Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

kumbe ile sera ya Slaa mfuko wa cement kuuzwa sh elf 5 haikuwa porojo
 
I see. Kwa hiyo tusema Kwa Kuanzia basi hata $5000 unaweza ukaaanza Biashara Sioooo!?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 

Unajua mnabishana kitu kidogo sana,kama mnataka kuanza kuexport vitu njee lazima muwe na siasa safi na muongozo bora,serikali lazima ijenge mazingira yaliyo bora kwa ajili ya mwekezaji wa ndani na sio kwa mwekezaji wa nje tu,kuwawezesha watu kwa mbinu mbalimbali mfano.mabenki yatoe mikopo kwa riba nafuu,watu wapewe elimu ya ujasiriamal, serikali ipunguze kodi au iondoe kabisa kodi kwa wanaoanzisha viwanda vya ndani pia iondoe kabisa urasimu,walimu walipwe mishahara mizuri ili kupunguza mambumbumbu nchini,ufisadi rushwa imalizwe manake ufisadi ndio unasababisha bei ya bidhaa za hapa ndani kuwa kubwa mfano.bei ya kuweka umeme ilikua juu kwa sababu ya huo ufisadi na bei ya umeme pia,bei ya ruti za ndege za humu ndani zilikua juu kwa ajili ya ufisadi mpaka fast jet ikaja ikawaumbua,miundo mbinu mingi ya maji yamearibiwa kwa ajili ya maslai binafsi na mambo mengine mengi...
 
Tunashukuru kwa kutoa idea yako
very interesting
 

Ila kama unajenga nyumba sio ya biashara..hizi nyumba kwa mfano za vyoo vinne tu....kwenda dubai unakuwa unasave lakini sio kivile sna..labda uwe na mwenzako...mka share container moja mkaweka vitu vyote..kwani bandarini container liwe full or half utalipa full.

Ukiangalia na time consumed ya wewe kwenda kule etc....though utapata vitu unique bado naamini inalipa sana hii kwa watu wenye mashule...Hotel kwa wao wanahitaji vitu vingi kwa wakati mmoja.
 

Hata nyumba ya kawaida inafaa sana, coz unanunua kila kitu, vifaa vya umeme vyote (kuanzia wiring mpaka vifaa venyewe) mambo ya jikoni, toilets, ukija tiles, milango,madirisha,rangi za aina zote,mapazia,vitanda,meza za jikoni sebuleni mpaka dining! masofa TV,Fredge na vitu vingine!

Kwa kifupi vitu vya 15M hapa bongo utapata kwa 40 mpaka 60M,

Kwa hiyo nyumba inakuwa na finishing ya ukweli. yaani utadhani ya bakhresa flani hivi
 

Mkuu hivyo vitu vyote unaweza kupata kwa 15 - 20 M? Mbona kama ni kidogo sana?
 
Mkuu hivyo vitu vyote unaweza kupata kwa 15 - 20 M? Mbona kama ni kidogo sana?

Mkuu malngo mmoja, wa chuma toka china ni 300,000 - 400,000/= let say una milango 6, dirisha moja kwa laki 2 mpaka 3 let say una madirisha 10, tiles za chumba kimoja kwa laki 5, let say una vyumba 6. hujaingia chooni, rangi na uje kwenye vitanda (0.5M @),makochi (2M),fridge (1.5M) TV (1.5M) kwenye umeme na maji bado!

Kwa kifupi finishing ya kawaida ni arround 20M, inaweza ikazidi kutokana na mahitaji ya mtu binafsi! sasa chukua hiyo 20M dumbukia zako china uende ukalete first class product uone nyumba yako itakuwaje!

Wenye hela anachukua na fundi kabia, anaenda shoping akirudi baada ya 1month anahamia kwake!
 

Ukiwa umefanya na roofing tayari it's reasonable nilifikiri hapo na roofing juu nilitaka kushangao hiyo ni reasonable kabisa
 
nikupe mfano tu,angalia bei ya cement ya pakstn na tz,ya pakstan ukiweka transptn cost,ushuru na kla kitu bado ni chee kulko ya tz,sasa unataka mwananchi ajiumize kwa kununua ya bei ghali wakati vya chee vipo tena kwa quality ile ile,kanunue vitabu vya international economics urudi class kidogo,ulikuwa unameza
 
GOD bless u mkuu kwa taarifa nzuri..umetufungua macho..ngoja nikichange niagize japo kontena moja nikikichanga nikiwa na 25ml si najaza kontena ya 20ft?
 

Siku tutakapo thamini shillingi yetu na kuiona ina maana kuliko dola ambayo siyo yetu hapo tutaweza kufikilia kuexport. Mjapani yuko na Yeni yake na wala hatumii dola hata siku moja. Sisi hata serikalini tunalipia bill kwa dola
 
kwa hiyo unapendenkeza na sisi tu-export cement yetu ya twiga na tembo ambazo hapahapa bongo tu tunauziwa kwa tsh.14000 na wakati hiyo inayozalishwa huko dubai ni 4000 ikishafika hapa bongo? unadhani watanunua cement yetu kwa bei hiyo? nyie kubalini tu kuwa ile sera ya Dr. Slaa ambay wengi waliibeza ya mfuko wa cement kwa sh 5000 inawezekana! tutaqnza ku-export baada ya manyang'au ya ccm kukaa benchi, azawaizi tutabakia kuwa dumping bin tu!
 
Ni kweli mkuu umenena vyema.Lakini sisi tutajaribu vipi hadi tufikie hatua walizofikia wenzetu?Kwani tunasheria zinatulazimisha turuke stage walizopitia wengine bali zinatutaka tufanye kila kitu kwa std ya Marekani ingawa wao pia hadi kufika walipo walianza kwa vitu vyenye viwango duni!Mie kwa ujuzi niliopata chuo nina uwezo wa kutengeza product nzuri kabisa kwa maana ya ubora kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika mazingira yangu lakini mamlaka inayohusika imeweka vikwazo lukuki nami nimeamua kuwa mchuuzi tu!Naumia sana ila ni kilio cha samaki!


Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Naomba kujua taratibu za visa n.k kwa mimi nisiye na kibali hata kimoja cha kutoka Tanzania zipoje. Mungu akisaidia nianze biashara haraka niwezavyo. Hii fursa ipo karibu kama pua na mdomo. Msaada wako ni muhimu sana!!!
 
vp kuhusu hi cement ya simba au twiga? Price zake zikoje kuanzia ununuzi hadi usafirishaji kuja dar. Nataka real facts kwa anaejua jaman!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…