Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri

Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri

aise nimepata kitu humu, je mnaweza kutapa ufafanuzi juu ya kirikuu? Ni ipi bora kati ya kirikuu na bajaji? na bei ya bajaji kwa sasa ni sh ngapi? min and maximum price
Kwa uzoefu wangu kirikuu nzuri mi carry ya kichwa kikubwa.
Hii iko kama mkate hivi,ina gia 5,na nzuri ni 4 wheel drive.
Hizi maderev wanasema zinanguvu sana hiyvo huweza kubebe mzigo mkubwa kidogo kulingana na nyingine,
Na pia 4wd inasaidi kupita kwenye barabara ngumu kama tope na kichanga.
 
Hello wakuu salaam zenu
kwa wale wazoefu na biashara ya bajaji naombeni mnipe mchanganuo coz kuna pesa kiasi hapa nataka kwekeza katika biashara hio , na pia ni bajaji gani ni imara kati ya boxer, Piaggio, au Atul?
Msaada wenu ni muhimu sana katika hili.

Katika biashara ni hatari sana kuwekeza kwenye mradi mmoja (Concentration Risk) kwani ukipata hasara basi umepoteza kila kitu. Ni muhimu sana kupanga kuyaweka mayai yako kwenye makapu tofauti ili kapu moja likioza kwa sababu yai moja limeoza ndani ya kapu hilo basi makapu mengine yasalimike na hivyo kukuwezesha kuendelea na biashara yako (Diversification).

Ili kufanya diversification yenye tija basi hakikisha miradi unayotaka kuifanya in risk profiles ambazo hazishabihiani kabisa kwa maana kwamba kama vyanzo vya hasara vikitokea kwenye biashara moja basi vyanzo hivyo ni vyanzo vya faida kwenye biashara nyingine.

Kwa mfano kama unataka kufanya biashara ya kuuza mablanketi basi fikiria kufanya na biashara ya kuuza barafu pia kwa sababu kama hakuna baridi basi mablanketi hayatauzika lakini barafu zitauzika kutokana na watu kutumia sana vitu vya baridi wakati wa joto hivyo hasara utakayoipata kwenye uuzaji duni wa mablanketi itafidiwa na faida utakayoipata kwenye uuzaji mwingi wa barafu.
 
Shafi_Abeid,

Ingekuwa hivyo watu wasingenunua. Ni bora hasara niipate pesa ikiwa imepotea mikononi mwangu,kuliko kumpa mwingine kisha nipate hasara zaidi ya ufuatiaji kwenye ufilisi.

Hizi Promo nyingine hembu acheni bidhaa ijipe promo yenyewe. Kama unafanya vizuri watu watakuja tuu, maada nyingine umeleta vituvingine kabisaaa
 
Nauza bajaji yangu, TVS, ina hali nzuri bei 3.5M.
Sababu ya kuuza nataka nibadili biashara kutokana na kukosa muda wa kuisimamia ipasavyo.
Kama unahitaji ni PM tuongee biashara.
 
Mkuu me nafanya hiyo biashara..na mpk sasa ninazo mbili! inalipa sana hapa town ila kwa njia ya mkataba otherwise itakutesa kama huyo mkuu hapo aliyekua anachukua 15 kwa siku!

Ni hiv mkataba huwa ni miez kumi na 8 (mwaka na nusu) na kwa siku kipande ni elfu 20 na anakupa kwa wik = laki na 40/- kwa mwez ( x 4 = 560,000/-) kwa mwaka na nusu itakua 560,000 x 18 = tshs 10080000/-

Kuhusu matengenezo huduma zote za kawaida anafanya dereva icpokua huduma kubwa kubwa tu ndo utahusika tena kwa kushea gharama na dereva!

Kuhusu ipi ni bora' kwa mkataba bora piagio siyo TVS

Kwann piagio? Kwasababu inanafas kubwa ya abiria kukaa na mizigo pia ukilinganisha na TVS
Tvs ni nzuri kwa mtu anaefanya biashara bila mkataba kwasababu ikimrudishia hela ni rahis kuiuza (inauzika kirahis/inasoko kubwa) na hii ni kwasababu ziliwah kuingia hapa bongo kabla ya piagio)

Uimara wa chombo uko mikonon mwa dereva! ila piagio sina shaka nazo kwenye uimara!

Nin faida ya kuingia mkataba?

1/ Bajaj haihitaj uangaliz mkubwa kwasabab dereva anajua baada ya miez kumi na 8 bajaj ni yake! ( hawez kuitumia roughLy)

2/ Ni win-win project yaan wote wanufaika dereva na boss pia hivyo bas haitakua kaz ngumu kumpata dereva

3/ Huduma za mara kwa mara hazitakuepo mana anakua anaiendesha kwa uangalifu mfano, hata *dei waka huwa hawatoi hawa madereva wa mikataba na kama ikitokea service anamaliza mwenyewe unLess iwe kubwa na pia mtashea gharama!

