Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

Biashara ya cement hususan kama utakuwa unauza kwa bei ya rejareja inatoka zaidi ikiwa inauzwa na vifaa vingine vya ujenzi. Hii ni sababu wateja wengi wa ujenzi huka tayari una duka la hardware, hata kama halina vifaa vingi, unaweza kuanza na hata mifuko 100-200. Ila kwa kiasi hiki kidogo cha cement, hutaweza kununua moja kwa moja kiwandani na kunufaika na bei ya kiwandani ambayo kwa sasa kwa mfano Dangote ni sh 9500/mfuko wa grade 32.5 na 10000/mfuko wa grade 42.5. Kiasi cha chini unachoweza kuagiza kiwandani ni tani 30 (mifuko 600) ambayo ni kati ya sh mil 5.7 - mil 6 kutegemea na grade. Kwa Dangote haultalipia usafiri na utaletewa hadi mlangoni. Kwa baadhi ya makampuni inabidi ujitegemee gharama za usafirishaji kutoka kiwandani hadi kwako.

Kwa mtaji wako wa mil 3, itabidi ununue kwa watu wa kati ambao wananunua kiwandani ambao wao huongeza faida ya kati ya sh 500-1000/mfuko. Kama utanunua zaidi ya mifuko 50, wauzaji wengi watakuuzia kwa bei ya jumla (10,000 au 10,500) kulingana na grade. Cha muhimu ni kuzungumza nao vizuri, maana mwingine anaweza hata kukuuzia chini ya hapo kama utachukua mzigo mkubwa kwa mara moja.

Ikija swala la faida, faida kwa mfuko wa cement ni ndogo sana (sh 500-1000) kulingana na soko na ushindani ni mkubwa. Ukinunua huo mfuko wa sh 10,000, ili kushindana na soko hutaweza kuuza zaidi ya sh 11,000 kutegemeana na eneo ulipo. Kama wauzaji ni wengi zaidi basi tegemea kuuza chini ya hapo. Biashara ya cement ni biashara ambayo inategemea "volume sale" ili uweze kuona faida ndio maana wafanyabiashara wengine wanaoagiza kutoka kiwandani wako tayari hata kupata faida ya sh 300/mfuko ili kuvuta wateja na kuhakikisha mzigo wa mifuko 600 au zaidi unaisha siku moja.
Kwa uzoefu wangu, biashara ya cement inahitaji mtaji mkubwa ili kuona faida nzuri. Fikiria mzigo wa tani 30 ambao ni sh mil 6 utazalisha faida ya laki 3 (sh 500/mfuko), ambayo si ndogo sana kama utaweza kuuza angalau tani 30/wiki lakini kama huo mzigo utakaa zaidi ya wiki 4 dukani (na hii inatokea kwa hali ya soko hivi sasa), utaona ni faida ndogo sana kwa uwekezaji huo. Maana kumbuka hapo kuna gharama za ushushaji wa cement ambayo kawaida ni sh 100/mfuko na kama umemweka mtu akusaidie naye inabidi umlipe. Kwa watu wenye mitaji mikubwa kidogo wanaongeza mzunguko wao cement kwa kuagiza mzigo mkubwa zaidi na kuisambaza kwa wafanyabiashara wadogo kwa faida si zaidi ya sh 500/mfuko. Lengo kuu ni kuhakikisha mzigo haukai dukani na unauzika kwa haraka .
Kwa uzoefu wangu changamoto kubwa kwenye cement ni kwamba wakati mwingine uzalishaji unakuwa si wa kuaminika, na hii ni kwa viwanda vyote (mara chokaa imeisha, makaa yameisha au malori ya kusafirishia hayatoshi n.k). Unaweza ukawa umelipia mzigo, halafu zikapita zaidi ya wiki mbili unazungushwa kupata mzigo. Sasa hii inaumiza especially kwa wenye mitaji midogo, maana hela umeshatoa kwenye mzunguko na wakati mwingine unakuwa umeshamwahidi mteja kwamba cement yake atapata kesho na hela yake ushachukua...

