Biashara ya viazi mviringo

Habari waungwana!

Leo nipo Jukwaani kuomba msaada toka kwa watu wenye uzoefu na taarifa sahihi kwa biashara ya viazi mviringo.

1. Mkoa upi utatoa viazi bora na kwa bei nafuu miongoni mwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini!?

2. Bei ya Jumla imekaaje!?

3. Gharama za usafiri toka huko vinapopatikana hadi Dar zikoje!?

4. Gharama za ushuru (kama zipo) nazo zipoje!?

Natamani nianze kwa kuchukua viroba 10, Je, ujazo wake unakuwaje!??

Ahsante!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uiwa na milion tatu unaweza coz mm ni kulima wa viaz
 
Njo njome uku viaz ving
 
Salam wakuu,
Nahitaji kujua msimu wa viazi hua ni mwezi wa ngapi hasa?

Msaada kwa wazoefu
 
Nashukuru mkuu... Vipi kuhusu ambavyo sio vya umwagiliziaji?
mkoa wa mbeya viazi huanza kulimwa kati ya mwezi wa 3 hadi wa 5, mavuno huwa ni kuanzia mwezi wa 7 hadi wa 10. Tofauti hapo ni aina ya kiazi na mvua, mvua ikiwa nyingi mwezi wa 3, hua wanachelewa kupanda, mvua inaozesha viazi.
 
mkoa wa mbeya viazi huanza kulimwa kati ya mwezi wa 3 hadi wa 5, mavuno huwa ni kuanzia mwezi wa 7 hadi wa 10. Tofauti hapo ni aina ya kiazi na mvua, mvua ikiwa nyingi mwezi wa 3, hua wanachelewa kupanda, mvua inaozesha viazi.
Shukrani makadirio ya juu kwa kulima ekari moja inaweza kuwa kiasi gani?
 
milioni mbili
Duh milion mbili?
Kwa mchanganuo gani huo chief..ifuatayo ni rafu yngu kwa uzoefu wangu mdogo naomba nisahihishwe nitakapokuwa nimekosea..
:-Kukodi shamba heka moja 100,000- 120,000
:-kulima 60,000
:- mbegu viroba vitano kimoja 50,000 =25000
:-Mbolea yakupandia DAP mfuko wa kilo 25 =35000 + keni mfuko wakilo 25= 22,000 jumla mbolea yakupandua inagharimu 57000
:-Wapandaji 40,000
:- MASTA KINGA kilo moja 18,000
:-mbolea yamaji 10,000
:-sumu 10,000
-palizi nakupandishia udongo :40,000
-: HESABU KUU INANIPA 600,000
 
shamba ni laki 3 mpaka 5 kwa mashamba mazuri ya Ndaga na Ntokela,
mbolea umesahau na NPK, na siyo kg 25, kwa heka moja unahitaji mifuko 4-5 ya kg 50, ambapo mfuko mmoja DAP ni kati ya elfu 52 hadi 56, CAN elfu 40 hadi 44 na NPK ni elfu 64 hadi 67 bei ni kutokana na brand. Mbegu nazo nzuri hua za kutoka ukingani ambapo gunia mpaka lifike shambani hua kati ya elfu 70 mpaka 90. Na kwa eka moja kama utapanda kwa mistari ya kukwarua itakuchukua gunia mpaka 10. Hili ni jibu la gharama za juu kabisa kwa eka moja, ukitaka hesabu za chini nazo zipo, kuna maeneo kama isyonje na mwakaleli gharama za upandaji ni ndogo lakini na bei ya uuzaji nayo ni ndogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…