Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

We unadhani kwa nini ikipelekwa nje iuzwe bei ndogo? Kwa taarifa nilizonazo hadi mwaka jana uzalishaji ni mkubwa kuliko mahitaji ya ndani na consumption growth rate ni moderate kuliko uwezo wa viwanda
 

Mkuu acha ubishi, navifahamu hivi viwanda vizuri sana.
Uwezo wa kiwanda unakuwa Determined na uwezo wa kiln kwa maana ya clinker inavyozalishwa, Cement mill mwisho wa siku ndio inaleta Cement, Hivyo viwanda nilivyokutajia hapo juu hasa hivi viwili vikubwa Dangote na Simba (Tanga) kila kitu kikiwa vizuri na cement mill zote zipo ok na kiln ziko ok na soko liko vizuri uzalishaji wa Dangote huwa ni 6000tone/day na Simba ni 4000tone/day.. Ila kukiwa na ups and downs huwa average per day ni 5000tone/day Dangote na 3000-3500tone/day Simba.

Hizo Tonnage ni Designed Capacity kwa maana ndio uwezo wa hizo plants, na kama kila kitu kipo ok tani hizo hupatikana bila shida. Breakdowns, maintenance, shutdowns, Hali ya soko ni vitu vya kawaida kwenye uzalishaji na huleta shida wakati fulani kiasi cha efficiency na production kupungua, Ila sio chanzo cha kusema eti haviwezi kuzalisha hizo tonnage. SI KWELI.
 
Hao Mbeya cement wanaongeza mtambo mwingine na rais alikuwa kuzindua majuzi Wana target kutoka tani 600,000 hadi tani 1,100,000 kwa mwaka by next year na wao wanalenga soko hilo la nje coz la ndani liko saturated
 
Hao Mbeya cement wanaongeza mtambo mwingine na rais alikuwa kuzindua majuzi Wana target kutoka tani 600,000 hadi tani 1,100,000 kwa mwaka by next year na wao wanalenga soko hilo la nje coz la ndani liko saturated
Hao mbeya cement ndio wauzaji wa hizo tani 2000 zilizo wekwa kwenye taarifa

Na huo mtambo mpya unashida kuliko wa zaman
 
Kuvifahamu hakuondoi kusema ukweli kwanini watanzania tunapenda kuambiwa uongo zaidi

Mimi pia nimefanya kwenye hivi viwanda zaidi ya miaka nane nina uzoefu na ninacho kwambia

Baada ya kuacha kazi za viwandani nikahamia kazi ya udereva kusambaza hiyo mizigo mpaka naacha kazi ya udereva nimepita viwanda vyote vikongwe isipo kuwa dangote tu
 
Mkuu unajitahidi kunyumbulisha hoja mpaka hapo nimekuelewa
 
Mbugoti na Timu asanteni kwa elimu nzuri. Naomba kujua Wakala (middle man) wa Simenti aliyepo maeneo ya King'azi/mbezi ya kimara ili kupata simenti kwa bei nafuu kwa ajili ya ujenzi siyo kuuza.
 
Ndugu, habari zenu

Nina kiasi cha mil 10 hivi kwa sasa nategemea kuanzisha biashara ya kuagiza cement kutoka kiwandani na kuiuza rejareja ila kwa mtaji wangu huo nahisi utatosha kwa kuanzisha duka la uuzaji cement tu.

Sasa naomba mwenye mtazamo mpana kuhusu biashara hii aweze kunishauri kwa mapana.
 
Kwa huu mdororo wa uchumi bora ufanye biashara za vyakula au duka la dawa bro.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama yupo interested na hiyo biashara anaweza kuchukua nafaka mikoani akaweka stoo kuanzia mwezi wa 9 huko anaweza kupata faida nusu ya mtaji wake.

Kwa hali ya sasa biashara anayowaza huwenda isiwe na faida pia kwa sababu ya upya wa biashara pale anapoenda kuisimika. Yaani ataanza kazi ya kutengeneza jina la biashara yake kisha atengeneze wateja ni tofauti na vyakula huuzika kwa haraka ukiotea sehemu nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…