Biashara yenye faida kubwa kwa mtaji wa Tsh milioni 15-20

Njoo na hela ndogo kwanza nikufundishe Namna ya kuflip pallets za kutoka Amazon kwa huku Africa.

Nenda YouTube jifunze Namna ya how to flip liquidation pallets and make money then nitakwambia wapi ukanunue kwa Bongo utengeneze pesa ambayo itakushangaza. Uje uanze na million tu! Then utaona direction yako inakupeleka wapi.

Nimepiga pesa saana, kwenye Hii arena na na Hadi muda huu sitoi ramani kirahisi Hadi nitoboe ili watu wasiwe wengi tukaflood market.

It's a multi billion dollar business.
 
kawombe Ntemii
Base oil, OBM na condiset ni mafuta yanayotumika kwenye kuchoronga miamba wakati wa utafiti na gesi na mafuta ardhini na baharini.. Yakishatumika huwa na matumizi mengine mbadala viwandani
Slage (sina hakika na spelling) ni mabaki ya mafuta meli za mafuta zinaposhusha mafuta, pia inapatikana kwenye yale matank makubwa ya kuhifadhia mafuta

Oil chafu inajulikana
IDO ni industrial Diesel Oil inayopatikana kupitia mvuke wa tairi zilizochomwa
 
MC kwenye sherehe. Mtaji suti na Microphone hainaga Kodi za TRA
 
Soko linapatikanaje mkuu? Na malighafi yananunuliwa wapi?

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
Mara ya kwanza nilikuwa nafanya biashara ya bodaboda kwa mkataba, nanunua nawapa vijana baada ya miezi 12 inakuwa ya kwake, hii biashara kwangu ishakuwa changamoto sana.
Ungefafanua juu ya hizo changamoto ili wadau wajifunze na wakupe idea zao..
Kuna wengine wanafanikiwa huko huko ulipokutana na changamoto!
 
NUNUA ARDHI IPIME KISHA UZA VIWANJA UTAZALISHA MARA DUFU NA HAINA HASARA TOFAUTI NA BIASHARA NYINGINE YOYOTE
 
Hii idea iko nje ya guidelines za uzi lakini ntachangia kidogo.
Hii unanunua bidhaa zilizorudishwa nawateja, mara nyingi zinakuwa mpya lakini ile packaging imefunguluwa, kwa hiyo amazon, ebay , etsy wanaziuza kama used products kwa bei ya chini kuanzia asilimia 10-40%.
Hizi zinapatikana kwa wingi marekani kwa sababu ecommerce volume ya huko ni kubwa.
Nafikiria changamoto kubwa ni usafirishaji kutoka marekani kuleta Africa vile vile bei za vitu vinavyouzwa marekani online vinakuwa ghali zaidi kulinganisha na nchi kama china au UAE, kwa hiyo utapata discount kwa american market, lakini ukivileta africa au UAE vitakuwa haviuziki.
Hapa UAE ipo amazon online warehouse wanauza hizo used products lakini bei haziko chini sana, uae used market unapata bei za chini zaidi kuliko za amazon warehouse.
Kwa ufupi hii idea ni nzuri sana kwa market ya marekani. Kwa market za Africa bora usogee UAE au nenda Alibaba.
Kwa maelezo zaidi nunua kitabu nimekiattach na huu uzi
 

Attachments

  • 184C22E5-951B-41F3-B73E-A5B97576B1F8.jpeg
    39.4 KB · Views: 114
hizi ndo hoja sasa za kusaidia watu
 
hii pesa ni nyingi sana kiasi kwamba kwa mwezi inaweza ingiza ml 3 kwa makadilio ya chini kama utaanzisha biasharq yq nafaka kwa kununua na kuuza kwa bei ya jumla! ninaifanya na ninaona matunda yake, mm ni mfanyakazi hvyo siend kununua mm ila kuna jamaa anafata mzgo analeta tunauza ni mwz wa pil sasa na nmeanza tayar bei ikiwa juu lkn nashukuru mungu sana
 
Mimi nataka niifanye hiyo ya kuwapa bodaboda pikipik Kwa mikataba, nisaidie changamoto na faida zake tafadhar
 
Nimejaribu kukufuata PM, nimeshindwa, system inaniambia I don't have enough permission to PM. Please nicheki PM kuhusu sources zinazo weza kuwa profitable kwa Bongo
 

Mkuu unanua kijijini (location) na soko linakuwa wapi (location)
 
Biashara zote ulizomshauri hapa ni biashara kichaa
Kama hiyo ya kuwakopesha watu ndio uwendawazimu kabisa,kipindi hiki sio cha kuwapa watu pesa halafu usubirie wakurudishie.
Angalau kidogo hiyo ya spea za pikipiki inaweza kumsaidia kwa vile ana uzoefu nazo na pia anajuana na waendesha bodaboda atapata connection kwa urahisi.
 
Hii post imenichekesha sana hasa hapo mwishoni imekaa kimtegomtego sana.
Anasema hataki watu wengi lakini kaja kuitangaza.
Yaani ni sawasawa mtu anakuita anakwambia njoo nikwambie kitu lakini ni siri usimwambie mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…