Biashara ya viazi mviringo

Jf sikuhizi imekua kama uwanja wa wivu wa kimaendeleo.
 
Mkuu huku Tarime labda uchukue ndizi ndo nyingi shambani mkungu Buku tatu mpaka tano

Viazi vipi lakini sio vingi sana ila bei yake cjajua ni ngapi kwa Gunia
 
Vile viazi havitoki Tarime, ni vya Kenya, sasa ukitaka ufanikiwe kwenye biashara hii fanya utafiti kwanza huko Mwanza bei viazi ipoje, wateja wakubwa lenga wauza chips ndio uende kule sirari upande wa Kenya kuchukua mzigo.
 
Mkuu je ulifanikiwa kulifanyia kazi hili wazo lako ?
 
Viazi safi kwa chakula kutoka Tukuyu vinauzwa, pia tunasafirisha Tanzania nzima.
Bei ya kiazi bila usafiri ni elfu arobaini kwa kipeto, safari inaanzia Mbeya wewe utalipia usafiri kutoka Mbeya jijini.
Bei ya usafirishaji inaanzia elfu 10 kipeto kwa safari za dar es Salaam.
Bei 40000 bila usafiri.
Karibuni PM na 0756254925
 
Hizo bei za wapi? Na ni aina gani ya viazi, kwani bei za viazi zilizopo sokoni kwa sasa dar ni kuanzia 37,000-40,000 kwa bei ya jumla!!! Hapo mtu ameshavinunua, na kuvisafirisha hadi dar na ndio anauza kwa bei hiyo, sass hiyo bei yako hata siielewi, au ni aina gani labda ya viazi tofauti na tigoni, obama?
 
Hiyo bei ya Mwezi wa 8 mpaka 9 mwanzoni, sasa hivi Obama haipo ndomana tumepandisha bei. Mwaka jana bei ilikua sh ngapi muda huu? Tunauza Obama ya stock.
 
Hiyo bei ya Mwezi wa 8 mpaka 9 mwanzoni, sasa hivi Obama haipo ndomana tumepandisha bei. Mwaka jana bei ilikua sh ngapi muda huu? Tunauza Obama ya stock.
Kwa mwaka jana kipindi kama hiki viazi kwa dar bei ilikuwa 58,000 ikaja kupanda hadi 70,000!!hiyo bei ninayokuambia hadi leo hii kwa soko la mbagala ndio iliyopo mkuu, obama ni 40,000-42000, kwa sasa bei hiyo kwa dar haipo, Juzi kuna jamaa aliweka uzi humu yupo huko mbeya obama anauza 20,000 akatoa mchanganuo hadi kufika dar ni kama 33,000!!huyo yupo sawa mtu akiuza 40,000 anapata. Ndio maana hiyo bei yako imenishutua au unaposema kipeto una manisha nini?? Nijuavyo mimi kipeto ni kile kigunia kimoja kama kinavyoonekana kwenye gari hapo!! Au una manisha vikiwa viwili ndio bei hiyo?!!
 

Ungemuuliza anauza kiazi gani, kipeto hicho hicho kimoja! Obama haipo mkuu, nilionayo mimi ni hazina ilikua inasubiria soko. Sasa hivi kiding'a inaisha isha na tigo nayo inaelekea kuisha so obama ina bei, kuna jamaa hapa bila 42 hauzi Obama nae ana hazina.
 
Dar kipeto moja usafiri ni 10000 tu
 
nimetoka kununua hapo soko la mabibo muda huu..Obama kipeto moja ni elfu 9 tu mkuu.
 
Dar kipeto moja usafiri ni 10000 tu
Huyo amechangana hiyo ni bei ya ndoo!! Mimi ninapokuambia hadi leo soko la viazi(obama) hapo mbagala hadi 40,000(kipeto)wanauza,tigoni ni 37,000!!!!any hapo sijui inakuwaje na kwa sasa viazi sokoni ni vingi, KILA RAHELI MKUU KWENYE BIASHARA YAKO.
 
Huyo amechangana hiyo ni bei ya ndoo!! Mimi ninapokuambia hadi leo soko la viazi(obama) hapo mbagala hadi 40,000(kipeto)wanauza,tigoni ni 37,000!!!!any hapo sijui inakuwaje na kwa sasa viazi sokoni ni vingi, KILA RAHELI MKUU KWENYE BIASHARA YAKO.
Shukrani, karibu nawewe ulime nna plot nauza ya vipeto 12 guaranteed au zaidi kutokana na wingi wa mbolea mil 2 na laki 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…