Biashara ya uwakala wa simu na benki (M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, fahari huduma na NMB Wakala) unaweza kuanza kwa mtaji wa shilingi ngapi?

Habari
Nataka kuanzisha biashara hii ya uwakala wa mitandao na bank:Mtaji 2.2 m
Naomba kuuliza biashara hii inalipa au hasara tupu?

Inalipa ila inategemea na location.
Ushauri.
1. Tafuta eneo/location yenye pilikapilika (watu wengi)
2. Anza na mitandao ya Simu (Tigo, Voda, Halotel na Airtel)
3. Pata semina ya UTAPELI (kutoka kwa hao watakao kupatia TILL za uwakala)
4. Hiyo frame uweke na vitu nyengine vya kuzalisha pesa. Weka hata pombe zile Take Away au kengine cha kutoka fasta.

Mengine tutajuzana kwenye comment...

#YNWA
 
Nilikuwa natamani biashara hii ya huduma za kifedha Ila upande wa  risk hapana kwakweli unaweza  kufa etiii 😥😥😥 wezi wakaniua na Ela yangu wakachukua 😭.
 
kwani wanaofanya biashara nyingine hawapigwi risasi?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha uwoga kijana 1.5ml kwa mwez sio ndogo na kumbuka ndan ya ofis waeza fanya na ishu nyingine tatizo la vijana wa leo mnataka mafanikio ya haraka hakuna iyo
 
Hii biashara naifanya tokea 2012 mpka sasa na nimeifanya kwa mafanikio vigezo kwangu naona

Eneo
Customer care nzur
Mtaji
Umakini
Uhakika wa huduma
Na huduma ya haraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…