jafarikyaka
JF-Expert Member
- Nov 13, 2014
- 378
- 269
Nataka safirisha viazi kutoka Mbeya to Tanga vipi kwa wanaoifahamu inalipa na gunia moja kwa Tanga huwa ni shilingi ngapi?
==========
Viazi mviringo (Solanum tuberosum) hupendelea maeneo yenye baridi kuanzia 7v°C hadi 26°C kwa siku 75 hadi 135 za ukuaji wake au zaidi, Hali ya joto hupunguza kiasi cha uzalishaji. Zao hili hupendelea udongo tifutifu usiotwamisha maji na wenye rutuba na wenye maozea "Matama huruku" (Organic matter) yenye pH ya 5.0 hadi 5.5.
Hivyo basi kutokana na hali hii ya hewa viazi hulimwa kwa wingi mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa kwa nchini Tanzania kutokana na kuwepo kwa hali ya baridi katika mikoa hiyo.
Hivyo wafanya biashara wengi wa viazi mviringo hufuata viazi kutoka katika mikoa hiyo na kuvipeleka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Bei za viazi hutegemea na msimu wa mazao kama viazi ni vingi au vichache ndio hutoa bei ya siko la viazi mviringo sokoni .
Michango ya wadau:

----Mimi nimefanya hii biashara, naijua vizur sana ni biashara nzuri sana, nilisimama kwa muda kutokana na kubanwa na masomo nategemea kurudi kwenye hii biashara mwezi wa kumi mwaka huu, kwa laki 8 kweli ni ndogo mkuu atleast uwe na kama 3milion ndoo utaona faida ya hii biashara.
Kwani gari ya chini huwa n fuso yenye uwezo wa kubeba magunia 75 kujaza mzigo siyo pungufu ya 2.4m ni bora ufanye ivo kuchukua gari yako kuliko kushare maana itakugharimu sana kwenye usafirishaji.
Nakaribisha tuungane mkuu kama kuna swali waitaji kujua waweza kuuliza apa apa ntakujibi.
Soko lipo vizuri, kama unavyoona watu kila siku wanazidi kupenda chips na matumizi ya viazi yanaongezeka cha muhimu ni uchaguzi mzuri wa viazi kule shambani, hakikisha unachagua kiazi kizuri na kiwe kikubwa soko zuri ni Buguruni na Mabibo Ilala siyo wazuri sana.
Kuhusu usafiri kama unachukua mzigo Njombe kulee kuna shida kidogo ya usafiri lakini tofauti na Mbeya usafiri hausumbui sana maana semi tyler nyinyi zinatoka zambia kuja Dar zingine zinakuwa tupu soo deal kaa izo hawawezi kuacha.