Biashara yangu inaniingizia faida ya Tsh. 200,000 kila mwezi; Je, Niiache niende chuo?

japo lugha ni tofauti lakini walau leo nimeona some glimpses za JF ya zamaaani......mahala ambapo palikua very challenging na mada zinazobadili mitazamo kabisa.
asanteni wadau
 
bill gates aliacha masomo akafanya biashara, saivi anampa magufuli msaada wa kuendesha nchi

usiache hiyo biashara, vyuo vya tanzania ni theoretical rather than practical.

namaanisha nini?

utakachopata chuoni hakitakusaidia sana nje ya chuo kama hiyo biashara yako
 
Yani nakushangaa sana!! unataka uende chuo??

Unahabari wataalam tanzania hasathaminiki??

Unajua magufuli anataka kuazima wataalam wa IT rwanda?

Unajua tunataka kuazima wataalam wa umwagiliaji Misri?

Mbaya zaidi wataalam hawa wapo na hawatumiwi!! sasa wewe unataka kwenda kusoma daah haya kila la heri!!

Kuliko uende chuo bora uende kwenye darasa la forex la ontario ukajifunze forex au usome chochote online!!
 
Kabla sijamaliza kusoma comment za wengine, nimeamua kukoment, binafsi ni mtumishi wa umma, lakini nawaza laiti nimgekomea darasa la saba, kidato cha nne au situ tu naamini ningekuwa mbali sana, nakuhakikishia usitamani kwenda kukaa darasani kusoma kwani lengo la kusoma ni hatima yake kuwa na maisha mazuri, lakini ni wasomi wachache wenye maisha mazuri. Kwa historia yako wewe unatoka kwenye familia sawa na mimi, sasa nakuomba inama umshukuru Mungu kwa ulipofikia, KAZI ZA KUAJIRIWA HASA SERIKALINI NI ANUANI TU NA SIVINGINEVYO yaani ujulikane kuwa huyu ni mfanya kazi maahala fulani ila HAMNA KITU. Kama unatamani kusoma naamini ukisha kaa sawa unaweza kwenda ukasoma hata kwa lesure tu, ila usiende kusoma as a way of solving your problems. Ujasiriamali ni zaidi ya kazi za kuajiriwa. Kama post yako ni kweli basi usijiroge kwenda kusoma ukaacha biashara yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tsh 200,000/= kwa mwezi?? Faida ya Tsh kwa mwezi inakuwezesha ukusanye pesa inayotosha kulipia ada ya Chuo kikuu kwa miaka mitatu?? Au ulimaanisha TSh 2,000,000/=

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana wazee wetu hawakukosea kutuaminisha hivyo, ila nyakati zao ni tofauti sana na nyakati zetu, mfn aliyekuwa na elimu ya darasa la nne soon after independence alikuwa mtu wa maana sana, after independence wazee wetu hawakuzidi milion tisa kwa idadi, leo we are talking of 50 milions and above, tafsiri yake ni kwamba many things are outdated and not applicable any more though they are still our pillar we can not ignore them. Hivyo kwa leo kuwekeza kwenye Booksh Education haina uzito km zamani japo ina umuhimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana wazee wetu hawakukosea kutuaminisha hivyo, ila nyakati zao ni tofauti sana na nyakati zetu, mfn aliyekuwa na elimu ya darasa la nne soon after independence alikuwa mtu wa maana sana, after independence wazee wetu hawakuzidi milion tisa kwa idadi, leo we are talking of 50 milions and above, tafsiri yake ni kwamba many things are outdated and not applicable any more though they are still our pillar we can not ignore them. Hivyo kwa leo kuwekeza kwenye Booksh Education haina uzito km zamani japo ina umuhimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nachokushaur panua profit ya business yako then nenda kasome profit ikifka hta laki tano itakua poa hta kwa huyo utakayemwachia ambaye hana uchungu na biashara yako kama weww
 
mkuu usijichanganye..wapo wengi tu wenye mashahada yao wala hawajui wayafanyie nini..yani wapo tu....elimu ni muhimu ila kwa kizazi hiki,kupata ajira ni kizaazaa..navyokushauri wewe endelea na biashara yako...kwani unataka usome ndio iweje?..unataka usome ndio mwishowe upate ajira ikusaidie kupata hela...kama ndio hivo basi komaa na business mzee baba....usipoteze fursa ila itumie kutengeza jina lako katika business
 
Kama wewe ni mtu wa kujisomea vitabu nakushauri jisomee vitabu hasa kuhusu hiyo field yako. Fikiria jinsi ya kupanua mtaji wako na kupanua biashara.

Elimu utaitafuta baadae ukishastabilize biashara yako.

Kwa sasa elimu ya chuo ni kwa ajili ya pride tu kwamba ulienda chuo. Otherwise you can get more than a degree holder has by reading books at home while pushing your business.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilifikiri utafundisha wengine jinsi ya kupata hiyo laki mbili Kwa mwezi coz ndio kazi ya jamii forums kumbe issue ni hiyo,basi achana na mambo ya chuo pigana hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kuleta hii mada hapa ni somo tosha. Naamini kuna watu wengi tutatoka hapa tumepanuka mawazo. Na yeyw akitoka hapa lazima apanuke kifikra na najua kuna siku atafungua Uzi mwingine kufundika wengine jinsi alivyoanza kutengeza milioni kutoka laki 2 kwa mwezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujuzi wote upo kwenye vitabu. Atakachokufundisha professor lazima kipo kwenye vitabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba chuo ndo kila kitu nenda kasome hizo kazi zipo tu
Chuo ni kila kitu kwa wenye mawazo ya kuajiriwa tu. Kwa hapa jamaa alipofika anahitaji kuongeza ujuzi wa jinsi ya kupanua biashara yake, kitu ambacho anaweza kukipata kwenye vitabu. Akishafikia malengo fulani anaweza kurudi shule ile na yeye atambulike kwamba ana digrii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka mwaka huu uanze umeshajisomea vitabu vingapi mkuu?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…