Pia kama unauza aina moja tu ya cement hio pia itakuwa changamoto, maana kuna wateja kwa mfano hawatumii brand yoyote zaidi ya twiga, kwa hio ni muhimu kuwa na angalau aina mbili au zaidi ya brand. Sasa kama mtaji mdogo itakuwa changamoto kuweza kuwa na brand tofauti za cement kwa wakati mmoja.

Changamoto nyingine hivi sasa ni soko. Kwa kweli soko limeshuka sana, lakini nafikiri hio si kwa cement tu, bali hata kwa bidhaa nyingine.
Ushauri wangu kwako: 1.Kama una duka la hardware na unataka kuongeza cement, basi anza na mifuko 100-200. Ingawa faida si kubwa, lakini uwepo wa cement kwenye duka la hardware inasaidia sana vitu vingine kuuzika kwa vile mteja wa cement mara nyingi atataka vitu vingine vya ziada zaidi ya cement.
2. Kama huna duka la hardware na unataka kufanya biashara ya cement peke yake nakushauri uongeze mtaji ili uweze kuagizia kiwandani. Hii itakusaidia kwenye ushindani wa bei ambayo itakuwezesha kuvuta wateja. Kumbuka wenye maduka ya hardware wana bidhaa nyingi ambazo humvuta mteja, lakini kwa upande wako itakubidi bei yako iwe ndo kigezo kikuu cha kumfanya mteja aje kwako kununua cement tu kwako, halafu atoke aende duka jingine kununua mahitaji mengine ya ujenzi badala ya kufanya manunuzi yote kwenye duka moja.
3. Kama ushindani si mkubwa eneo lako, unaweza ukaanza na mifuko 200-300 kwa biashara ya cement pekee, lengo lako la awali likiwa ni kutengeneza soko na kujifunza biashara huku ukikuza mtaji ili kuweza kuagiza kutoka kiwandani.

Hakika umebarikiwa hongera na asante maana hata mimi nimejifunza kitu.
 
Ubarikiwe sana nimejifunza kitu hapa yaani umelelezea kwa ufasaha sana
 
Biashara ya cement hususan kama utakuwa unauza kwa bei ya rejareja inatoka zaidi ikiwa inauzwa na vifaa vingine vya ujenzi. Hii ni sababu wateja wengi wa ujenzi huka tayari una duka la hardware, hata kama halina vifaa vingi, unaweza kuanza na hata mifuko 100-200.

Ila kwa kiasi hiki kidogo cha cement, hutaweza kununua moja kwa moja kiwandani na kunufaika na bei ya kiwandani ambayo kwa sasa kwa mfano Dangote ni sh 9500/mfuko wa grade 32.5 na 10000/mfuko wa grade 42.5. Kiasi cha chini unachoweza kuagiza kiwandani ni tani 30 (mifuko 600) ambayo ni kati ya sh mil 5.7 - mil 6 kutegemea na grade. Kwa Dangote haultalipia usafiri na utaletewa hadi mlangoni. Kwa baadhi ya makampuni inabidi ujitegemee gharama za usafirishaji kutoka kiwandani hadi kwako.

Kwa mtaji wako wa mil 3, itabidi ununue kwa watu wa kati ambao wananunua kiwandani ambao wao huongeza faida ya kati ya sh 500-1000/mfuko. Kama utanunua zaidi ya mifuko 50, wauzaji wengi watakuuzia kwa bei ya jumla (10,000 au 10,500) kulingana na grade. Cha muhimu ni kuzungumza nao vizuri, maana mwingine anaweza hata kukuuzia chini ya hapo kama utachukua mzigo mkubwa kwa mara moja.

Ikija swala la faida, faida kwa mfuko wa cement ni ndogo sana (sh 500-1000) kulingana na soko na ushindani ni mkubwa. Ukinunua huo mfuko wa sh 10,000, ili kushindana na soko hutaweza kuuza zaidi ya sh 11,000 kutegemeana na eneo ulipo. Kama wauzaji ni wengi zaidi basi tegemea kuuza chini ya hapo. Biashara ya cement ni biashara ambayo inategemea "volume sale" ili uweze kuona faida ndio maana wafanyabiashara wengine wanaoagiza kutoka kiwandani wako tayari hata kupata faida ya sh 300/mfuko ili kuvuta wateja na kuhakikisha mzigo wa mifuko 600 au zaidi unaisha siku moja.

