Biashara ya viazi mviringo

Biashara ya viazi mviringo

jafarikyaka

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2014
Posts
378
Reaction score
269
Nataka safirisha viazi kutoka Mbeya to Tanga vipi kwa wanaoifahamu inalipa na gunia moja kwa Tanga huwa ni shilingi ngapi?

==========
1592126264391.png

Viazi mviringo (Solanum tuberosum) hupendelea maeneo yenye baridi kuanzia 7v°C hadi 26°C kwa siku 75 hadi 135 za ukuaji wake au zaidi, Hali ya joto hupunguza kiasi cha uzalishaji. Zao hili hupendelea udongo tifutifu usiotwamisha maji na wenye rutuba na wenye maozea "Matama huruku" (Organic matter) yenye pH ya 5.0 hadi 5.5.

Hivyo basi kutokana na hali hii ya hewa viazi hulimwa kwa wingi mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa kwa nchini Tanzania kutokana na kuwepo kwa hali ya baridi katika mikoa hiyo.

Hivyo wafanya biashara wengi wa viazi mviringo hufuata viazi kutoka katika mikoa hiyo na kuvipeleka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Bei za viazi hutegemea na msimu wa mazao kama viazi ni vingi au vichache ndio hutoa bei ya siko la viazi mviringo sokoni .

Michango ya wadau:

Mimi nimefanya hii biashara, naijua vizur sana ni biashara nzuri sana, nilisimama kwa muda kutokana na kubanwa na masomo nategemea kurudi kwenye hii biashara mwezi wa kumi mwaka huu, kwa laki 8 kweli ni ndogo mkuu atleast uwe na kama 3milion ndoo utaona faida ya hii biashara.

Kwani gari ya chini huwa n fuso yenye uwezo wa kubeba magunia 75 kujaza mzigo siyo pungufu ya 2.4m ni bora ufanye ivo kuchukua gari yako kuliko kushare maana itakugharimu sana kwenye usafirishaji.

Nakaribisha tuungane mkuu kama kuna swali waitaji kujua waweza kuuliza apa apa ntakujibi.
----
Soko lipo vizuri, kama unavyoona watu kila siku wanazidi kupenda chips na matumizi ya viazi yanaongezeka cha muhimu ni uchaguzi mzuri wa viazi kule shambani, hakikisha unachagua kiazi kizuri na kiwe kikubwa soko zuri ni Buguruni na Mabibo Ilala siyo wazuri sana.

Kuhusu usafiri kama unachukua mzigo Njombe kulee kuna shida kidogo ya usafiri lakini tofauti na Mbeya usafiri hausumbui sana maana semi tyler nyinyi zinatoka zambia kuja Dar zingine zinakuwa tupu soo deal kaa izo hawawezi kuacha.
 
Why Tanga na sio Dar au Mkoa mwingine ?

Sina uhakika kama ni sahihi lakini gazeti la guardian huwa lina bei elekezi za mazao masokoni..., ila kwa ushauri ili usisikie la kuambiwa tu na usije ukaleta mzigo siku bei imeshuka nenda mwenyewe ufanye tathmini kwa muda wa kama wiki ili ujue bei zinavyopanda na kushuka.

Na uongee na wauzaji kama wanaweza kupokea mzigo (ila usiwaamini sana hawa wanaweza wakasema ulete mzigo siku ukileta wanaanza kuleta habari ya kwamba siku mbaya na bei ya mizigo imeshuka)
 
Nataka safirisha viazi kutoka mbeya to tanga vipi kwa wanaoifahamu inalipa na gunia moja kwa tanga huwa ni shillingi ngapi??

Kwa Tanga mkuu sikushauri hasa ukizingatia viazi vnavyopatikana kwa wingi sasa ni kutoka Mbeya,viazi ambavyo havivumilii shida atleast ingekuwa vya Njombe, pia Tanga sasa wanapata toka Rombo,kwa ushauri zaidi nipm nina uzoef wa miak 4 na ishu hizo. NB:una moyo wa kufanya biashara za kuoza.
 
Wakuu itifaka imezingatiwa.

Nina mawazo ya kuanza biashara ya kununua viazi mviringo (viazi vya chipsi) kutoka Njombe na kuvileta Dar es Salaam. Mtaji wangu sio mkubwa kivile ni shilingi laki 8. Kwa mtu mwenye uzoefu biashara hii naomba ushauri tafadhali nini nifanye ili nifanikiwe.

Na je mtaji huo utatosha japo kwa kuanzia?

NAWASILISHA
 
Nenda pale Soko la Ndizi ufanye physical observation. Ni biashara nzuri sana though nafkiri kwa hiyo laki 8 inaweza kuwa ndogo. Na fursa za mkopo hakuna.

Dawa ni kuichagua Ukawa ifikapo oktoba ili vijana tupate fursa bora zaidi ya kujiajiri na kuajiriwa kama anavyoahidi Lowassa.
 
