Biashara yangu inaniingizia faida ya Tsh. 200,000 kila mwezi; Je, Niiache niende chuo?

The CIA

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2017
Posts
479
Reaction score
479
Wakuu habari zenu,. Mwaka 2014 nilihitimu kidato ya sita shule mojawapo nchini, nikafanya application kuingia chuo kikuu nikachaguliwa kwenda kusoma course ya uchumi pale udsm.

Kwa bahati mbaya sikupata mkopo kutoka HESLB kwa ajili ya kuniwezesha kupata elimu hiyo ya juu,

Nikatazama nyuma na mbele nikagundua sina support kutokana na umasikini uliokithili ndani ya familia yangu,

Baada ya hapo nikachukua maamzi magum, nikasafiri kutoka mkoani mpaka jijini na nikafuta na kufuta kabisa mawazo ya hiyo elimu ya chuo kikuu kwanza kwenye ubongo wangu.

Mawazo yangu na bongo langu nikahamishia kwenye neno "ajira" nikaanza kutembeza bahasha la vyeti vyangu ya secondary kutafuta ajira hapa mjini, hata hivyo sikuweze kupata ajira baada ya kuzunguka sana na bahasha hapa jijini,. Baada ya changamoto hiyo ikanifundisha tena kubadili mawazo kutoka kutafuta ajira mpaka kutafuta "mtaji" ili nijiajiri, nikiwaza ni jinsi gani niachane na suala la kutembeza bahasha kila ofisi naonekana kama bango,

nikaamua kukusanya kamtaji kwa kuanzia na kale kale ambako nilikuwa nazunguka nako kutafuta ajira nikapiga vibarua vya hapa na pale, nikasaidia sana mafundi site mbalimbali, nikapata kamtaji, nikaachana kwanza na vibarua nikaanzisha biashara fulani.

kwa sasa biashara yangu hiyo inanilipa faida tasilimu ya shilingi laki mbili kila mwezi, na mpaka dakika hii nimeweza kukusanya ada ya kuweza kujilipia university nchini.,

Je niende chuo au niendelee na biashara yangu hii.

NB nikimuachia mtu kuisimamia hii business lazima ife ndani ya muda mfupi sana maana inahitaji kujitoa sana. Japo kulingana na hela niliyonayo cash lazima chuo nimalize bila wasiwasi kabisa..

Naombeni ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakushauri fanya biashara mpaka pale utakapoona IPO stable ata kumwachia mtu,. Swala kusoma limebaki kwenye vitabu, application yake ni kama tu utaiweka kweny kujiajiri lakini kam utatumia nguvu nying kusoma sasa kuna uwezekano ukapoteza vyote ukarudi kweny msoto, ur still young kama umeweza kujiingiza kweny biashara ukafanika, elimu unayoitaj apo ni ndogo sana,.. So jitaidi biashara iwe stable kwanza then ujipe majukumu mengine,
 
University ni hiyo biashara yako dont get twisted,hiyo ada ulinayo igeuze mtaji kisha fungua project nyingine...chuoni hamna kitu kule...kama ni kupata elimu utakua unasoma online ukiwa kwenye mambo yako,vitabu vyote vinavyotumika vyuoni viko kwenye mtandao tena bure.
 
Okay, ASANTE kwa ushauri ngoja tusubiri mawazo ya wengine pia tuamue kwa pamoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu chuo kipo hakiondoki kipo tu na kitaendelea kuwepo. Kuza mtaji anzisha mfumo ambao hauto tegemea uwepo wapo ili biashara iende, ongeza biashara nyingine ili uwe na chanzo cha mapato zaidi ya kimoja. Halafu ndio uende chuo kumalizia masomo,
 
Aisee! Very touching, biashara yangu na mtaji wangu ndo university.
ila napatamani nikiamini nikihitimu nitaanza kutembelea STK

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado wewe sio mjasiriamali kama hata baada ya kufika hapo still unawaza kukaa darasani :
Kajifunze upya maana halisi ya kuwa mfanya biashara :
You are still a self employed personnel. You need to be a real businessman in thoughts & actions.
 
Aisee! Very touching, biashara yangu na mtaji wangu ndo university.
ila napatamani nikiamini nikihitimu nitaanza kutembelea STK

Sent using Jamii Forums mobile app
Fikiria kutembelea Buggati,achana na mikweche ya toyota iliyobandikwa no STK.

Kiuhalisia vyuo vya tanzania tunapoteza muda,kwa mtu kama wewe ambaye ulijiongeza namna hiyo,kwanza mpaka hapo una master degree,sababu hao walioenda university wenyewe wako mtaani eti hawajui cha kufanya,sasa hiyo ni akili au ujinga,yaani mtu ana degree halafu anailaumu serkali eti imeshindwa kumpa ajira
 
Bado wewe sio mjasiriamali kama hata baada ya kufika hapo still unawaza kukaa darasani :
Kajifunze upya maana halisi ya kuwa mfanya biashara :
You are still a self employed personnel. You need to be real businessman in thoughts & actions.
Hata hivyo sijasema nimewahi kuwa mjaliamali au mimi ni mjasiliamali, umeninukuu vibaya. Sina specialisation mpaka sasa ndiyo maana nimekuja kuomba ushauri.

Soma post upya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…