bajaji ni laana, pikipiki ni laana,
utaishia kujuta.
1. Asilimia kubwa anapata dereva anakusanya 50000/= anakupa 20000/=
2. Ni lazima umuachie makusanyo siku mbili tatu ili aifanyie service ya uhakika, ukiwa mbishi itafanywa tambala bovu. Service mara mbili kw mwez, au moja, mbili ni bora zaid
3. Asilimia 90 Hazirejeshi bei ya manunuzi. Buni bisshars tofaut
Ngoja nikujibu
1. Asilimia kubwa anapata dereva anakusanya 50000/= anakupa 20000/=
Kusema kwamba asilimia kubwa anapata Dereva na kumpangia hesabu anayopata yeye wakati yeye yupo njiani na wewe upo nyumbani.
Sasa we kwa akili yako ya kijani unafikiria kwamba anachokipata yeye na kwa juhudi zake kubwa za kufanyakazi katika mazingira magum ndio mgawe sawa?
We si umesign mkataba? na mikataba yote kwa wazoefu wa Biashara na hesabu za Tajiri zinafahamika.
Hii ni sawa na Daladala,huwezi kusema eti wanachopata wafanyakazi kikubwa kuliko chako,wakati wenzio wote ndio wanavyofanya,mbona siku ya hasara hamsemi mgawe hasara pamoja.
Nakuonea huruma sana kwamba kasi ye maendelea ya dunia ya sasa katika biashara na maisha kwa ujumla imekuacha mbali sana.
2. Ni lazima umuachie makusanyo siku mbili tatu ili aifanyie service ya uhakika, ukiwa mbishi itafanywa tambala bovu. Service mara mbili kw mwez, au moja, mbili ni bora zaidi
Huu ndio ukihiyo mwingine na umbulula,we umeona wapi biashara inafanywa hivi.Hesabu inafahamika kwa wiki na kuna siku inaachwa. Na kwa kukushauri tu ni kwamba Services ya Bajaji ni miongoni mwa Services zinazotumia dakika kadhaa tu kumaliza.
3. Asilimia 90 Hazirejeshi bei ya manunuzi. Buni bisshars tofaut
Hapa ndio nimekuona kwamba umezaliwa kwa bahati mbaya na unaishi kwa makusudi. Bajaji, bodaboda zote zinarejesha pesa yake kwa asilimia 100.
Kuna mdada mmoja anazo Bodaboda 26, na alianza na mbili, na ndio ile miaka ya mwanzo zinaanza.
Lei hii akienda bank kuweka pesa ni heshima.Tena Mdada mdogo tu. Na alipohojiwa kwenye Tv anakuambia changamoto za kawaida sana kama ukijitoa.
Mzalendo. Wewe timiza ndoto zako, nunua mpe Driver upate hesabu yako na ndani ya mwaka pesa imerudi.
Na Bajaji unatumia zaidi ya mwaka mmoja. Kuchoka kwa chombo cha moto ni matunzo yako tu.
Inapotokea kasoro basi irekebishe mapema kabla haijawa kubwa.Muhim ni kutafuta sehem ambayo utamuambia Driver wako atakuwa akipeleka kwa ajili ya Service. Maana hivi ni kama Pikipiki tu,s asa baadhi ya Drivers hujifanya kufanya services kivyao na Oil hizi za mitaani zilizokuwa na kiwango duni sana.
Kila la Kheir and Stay blessed