Sidhani kama Mtaji wa milioni moja utatosha,labda nikuulize hapo ume include kodi ya pango,kumlipa muuzaji etc.Nikupe mfano tairi ya pikipiki size ya san lg kubwa moja ni 50000 jiulize na spea zingine itakua bei gani?
Kaa chini survey uone vifaa gani vinahitajika sana kwa watumiaji ambapo unaenda kufungua duka,andika list yake na bei za manunuzi.
tazama faida ya kila kifaa angalia makadirio ya mauzo ghafi na baadae faida halisi utakayopata ukikamilisha hayo angalia kamtaji kako kama kanatosha.Ili uweze kufanikiwa ni lazima ujenge network na bodaboda owners ili waje kwako na ikiwezekana walete wenzao..
Unaweza kuwa unawapa motisha wakileta wateja hata kuwapunguzia kidogo bei ilimradi isiathiri profit margin yako!
Wengine ongezeeni.