Biashara yenye faida kubwa kwa mtaji wa Tsh milioni 15-20

Biashara yenye faida kubwa kwa mtaji wa Tsh milioni 15-20

Hiyo ya kutoa mkataba kwa boda boda kuna changamoto gani kubwa , nafikiria kuifanya mambo yakienda vizuri hivi karibuni
Usiifanye Kaka bodaboda woote ambao hawana pikipiki sio waaminifu wengi walio waaminifu tayar Wana pikipiki zao. Watakusumbua
 
Habari wakuu,

Naomba ushauri wa biashara nzuri kwa mtaji wa sh ml.15 mpaka 20.

Mara ya kwanza nilikuwa nafanya biashara ya bodaboda kwa mkataba, nanunua nawapa vijana baada ya miezi 12 inakuwa ya kwake, hii biashara kwangu ishakuwa changamoto sana.

Naombeni mawazo yenu mbali mbali kwa biashara ipi naweza kufanya maana mimi sio mzoefu ya biashara nyingi nilikuwa kwenye biashara moja tu, najua kwa ushauri wenu naweza kupata pakuanzia na kila changomoto kwa biashara husika.

Asanteni
Hata hivyo nakupongeza hela yako haijafa kwenye pikipiki,hiyo kazi Ina changamoto Sana kwasababu madereva wengi waaminifu Wana pikipiki zao,ukiona dereva Hana pikipiki ana matatizo niamini Mimi.
 
Wakati unatafakari biashara ya kufanya ya kudumu,, Njoo huku kilwa Nanjilinji huu ni msimu mavuno ya zao la ufuta, unanunua kwa wakulima kwa kg moja 1500, unauza kwenye mnada shs 2800 kwa kilo moja. Ndani week moja Unapata pesa yako...Ufuta hauna shida kama Korosho watu wanapiga pesa kimya kimya huku..! Au pia Fursa nyingine Nunua pikipiki ya Tairi itatu, (Maguta) unanunua mawili yenye Thamani ya Shs 12,500,00. Unakuja kupiga pesa huku, Unatoa mazao mashambani unaleta mjini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama unaweza fungua ka microfinance kadogo ukopeshe mfano
100k kwa asilimia 30-40 inadependi na wewe mwenyewe hawa wanarejesha kila siku 4500 au 4000 inalipa (haikosi changamoto)

au
fungua wakala wa bank na mitandao (tafuta location nzuri huko ulipo unaweza ukapata hapa location mbili... upae vijana waamifu na uee makini unaweza weka na gesi hapo hapo

au
kama uko dar fungua duka la nafaka kama ni mkoani mkoa ulipo anza kusafirisha mchele to dar ila uwe makini nayo

fungua duka ka spea za pikipiki na vifaa vingine
au
kanunue bond UTT au BOT

au kaweke Fixed kwenye bank inayotoa commision nono
Biashara zote ulizomshauri hapa ni biashara kichaa
 
Mkuu kwani PM hata wewe si unaweza fika?AU sote hatuwezi kufika PM?
Weka hadharani watu wote wapate mwanga na pia waweze kutoa mawazo yao ili kuboresha zaidi hiyo biashara.

Kuitana pm kwa haraka hivyo haswa kwa mambo ya ngawira kunaleta kujiuliza.
 
Weka hadharani watu wote wapate mwanga na pia waweze kutoa mawazo yao ili kuboresha zaidi hiyo biashara.

Kuitana pm kwa haraka hivyo haswa kwa mambo ya ngawira kunaleta kujiuliza.
Mkuu,sio kila business idea ni kwa ajili ya Mass consumption
 
Wakati unatafakari biashara ya kufanya ya kudumu,, Njoo huku kilwa Nanjilinji huu ni msimu mavuno ya zao la ufuta, unanunua kwa wakulima kwa kg moja 1500, unauza kwenye mnada shs 2800 kwa kilo moja. Ndani week moja Unapata pesa yako...Ufuta hauna shida kama Korosho watu wanapiga pesa kimya kimya huku..! Au pia Fursa nyingine Nunua pikipiki ya Tairi itatu, (Maguta) unanunua mawili yenye Thamani ya Shs 12,500,00. Unakuja kupiga pesa huku, Unatoa mazao mashambani unaleta mjini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Apo kwenye ufuta tayari ishajulikana kama bei ya kuuza ni 2800 kwa kilo??
 
Upo sahihi kabisa aisee, yaan madereva wengine wanasumbua sana. Anaweza asilete rejesho hata la wiki nzima mpaka muanze kutaftana.
Hata hivyo nakupongeza hela yako haijafa kwenye pikipiki,hiyo kazi Ina changamoto Sana kwasababu madereva wengi waaminifu Wana pikipiki zao,ukiona dereva Hana pikipiki ana matatizo niamini Mimi.
 
kuna jamaa yangu mmoja alijifanya amepata hela kadhaa aanze kuimport vipodozi toka Nairobi, mwanzoni alipata faida, ila alipoingia mkenge alichofanywa TFDA/TMDA hatakuja asahau. kuna biashara zina faida ila zina risk balaa.
 
Nenda mbeya wilaya ya mbalizi kijiji kinaitwa ISUTO, nunua kahawa wanauza donya moja 300 , debe 7000 mbichi na zilizokauka 10000 , nunua mashine ndogo ya kuzibangua then uza kwa 50 elfu mpka 60 kwa kampuni ya Olden iliyoko mkoa wa songwe kijiji cha Iwowo.

Ushauri tu.
TEKERI.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Usijaribu hii kitu utalia kilio cha mbwa mwitu...utapiga ukunga uwo mpakaa akili ikukae sawa...
 
Habari wakuu,

Naomba ushauri wa biashara nzuri kwa mtaji wa sh ml.15 mpaka 20.

Mara ya kwanza nilikuwa nafanya biashara ya bodaboda kwa mkataba, nanunua nawapa vijana baada ya miezi 12 inakuwa ya kwake, hii biashara kwangu ishakuwa changamoto sana.

Naombeni mawazo yenu mbali mbali kwa biashara ipi naweza kufanya maana mimi sio mzoefu ya biashara nyingi nilikuwa kwenye biashara moja tu, najua kwa ushauri wenu naweza kupata pakuanzia na kila changomoto kwa biashara husika.

Asanteni
IDO, BASE OIL, CONDI SET, SLAGE NA OIL CHAFU huko ni pesa tupu
 
Back
Top Bottom