Biashara yangu imedorora sana, hali hii ni kwangu tu au wote?

Biashara yangu imedorora sana, hali hii ni kwangu tu au wote?

Sasa hivi watu watanunua nyumba na viwaja kwa bei nafuu mabenk mengi wadaiwa wao hawajarejesha mikopo waliyokopa na waliweka vitu hivyo dhamana hivyo sio biashara tu kila sehemu sasa hivi deal zimepungua watu wanaishi kwa mshahara
 
Habari za jioni wana JF? Mimi ni mfanyabiashara, ndogo ndogo aina ya bidhaa ninazo uza ni bedshit, taulo, mapazia, n.k cha kushangaza nilikua nafanya biashara vizuri na kuniingizia kipato kiasi lakini toka ameingia rais mpya hasa wiki hizi mbili biashara imekua ngumu kupita kiasi, mauzo yale ya laki mbili kwa siku yameshuka hadi elfu arobaini, mpaka najiuliza ni mimi tu nliyoanza kuishi kwa shida namna hii au na nyinyi wenzangu?
Hiyo ni kote mkuu! Mambo yanabana kote kote! HAPA KAZI KWELI KWELI
 
Sasa hivi watu watanunua nyumba na viwaja kwa bei nafuu mabenk mengi wadaiwa wao hawajarejesha mikopo waliyokopa na waliweka vitu hivyo dhamana hivyo sio biashara tu kila sehemu sasa hivi deal zimepungua watu wanaishi kwa mshahara
Na hali itazidi kuwa mbaya sana hasa kwa sisi watanzania wa hali ya chini! Sema sio mbaya tuzidi kumuomba Mungu atutie nguvu
 
Na hali itazidi kuwa mbaya sana hasa kwa sisi watanzania wa hali ya chini! Sema sio mbaya tuzidi kumuomba Mungu atutie nguvu
Kikubwa kujituma na kuacha starehe ambazo hazina faida kitu ambacho nimejifunza kwa wenzentu waliondelea wanajirusha saana hawa hawa watu waliofanikiwa ila kila mtoko kwake unakuwa na faida ya kwenda kukutana na mtu ambae watafanya biashara sio kama sie
 
Huu ni mda wa tumbuatumbua pesa haukuna .mda sio mrefu baadhi ya mabenk yatafungasha virago
 
Kikubwa kujituma na kuacha starehe ambazo hazina faida kitu ambacho nimejifunza kwa wenzentu waliondelea wanajirusha saana hawa hawa watu waliofanikiwa ila kila mtoko kwake unakuwa na faida ya kwenda kukutana na mtu ambae watafanya biashara sio kama sie
Kweli kaka Starehe zitatuzamisha zikiendekezwa
 
serio hapo unesea usingefunga, tuendelee kuishi kwa matumain ndugu huenda biashara ikabadilika tu.
Mkuu goods haziendi.. Nimeona nifunge nikomae na kutoa services.. Hizo naweza kufanya "home based business" na expiry date ya bidhaa naiepuka
 
Mkuu cha kwanza hakikisha biashara yako ipo "formalized" sajili katika mamlaka husika kama BRELA na Manispaa/Halmashauri upate leseni ya biashara. Pia hakikisha una TIN ili uwe unalipa kodi, lipa kodi zote kwa wakati.

Baada ya hapo lijue soko lako linahitaji nini... jua wateja wako wanauhitaji wa vitu gani halafu uwape kwa bei nzuri sio bei za kuwanyonya.

Kingine hakikisha bidhaa zako zina ubora mzuri na wekeza katika matangazo inavyostahili.

Kwa ufupi ni hivyo tu mkuu.
NADHANI HUJAELEWA HOJA,NI HIVI MFANO MM NIMEFUATA YOTE ULIO SHAURI ILA MWEZ ULIOPTA NIMEFUNGA HESABU YA SHILING LAKI MBILI WAHATI NILIKUWA NAKUSANYA M2.5 HADI 3M
 
Inategemea na aina ya biashara, kuyumba kwa biashara ni kawaida
 
Bidhaa mnazouza ni Made in PRC People's Republic of China sasa mfunge uchuuzi njooni tuzalishe vyetu tuchuuze huko nje.
 
Mkuu mauzo yake sio mazuri, shilingi elfu 40 akishalipia kodi ndio biashara itaenda vizuri.?

Me ningemshauri abadilishe biashara kwa kuuza bidhaa za vyakula kipindi watu wakiwa na kipato kidogo. Kuliko kuendelea kuuza mashuka na mapazia.
Mkuu

Hata kwenye biashara ya chakula napo mambo sio mazuri ki vile.

Sasa hivi watu wanakula milo 2 kwa siku na pia mezani mboga ni moja tu sio mboga 3 tena kama zamani.
 
Mkuu

Hata kwenye biashara ya chakula napo mambo sio mazuri ki vile.

Sasa hivi watu wanakula milo 2 kwa siku na pia mezani mboga ni moja tu sio mboga 3 tena kama zamani.

Mkuu namaanisha biashara za vyakula zina nafuu kidogo kwa kutoka kwani ni lazima watu wale hata kama ni mlo 1 ukilinganisha na bidhaa kama nguo, vifaa vya ujenzi wakati wa kufunga mkanda.
 
Ki ukweli hali ni tete nina vijana wangu wapo shule za boarding za binafsi nimeshawapa angalizo kwamba mwakani wanakuja shule za kata a.k.a Kayumba
 
Mkuu

Hata kwenye biashara ya chakula napo mambo sio mazuri ki vile.

Sasa hivi watu wanakula milo 2 kwa siku na pia mezani mboga ni moja tu sio mboga 3 tena kama zamani.
Hahaaaa huku ni kuisoma namba sikuhizi bar kweupe kweli hali ngumu tutanyooka tu bila kupenda
 
Pole sana mkuu.

Kwa kifupi hali ni tete sana sasa hivi.

Vile vile yakupasa ubadili hata lifestyle yako, kama ulikuwa unapata milo 3 kwa siku, sasa hivi kula milo 2.
[emoji122] [emoji122] [emoji122] umenipa ujuzi
 
Back
Top Bottom