo sijawahi kwenda Dodoma yapo barabara ya 8 na 9,na duka la vifungashio tu lipo nyuma ya jengo la ccm
 
Nakushauri uende ofisi ya SIDO iliyo karibu nawe utapewa ushauri mzuri na hata msaada wa kudesign hivyo vifungashio
 
Habari za Asubuhi Ndugu jamaa na marafiki.

Ninaomba ushauri wenu katika hili ninalotaka kulifanya. Nina mtaji wa 10mil hivi, na ndoto zangu ilikuwa kufungua biashara ya bakery ndogo tu. naombeni mawazo yenu kama huu mtaji utatosha.
 
Fungua duka genge mtaani (uswahilini kwa 5m) then from zea bakery itajizaa mumo humo.
 
Nnataka nianze biashara ya kutengeneza vitafunwa vya kuoka lakn sina vifungashio.Msaada wenu na ushaur tafadhal.Mfano wa vitafunwa ni kama hyo pcha chini
d9a0f03ae57846e8fd054a1265ae3257.jpg
Kama umekosa vifungashio hapa nchini, unaweza ukaagiza China tena wanaweza kukutengenezea vikiwa na label yako na kwa gharama nafuu kabisa. Unaweza kunicheki ili nikusaidie namna ya kuagiza hivyo vifungashio.
 
Naomba mwenye uelewa juu ya uokaji wa mikate, cake na bidhaa kama hizo.

Mashine za medium size zinapatikanaje? Faida yake ikoje na vutu kama hivyo

Niko Geita
 
Back
Top Bottom