Asante bro kwa ushauri, ngoja nijitahidi kujikusanya si unajua mitaji yetu hii.

kuhusu ukawa hilo halina mjadala tayar nina kichinjio jimbo la kubenea.
 
Mimi nimefanya hii biashara, naijua vizur sana ni biashara nzuri sana, nilisimama kwa muda kutokana na kubanwa na masomo nategemea kurudi kwenye hii biashara mwezi wa kumi mwaka huu, kwa laki 8 kweli ni ndogo mkuu atleast uwe na kama 3milion ndoo utaona faida ya hii biashara.

Kwani gari ya chini huwa n fuso yenye uwezo wa kubeba magunia 75 kujaza mzigo siyo pungufu ya 2.4m ni bora ufanye ivo kuchukua gari yako kuliko kushare maana itakugharimu sana kwenye usafirishaji.

Nakaribisha tuungane mkuu kama kuna swali waitaji kujua waweza kuuliza apa apa ntakujibi.
 
Mimi nimefanya hii biashara, naijua vizur sana ni biashara nzuri sana, nilisimama kwa muda kutokana na kubanwa na masomo nategemea kurudi kwenye hii biashara mwezi wa kumi mwaka huu, kwa laki 8 kweli ni ndogo mkuu atleast uwe na kama 3milion ndoo utaona faida ya hii biashara

Kwani gari ya chini huwa n fuso yenye uwezo wa kubeba magunia 75 kujaza mzigo siyo pungufu ya 2.4m ni bora ufanye ivo kuchukua gari yako kuliko kushare maana itakugharimu sana kwenye usafirishaji

Nakaribisha tuungane mkuu kama kuna swali waitaji kujua waweza kuuliza apa apa ntakujibi

Bro! Naweza kuonana nawe ili tuongee zaidi! Pls ni PM. Nimekuwa natafuta data za hii biashara na nijue mahala pa kuanzia!
 
Mimi nimefanya hii biashara, naijua vizur sana ni biashara nzuri sana, nilisimama kwa muda kutokana na kubanwa na masomo nategemea kurudi kwenye hii biashara mwezi wa kumi mwaka huu, kwa laki 8 kweli ni ndogo mkuu atleast uwe na kama 3milion ndoo utaona faida ya hii biashara

Kwani gari ya chini huwa n fuso yenye uwezo wa kubeba magunia 75 kujaza mzigo siyo pungufu ya 2.4m ni bora ufanye ivo kuchukua gari yako kuliko kushare maana itakugharimu sana kwenye usafirishaji

Nakaribisha tuungane mkuu kama kuna swali waitaji kujua waweza kuuliza apa apa ntakujibi

Asante sana mkuu, vp chanel ya soko kwa hapa dar inakuaje maana si unajua viazi ni vitu vya kuharibika. Na je, kuhusu usafiri kwa kuanzia nikiwa nadandia 'semi trailers' vp inaweza kunisaidia japo kwa kipindi ambacho cjaweza kusimama mwenyewe.
 
Soko lipo vizuri, kama unavyoona watu kila siku wanazidi kupenda chips na matumizi ya viazi yanaongezeka cha muhimu ni uchaguzi mzuri wa viazi kule shambani, hakikisha unachagua kiazi kizuri na kiwe kikubwa soko zuri ni Buguruni na Mabibo Ilala siyo wazuri sana.

Kuhusu usafiri kama unachukua mzigo Njombe kulee kuna shida kidogo ya usafiri lakini tofauti na Mbeya usafiri hausumbui sana maana semi tyler nyinyi zinatoka zambia kuja Dar zingine zinakuwa tupu soo deal kaa izo hawawezi kuacha.
 
Kwa wanaohitaji mashine za kumenyea viazi inapatikana sasa jijini Dar kwa bei nafuu ya milioni 5.5 mashine uwezo wake ni kilo 300 kwa lisaa, usichelew zipo chache saana, na hazili nyama, zinatoa ganda tuu. Wapige kwa mhusika 075282714
 
Hello
Naomba niasaidie yafuatayo;
Unasema kujaza fuso mil 2.4,,hii ni pamoja na usafiri?
Unashushia wapi?kwa dalali au?
Huko njombe unanunua kwa wakulima ?
 
Hapana mkuu usafiri hujaweka apo mara nyingi huwa wanaitaji advance siyo zaidi ya lak 3 kwenye usafiri, izoo gharama zingine za usafiri unalipa baada yaa mauzo kufanya ata dalali analipwa baada yaa mzigo kuuzwa.

Bei huwa zina range kati yaa 26,000-32,000 kutegemeana na wapi na aina ya kiazi iyo bei ni guniaa ad liko ndani yaa gari, au kwa maana nyingine umelipa wapakiaji,ushuru, na gunia na kambaa.
 
Back
Top Bottom