Kwa uzoefu wangu, biashara ya cement inahitaji mtaji mkubwa ili kuona faida nzuri. Fikiria mzigo wa tani 30 ambao ni sh mil 6 utazalisha faida ya laki 3 (sh 500/mfuko), ambayo si ndogo sana kama utaweza kuuza angalau tani 30/wiki lakini kama huo mzigo utakaa zaidi ya wiki 4 dukani (na hii inatokea kwa hali ya soko hivi sasa), utaona ni faida ndogo sana kwa uwekezaji huo. Maana kumbuka hapo kuna gharama za ushushaji wa cement ambayo kawaida ni sh 100/mfuko na kama umemweka mtu akusaidie naye inabidi umlipe. Kwa watu wenye mitaji mikubwa kidogo wanaongeza mzunguko wao cement kwa kuagiza mzigo mkubwa zaidi na kuisambaza kwa wafanyabiashara wadogo kwa faida si zaidi ya sh 500/mfuko. Lengo kuu ni kuhakikisha mzigo haukai dukani na unauzika kwa haraka.

Kwa uzoefu wangu changamoto kubwa kwenye cement ni kwamba wakati mwingine uzalishaji unakuwa si wa kuaminika, na hii ni kwa viwanda vyote (mara chokaa imeisha, makaa yameisha au malori ya kusafirishia hayatoshi n.k). Unaweza ukawa umelipia mzigo, halafu zikapita zaidi ya wiki mbili unazungushwa kupata mzigo. Sasa hii inaumiza especially kwa wenye mitaji midogo, maana hela umeshatoa kwenye mzunguko na wakati mwingine unakuwa umeshamwahidi mteja kwamba cement yake atapata kesho na hela yake ushachukua...

Pia kama unauza aina moja tu ya cement hio pia itakuwa changamoto, maana kuna wateja kwa mfano hawatumii brand yoyote zaidi ya twiga, kwa hio ni muhimu kuwa na angalau aina mbili au zaidi ya brand. Sasa kama mtaji mdogo itakuwa changamoto kuweza kuwa na brand tofauti za cement kwa wakati mmoja.

Changamoto nyingine hivi sasa ni soko. Kwa kweli soko limeshuka sana, lakini nafikiri hio si kwa cement tu, bali hata kwa bidhaa nyingine.

Ushauri wangu kwako:
1. Kama una duka la hardware na unataka kuongeza cement, basi anza na mifuko 100-200. Ingawa faida si kubwa, lakini uwepo wa cement kwenye duka la hardware inasaidia sana vitu vingine kuuzika kwa vile mteja wa cement mara nyingi atataka vitu vingine vya ziada zaidi ya cement.

2. Kama huna duka la hardware na unataka kufanya biashara ya cement peke yake nakushauri uongeze mtaji ili uweze kuagizia kiwandani. Hii itakusaidia kwenye ushindani wa bei ambayo itakuwezesha kuvuta wateja. Kumbuka wenye maduka ya hardware wana bidhaa nyingi ambazo humvuta mteja, lakini kwa upande wako itakubidi bei yako iwe ndo kigezo kikuu cha kumfanya mteja aje kwako kununua cement tu kwako, halafu atoke aende duka jingine kununua mahitaji mengine ya ujenzi badala ya kufanya manunuzi yote kwenye duka moja.

3. Kama ushindani si mkubwa eneo lako, unaweza ukaanza na mifuko 200-300 kwa biashara ya cement pekee, lengo lako la awali likiwa ni kutengeneza soko na kujifunza biashara huku ukikuza mtaji ili kuweza kuagiza kutoka kiwandani.
Nami pia umenielewesha sana mkuu. Ubarikiwe kwa hilo
 
Ntakupa maelezo mazuri sana kama ukiwa serious yatakusaidia. Mimi naishi dubai huu ni mwaka wa 6 sasa, siku moja nikiwa likizo Tz niliona maduka mengi yakiwa na cement toka arabuni na pakistan..wale watu wanapata faida kubwa sana..mfuko mmoja wa kiwango cha juu kuununua na kuutuma mpaka port dar itakugharimu kama tsh 3500,sasa tatizo ni kwenye kuutoa..kipindi kile ufisadi bandarini ulikuwa mkubwa wakanisumbua sana japo nilikuwa na mifuko 100 tu kwa ajiri ya kibanda changu.