4/ Payback period ni kubwa kwa muda mfupi..

ANGALIZO>> usisahau kukatia BIMA bajaj yako tena BIMA kubwa! ili uondokane na stress inapokua barabarani!
Mkuu hiyo bima kubwa ni shilingi ngapi?
 
C bora uwe na bodaboda 3 za mkataba wa miezi 12 wa elfu 10 kwa siku ambayo itakuletea kiasi kama hicho cha bajaj ambayo inachukua miez 18!!?
 
- itaharibika mara ngapi mwaka mzima?
- haitafanya kazi mara ngapi kwa sababu ya dereva mgonjwa au safari binafsi(lets say matatizo)
-utatumia wewe kwa matumizi yako binafsi mara ngapi.?
-itakamatwa na polisi mara ngapi(kutoa rushwa)
- etc..
Baada ya mwaka unasema unamwachia,bajaji umenunua mil 5 mwisho wa mwaka umepata mil 10 na bajaji umemwachia mtu huoni faida inakuwa ni chini ya mil 5 mwaka mzima? Na umempa mtu mil 5 hivi hivi? Halafu utanunua mpya au??????
Only risk takers can survive and succeed in any business.
Acha kukatisha watu tamaa hapa.
 
Dahh biashara bomba sana kama utaendesha mwenyewe but kama ya kumkabidhi mtuu dahh majanga sana. Mi nilikiwa na yangu kipande 15 kwa siku, but dereva alikiwa anaingiza total 55000 kwa siku akitoa wese 12000, ya bosi 15 kinachobaki chake but ikizingua chochote ni lako wewe mwenyebajaji. Yako ikiwa mbovu anachakupoteza anapiga dayworker, nilikuwa na komaa mwenyewe ahhh mbona safi tuu
Umesahau kuwa siku nyingine naye hapati kitu na ww unamkomalia hesabu yako bila huruma. Usiangalie upande mmoja wa shilingi mkuu.
 
Fanya hivi ingia na mtu mkataba wa mwaka mmoja. baada ya mwaka unamwachia. Terms ni kwamba kila siku lazima alete pesa endapo ikifika week hajaleta mnamnyang'anya. Matengenezo yoyote juu yake. Kila siku anakuletea 30k. 30,000*30*12=10,800,000
Huu ndio ushauri mzuri, ukitegemea kumuweka mtu akuletee tu ni kazi bure, mi hii kitu ilishaniliza, niliweka mtu ikawa ni usumbufu tu mwishowe nikauza, kama vipi unaweza endesha mwenyewe for supernormal profit.
 
Mkuu hamna biashara inayokosa changamoto so ni kumpa moyo na kumpa ushauri mzuri mkuu...karibu Sana Event 9 limited tukusaidie kuhusu biashara hii
Hiyo business kichefuchefu hata ukimpata kijana mstaarabu, labda tu uendeshe mwenyewe ndipo utaona faida, ni upuuzi kusubiri faida ya 2mln kwa mwaka mzima.
 
Habarini za muda huu,

Nikiwa kama kijana mtafutaji najiandaa na maisha yangu baada ya kumaliza chuo mwezi wa saba mwaka huu(2017) nimejibana hatimaye nimefanikiwa kua na mtaji wangu wa pesa taslimu 3.2Mil, natarajia kua hadi siku nitakapomaliza chuo nitakua na 4Mil cash.

Nimepanga nitakapomaliza chuo mwezi wa saba ninunue bajaji tvs-king kwa mtu(used) kisha niendeshe mwenyewe ili nijitafutie ridhiki yangu ya kila siku(maisha baada ya chuo) hapa jijini DSM.

Lengo la kuleta hoja hii ni kufahamishwa mambo yafuatayo kuhusiana na biashara hii ya bajaji.

1. Kununua bajaji kwa mtu hakutokatisha ndoto zangu? kama ni vibaya kwa biashara niachanenayo maana sina uwezo wa kununua mpya dukani

2. Changamoto za hii biashara ni zipi? (sitomkabidhi mtu bajaji, nitaendesha mwenyewe)
 
Umeona mbali sana maana ajira zinaonekana kwa Tochi. Hii biashara ni nzuri mkuu. Kikubwa wewe mwenyewe umejipangaje. Kama umeweza kujichanga 4m kupitia Boom lako Naamini hata hii utaweza kujichanga na kufanya makubwa.
 
Kiukweli mi nimmiliki wa bajaji changamoto kubwa huwa ni madereva kama utaendesha mwenyewe basi zingatia tu matunzo, pia unaponunua kwa mtu si ajabu ukahitaji matengenezo makubwa mwanzoni. Kila la kheri kijana.
 
Back
Top Bottom