Pia tbs watachukua mfuko mmoja ili kupima ubora na gharama ilikuwa tsh 20000 ilikuwa mwaka jana sijuhi kwa sasa..homework unayotakiwa kuifanya ni kutafuta agent mzuri mwenye ofisi na umwulize process ya utoaji ilivyo, navyojua chaji za tra si kubwa sana ila bandarini walinisumbua...nina akika kuna faida kubwa sana kama ukijua utoaji bandarini ulivyo...na utapata faida kubwa zaidi kama utanunua mzigo mkubwa...nakutakia kila la kheri gharama za ujenzi kwa wenzetu huku ni ndogo sana ila wana tatizo la plots za kujengea...sisi tatizo ni gharama za vifaa vya ujenzi wakati maeneo tunayo.

Karibu sana najisikia vizuri nionapo mtu anatafuta maisha
Maisha kwl ni kutafuta but changamoto ni kubwa ebu nipe fursa mkuu hata moja huko mambeleeee
 
Ntakupa maelezo mazuri sana kama ukiwa serious yatakusaidia.

Mimi naishi dubai huu ni mwaka wa 6 sasa, siku moja nikiwa likizo Tz niliona maduka mengi yakiwa na cement toka arabuni na pakistan. Wale watu wanapata faida kubwa sana. Mfuko mmoja wa kiwango cha juu kuununua na kuutuma mpaka port Dar itakugharimu kama Tsh 3500, sasa tatizo ni kwenye kuutoa.

Kipindi kile ufisadi bandarini ulikuwa mkubwa wakanisumbua sana japo nilikuwa na mifuko 100 tu kwa ajiri ya kibanda changu. Pia TBS watachukua mfuko mmoja ili kupima ubora na gharama ilikuwa TSH 20,000. Ilikuwa mwaka jana, sijuhi kwa sasa. Homework unayotakiwa kuifanya ni kutafuta agent mzuri mwenye ofisi na umwulize process ya utoaji ilivyo.

Navyojua chaji za TRA si kubwa sana ila bandarini walinisumbua. Nina hakika kuna faida kubwa sana kama ukijua utoaji bandarini ulivyo na utapata faida kubwa zaidi kama utanunua mzigo mkubwa.

Nakutakia kila la kheri gharama za ujenzi kwa wenzetu huku ni ndogo sana ila wana tatizo la plots za kujengea. Sisi tatizo ni gharama za vifaa vya ujenzi wakati maeneo tunayo.

Karibu sana najisikia vizuri nionapo mtu anatafuta maisha.

Hujasema bei ya mfuko ni bei gani dh ngapi huko dubai na koteina ya ft ngapu inaingia mifuko mia container kutuma bei gani
 
Wakuu, naombeni mawazo yenu
Nataka kuwa Wakala wa kuuza Cement, ila sijaamua nijiunga na Kampuni gani hasa, naombeni kujua kampuni ipi ni nzuri, criteria za kuwa Wakala, na taarifa nyingine zozote zitakazonisaidia, natanguliza shukrani saaana. ni Wakala wa kuuza Cement.
Asanteni
Nenda Lake cement wazalishaji wa Nyati cement na hutojutia uamuzi wako mkuu,,ofisi zao ziko jengo la atcl town
 
Hivi biashara hii huwa ikoje?

Faida zikoje?

Changamoto zikoje?

Kwa sasa mfuko wa cement ni sh. 19000 huku kigoma na chokaa 4500. Nataka nifungue duka huku kigoma mjini
 
Hii biashara ni mhimu mno. Maana kila siku watu wanajenga hasa hii mikoa inayoendelea kujengwa ili ikue
 
Mkuu uhakikishe uwe na mtaji wa kutosha. Me nipo Kasulu nilikuwa nataka nifungue duka la vifaa vya ujenzi hilo ndo wazo langu
 
Back
Top Bottom